Mafanikio ya Rais Magufuli: Viva Rais Magufuli, viva Tanzania

Hutaki unaacha. Huo ndio ukweli. Wanamkubali kimoyo moyo na wanamtaja kimoyomoyo. Wakitoka nje wanajifanya kumsema vibaya. Nampa Tano Magu. Namshauri ashikilie hapo hapo
 
Wakuu huu ni uzi maalumu wa kuunga mkono juhudi zinazofanywa na rais Magufuli katika kuinua uchumi wa nchi pia katika kuelekea Tanzania ya viwanda.Katika uzi huu tutaelezea juhudi zote zinazofanywa na Magufuli katika kuleta maendeleo
 
Mtu ameshaitia hasara nchi kwa kununua ferry ya Sh4 billion yeye kauziwa sh8 Billion!
Kesi ya samaki na Meli ya China serikali inadaiwa zaidi ya sh3 billion.

Kule Mwanza Halmashauri ya jiji ililipishwa mamilioni kwa amri yake ya kubomoa kituo cha mafuta.

Bado hujazungumzia nyumba za serikali walizouziana.

Bado hujazungumzia uwanja wa ndege chato usio na faida kwa Taifa
Bado unatafuta hasara gani zaidi.
Mungu epushia mbali

Sent using Jamii Forums mobile app
 
wakuu huu ni uzi maalumu wa kuunga mkono juhudi zinazofanywa na rais jpm katika kuinua uchumi wa nchi pia katika kuelekea Tanzania ya viwanda.Katika uzi huu tutaelezea juhudi zote zinazofanywa na jpm katika kuleta maendeleo
@admin2 uko wapi nyuzi za hivi zimekua nyingi hadi zinaboa
 
wakuu huu ni uzi maalumu wa kuunga mkono juhudi zinazofanywa na rais jpm katika kuinua uchumi wa nchi pia katika kuelekea Tanzania ya viwanda.Katika uzi huu tutaelezea juhudi zote zinazofanywa na jpm katika kuleta maendeleo

Nyuzi kama hizi zimeshaletwa nyingi hapa jukwaani,kuliko kuendelea kuzileta hapa bora ungeandaa maandamano ya kumpongeza kwa kuvunja dirisha la bweni alipokuwa kidato cha Tatu Katoke seminari.
 
Mhe Rais amefanya vizuri sana kwenye maeneo mengi nitataja machache kama promotion, new recruitment, transfer, uhakiki kwa watumishi wa umma, milion 50 kwa kila kijiji, democracy, viwanda (vyerehani 4), bunge live, mikutano ya kisiasa, kuwapenda matajiri kama akina Manji, Ruge, Masamaki n.k
 
Kwa jinsi maisha yalivyo magumu na anayesababisha kwa kiwango kikubwa asilimia 60% ya watanzania kila siku somewhere lazima wataje jina la MAGU labda kwa mazuri au mabaya
 
Back
Top Bottom