Viungo vya binadamu sokoni | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Viungo vya binadamu sokoni

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Lutala, Sep 15, 2010.

 1. Lutala

  Lutala JF-Expert Member

  #1
  Sep 15, 2010
  Joined: Jun 17, 2010
  Messages: 845
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 35
  Wahudumu chumba cha maiti wakutwa na viungo vya mwanamke
  Wednesday, 15 September 2010 05:21
  NAIROBI,Kenya

  JESHI la Polisi nchini Kenya linawashikilia wanaume wawili wahudumu wa vyumba vya kuhifadhi maiti kwa tuhuma za kukutwa na viungo vya wanawake.

  Habari kutoka nchini humo zimeeleza kuwa watu hao walikamatwa jana saa 6:30 mchana wakiwa na mfuko wa plastiki ambao ulikuwa umehifadhiwa viungo hivyo ambavyo vinasadikika kunyofolewa katika maiti hospitalini. Imeelezwa kuwa kati ya watu hao mmojawapo anasemekana kuwa ni muhudumu katika chumba cha kuhifadhia maiti katika Hospitali ya Taifa ya Kenyatta na mwingine ni muhudumu katika kampuni moja binafsi inayoshughulika na mazishi iliyopo katika eneo hilo.

  Imeelezwa kwamba watu hao walikamatwa baada ya polisi kupewa taarifa za kuwepo kwa biashara ya viungo vya binadamu na kisha kuvamia sehemu hiyo na kuwakuta watu hao wakiwa na viungo hivyo ambapo haikufahamika walikuwa wakivipeleka wapi.

  Kwa mujibu wa Kaimu Kamanda wa Wilaya ya Kilimani, Johana Chebii,polisi walivamia eneo la maegesho ya gari katika hospitali ya KNH ambako walimshuhudia muhudumu wa chumba cha kuhifadhia maiti akiingia katika gari lililokuwa limeegeshwa eneo hilo na kumkamata kabla hajaondoka.

  “Kulikuwepo na taarifa za kuwa kuna watu wanajihusisha na biashara ya kuuza viungo vya bianadamu.Wapelelezi walikwenda katika hospitali ya KNH na kuvamia ghafla. Mwanamume mmoja alikuwa amebeba mfuko wa rangi ya kijani na kuuweka ndani ya gari na ulipofanyiwa upekuzi ulikutwa na viungo vya mwanamke vikiwa vimefungwa ndani ya karatasi,” alisema Kamanda Chebii.

  Amesema hadi jana jioni Polisi walikuwa wakitafuta maiti ili kubaini mahali viliponyofolewa viungo hivyo.

  Amesema kuwa timu ya wapelelezi ikiongozwa na mkuu wa upelelezi wa Kilimani, Mwenda Italia wanawahoji wanaume hao wawili kuhusu biashara hiyo ya ajabu na ni muda gani tangu wajihusishe nayo.

  Polisi wanaamini kuwa biashara hiyo imekuwa ikiendelea kwa muda kwa sababu watuhumiwa wamekuwa wakinyofoa viungo hivyo na kisha kuondoka hospitali na kirahisi.

  “Hatufahamu endapo biashara hii kama ilikuwa ikiendelea kwa muda mrefu na inawahusisha watu wangapi,"alisema kamanda huyo.

  “Tunatoa wito kwa ndugu za marehemu kukagua miili ya ndugu zao wakati watakapokuwa wakichukua maiti ili kubaini kama wanaviungo vyote vya mwili kabla ya kuzichukua,” aliongeza Kamanda Chebii kabla ya kusema kuwa watuhumiwa watafikishwa mahakamani haraka iwezekanavyo mara baada ya upelelezi kukamilika.
   
 2. Smiles

  Smiles JF-Expert Member

  #2
  Sep 15, 2010
  Joined: Aug 24, 2009
  Messages: 1,231
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Watu wana mambo ya ajabu jamani,
  afu sasa baada ya hapo wanapeleka wapi....?
  na imani zetu zuko wapi....? au wapagani....?
  Mbona inasikitisha....
   
 3. Lutala

  Lutala JF-Expert Member

  #3
  Sep 16, 2010
  Joined: Jun 17, 2010
  Messages: 845
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 35
  Kwa kweli inasikitisha
   
 4. pmwasyoke

  pmwasyoke JF-Expert Member

  #4
  Sep 16, 2010
  Joined: May 27, 2010
  Messages: 3,583
  Likes Received: 189
  Trophy Points: 160
  Ushirikina ni laana ya jamii!
   
Loading...