Mafanikio ya Rais Magufuli: Viva Rais Magufuli, viva Tanzania

Ila mwendo wa dreva wa gari hii safari hii tumepatikana!gari ni spidi na ukizingua anakushusha popote hajali ni mikumi au kibiti anakushusha tu!walah tutanyooka tu,ila jamaa nao wametuibia sanaaaa,ikiiisha miaka 5 "bwana yule" atabaki na "yule bwana" tu ofisini,sioni msafi atakae pona kushushwa kwenye hili tipa!!!
 
Tunabaki kuwa ma maswali mengi ambayo yote hatuna majibu,hivi haya mambo siku zote katika kipindi cha mzee wa Lushoto na yule wa Bagamoyo haya mambo yalikua hayaonekani au ndio hivyo tulukua tunafanya kazi kwa mazoea...Kweli Tanzania ni zaidi ya uijuavyo
 
Dereza tumwage!Dereva tumwage!Dereza tumwage!Dereza tumwage! Daah raha sana kama vile zile safari za macamp kwenda coco beach siku za keekend miaka ileee ya 2000
 
Naona watu leo wanashangilia Sana ripoti ya mchanga wa madini na kuona kwamba JPM ni mzalendo kweli kweli

Lakini nionavyo wizi wote wa Mali ya umma ,dhuluma yote ya Mali za umma ni uzao wa CCM na tawala zake

Suala la madini lilishapigiwa sana kelele na upinzani mikataba iangaliwe upya wakapuuzwa
Tumeibiwa Sana tunakumbuka shuka kumekucha halafu watu wanaanza kuwasifia watu walio ndani ya chama kilichosababisha wizi wa rasilimali zenu.
 
Unajua watu wa lumumba wanapiga mziki halafu wanacheza wenyewe, walitakiwa wajitathimini pia wajiulize yote haya yamefanywa na akina nani? ?
 
Back
Top Bottom