Viungo vya Mtoto wa Kijapani vyaponesha wagonjwa...! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Viungo vya Mtoto wa Kijapani vyaponesha wagonjwa...!

Discussion in 'Jamii Photos' started by MziziMkavu, Jan 4, 2012.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Jan 4, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  [TABLE="class: tborder, width: 100%, align: center"]
  <tbody>[TR]
  [TD="class: alt1, bgcolor: #FFFFFF"]

  Madaktari nchini JAPANI wameondoa viungo kutoka kwa mtoto mwenye umri wa chini ya miaka 15 ambaye ubongo wake ulikufa kwa ajili ya upandikizaji.Mtoto huyo alikuwa akitibiwa katika hospitali moja katikati ya jiji la TOKYO hadi juzi Jumanne alipofariki na viungo vyake kuonekana kufaa kwa upandikizaji.

  [​IMG]

  Wazazi wa mvulana huyo walisema katika tamko lao kuwa hawakuwahi kuzungumza kuhusu uchangiaji wa viungo na mtoto wao lakini wanafikiri kuwa kuwasaidia watu kuishi kwa kutumia viungo vya kupandikiza kunaweza kukidhi matarajio yake. Jana Jumatano kazi ya kuondoa viungo ilifanyika ambapo moyo, mapafu , maini , figo na kongosho viliondolewa hadi kufikia asubuhi ya jana.

  [​IMG]

  Hii leo Alhamisi kazi nzima ilikuwa imekamilika. Moyo uliotolewa kwa kijana huyo umepandikizwa kwa mvulana mmoja wa umri wake aliyekuwa na matatizo ya moyo katika hospitali ya Chuo Kikuu cha Osaka huko Suita , mkoa wa Osaka , mapafu yametumika kumpandikiza mwanamke mmoja mwenye umri wa miaka 50 aliyekuwa akisumbuliwa na tatizo la Shinindizo la damu katika mapafu ‘pulmonary hypertension’ katika operesheni iliyofanyika katika Hospitali ya Chuo Kikuu cha Tohoku huko Sendai na maini yalipandikizwa kwa mwanaume mmoja mwenye miaka 20 aliyekuwa na ugonjwa wa umetaboli wa ini ‘metabolic hepatic , operesheni iliyofanywa katika hospitali ya Chuo Kikuu cha Hokkaido.

  [​IMG]

  Moja ya figo yake na kongosho zilipandikizwa kwa mwanamke mmoja mwenye miaka 30 aliyekuwa na tatizo la sukari katika figo zake katika hospitali ya Chuo Kikuu cha Fujita huko Toyoake karibu na Jiji la Nagoya mkoani Aiichi wakati figo ya pili imepandikizwa ma mwanamme mmoja mwenye miaka 60 aliyekuwa akiugua tatizo sugu la figo na operesheni hiyo imefanyika katika hosptali ya Chuo Kikuu cha tiba za wanawake jijini Tokyo.
  Hivi vitakuwa viungo vya kwanza kwa ajili ya kupandikizwa kutoka kwa mchangiaji mtoto nchini JAPANI tangu sheria iliporekebishwa mwezi Julai mwaka jana inayoruhusu uchangiaji wa viungo kutoka kwa watoto wa umri wa kati kwa ridhaa ya familia zao.

  Japanese Media..
  [/TD]
  [/TR]
  </tbody>[/TABLE]
   
 2. Chris_Mambo

  Chris_Mambo JF-Expert Member

  #2
  Jan 4, 2012
  Joined: Aug 11, 2010
  Messages: 597
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Very interesting!!
   
 3. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #3
  Jan 4, 2012
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  wenzenu wanafikiria boko haram.
   
 4. Tz-guy

  Tz-guy JF-Expert Member

  #4
  Jan 4, 2012
  Joined: Aug 10, 2011
  Messages: 439
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Duh, hawa watu wako mbali sana.
   
 5. chapaa

  chapaa JF-Expert Member

  #5
  Jan 4, 2012
  Joined: Feb 19, 2008
  Messages: 2,355
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  sie kwetu alivyozaliwa bila kichwa si walimuwekea nazi
  nasikia sku hizi kawa .........
   
 6. Capt Tamar

  Capt Tamar JF-Expert Member

  #6
  Jan 4, 2012
  Joined: Dec 15, 2011
  Messages: 6,660
  Likes Received: 3,311
  Trophy Points: 280
  Msaada jamani kwa anayejua mganga mashuhuri wa ndumba anielekeze kuna mtu huku JF simpendiii nipo mitaa ya msoga tafadhalini jamani.
   
 7. m

  mamanalia JF-Expert Member

  #7
  Jan 4, 2012
  Joined: Nov 7, 2009
  Messages: 671
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Cha kufurahisha zaidi hizo opereshi kubwa zinafanyika kwenye hospitali za vyuo vikuu. Muhimbili/MUHAS kazi yao ni mabingwa wa ku refer mafisadi India.
  serikali imeshindwa hata kuchagua hospitali moja kama ya muhimbili na kuifanya the best angalau hata wao na ufisadi wao waweze kutibiwa wakiwa home. Naomba siku moja mmoja wao afie kwenye ndege akipelekwa India ndo watajifunza.
   
 8. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #8
  Jan 4, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  Eleza sababu kwanini humpendi huyo Mtu wa J.F.?
   
 9. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #9
  Jan 4, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  Ni kweli usemayo lakini kuna Siri kubwa hapo mpaka Serikali imeona bora viongozi wake kuwapeleka india kimatibabu.
   
 10. p

  pilu JF-Expert Member

  #10
  Jan 5, 2012
  Joined: Dec 16, 2011
  Messages: 488
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  nikweli mkuu wako mbali, ndomana hata nauli ya kwenda kwao ni ghali.
   
 11. p

  pilu JF-Expert Member

  #11
  Jan 5, 2012
  Joined: Dec 16, 2011
  Messages: 488
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  siri ipi mkuu!
   
 12. urioglory

  urioglory Member

  #12
  Jan 5, 2012
  Joined: Jan 5, 2012
  Messages: 7
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sisi maskini ndio tutafia hapo muhimbili, wenye hela zao India . Kweli tutafika jamen
   
 13. urioglory

  urioglory Member

  #13
  Jan 5, 2012
  Joined: Jan 5, 2012
  Messages: 7
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sisi maskini ndio tutafia hapo muhimbili, wenye hela zao India . Kweli tutafika jamen
   
Loading...