Mafanikio ya Rais Magufuli: Viva Rais Magufuli, viva Tanzania

Ndugu wana JF kama mada inavyohusika katika somo tajwa hapo juu. Mheshimiwa Rais anasimamia UKWELI na kuongea UKWELI kila anapopata wasaa. Sisi watawaliwa tunampongeza kwa kusimamia UKWELI na kuishi katika UKWELI. Swali ama swala gumu hapa ni UKWELI according to Mh. Rais ni UPI?? Nakumbuka alipokuwa kwenye ziara yake kanda ya ziwa alisema UKWELI kuwa nchi yetu haina njaa na watu walime, wafanye kazi..yeye hatatoa chakula cha msaada kwa ajili ya njaa. Ni kweli watu wameishi na wanendelea kuishi na hakuna laiyekufa kwa njaa. Ikatangazwa na hata na wasaidizi wake akiwemo Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani kuwa atakayesema ama kutangaza kuna njaa atakamatwa na kufunguliwa mashtaka. Kwa sisi wanachama wa chama chetu tulimuamini kabisa.

Ikaja issue ya Uvamizi wa Kituo cha Clouds TV..Waziri akajaribu kutafuta na kulaani kile kilichotokea kwa kuweka UKWELI wa mambo hadharani..ambao haukuwa sawia na imani ya UKWELI anaouamini Mh. Rais.

Ikaja hili la Mchanga wa Madini sasa..akasema UKWELI alipokwenda Bandarini kuwa ni makontena yana dhahabu kwa asilimia zaidi ya 90. Mkurugenzi wa bandari akamuunga mkono Mh. Rais na kuunga mkono UKWELI huo. Mh. Rais ameambiwa UKWELI na wanaosema UKWELI katika kuvumbua sakata hili.

Spika wa Bunge akapitia maeneo ya bandari kwa minajili ya kukariri UKWELI wa Mh. Rais na ni kweli akakutana na UKWELI kutoka kwa Eng. Kakoko juu ya madini kwenye kontena UKWELI aliorithi kwa Rais wangu. Mteule wa Rais tena Prof Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na madini akaamua ku reason kama msomi..alikosea kutaka kuhakiki/kuhoji UKWELI wa Mh. Rais. Alishauri tu kuhakiki kwa kufungua na kufanya vipimo kwa sampuli za makontena yaliyopo hapo bandarini. Kilichotokea kinafahamika japo labda yapo mengine kando kando yaliyosababisha utenguzi wake. Hata hivyo Waziri Mkuu ameshachukua sampuli na uchunguzi unafanyika.

Pia Mh. Rais anautafuta UKWELI kwa kuunda kamati kutafuta huo UKWELI ambao Professor alitaka utafutwe..Nina uhakika UKWELI anaouamini Mh. Rais utapatikana tu kama ulivyokuwa. Na tume ijitahidi ipate UKWELI unaofanana na UKWELI wa Mh. Rais na si vinginevyo. Namtakia kila la heri Mh. Rais katika kuweka mambo sawa na kuupata UKWELI wa mambo meengi ya Tanzania. Msema KWELi ni mpenzi wa Mungu.

Nawasilisha.
Sasa kama akili zenu zinafanana lazima tu mtafurahiana matendo yenu!
 
Mwinyi,Mkapa,Kikwete hakuna hata mmoja aliyesifiwa akiwa madarakani.Wamemwagiwa sifa baada ya kuondoka.Alivyotukanwa Kikwete huwezi kuamini Leo anasifiwa.Watamsifia Magufuli baada ya kuondoka.Kama kuna upungufu ni wa kibidamu.Hakuna mkamilifu.Kama isingekuwa Magufuli nani basi mwingine anayefaa.Wakati wa uchaguzi mkuu tulikosa.Hata sasa Mimi sioni mwingine.Anayemjua mwingine zaidi ya Magufuli anitajie.
 
Mwinyi,Mkapa,Kikwete hakuna hata mmoja aliyesifiwa akiwa madarakani.Wamemwagiwa sifa baada ya kuondoka.Alivyotukanwa Kikwete huwezi kuamini leo anasifiwa.Watamsifia Magufuli baada ya kuondoka.Kama kuna upungufu ni wa kibinadamu.Hakuna mkamilifu.Kama isingekuwa Magufuli nani basi mwingine anayefaa?.Wakati wa Uchaguzi Mkuu tulikosa.Hata sasa Mimi sioni mwingine.Anayemjua mwingine zaidi ya Magufuli anitajie.
 
Q
 
Duuh itakua viatu vya bora
 
ungeweka sifa za rais bora halafu ungezioanisha na rais wetu magufuli kutokana na uhalisia hapo ningekuelewa lkn hizo umeweka mbwembwe tu
 
Katika historia, Tanzania wala Africa nzima haijawai kupata rais anayesifiwa na mataifa yote ulimwenguni...Magufuli ni wa kwanza...ardhi ya tanzania imetoa zao linaloangaza na kutumika kama mfano dunia nzima...
 
Mwinyi,Mkapa,Kikwete hakuna hata mmoja aliyesifiwa akiwa madarakani.Wamemwagiwa sifa baada ya kuondoka.Alivyotukanwa Kikwete huwezi kuamini leo anasifiwa.Watamsifia Magufuli baada ya kuondoka.Kama kuna upungufu ni wa kibinadamu.Hakuna mkamilifu.Kama isingekuwa Magufuli nani basi mwingine anayefaa?.Wakati wa Uchaguzi Mkuu tulikosa.Hata sasa Mimi sioni mwingine.Anayemjua mwingine zaidi ya Magufuli anitajie.
Nahisi utakuwa umetoroka milembe hebu rudi kwanza ukamalize dozi
 
Back
Top Bottom