Viungo bandia vya siri vyauzwa kama njugu Dar | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Viungo bandia vya siri vyauzwa kama njugu Dar

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Boflo, Mar 19, 2012.

 1. Boflo

  Boflo JF-Expert Member

  #1
  Mar 19, 2012
  Joined: Jan 20, 2010
  Messages: 4,394
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Florence Majani | Mwananchi

  KATIKA kile kinachoonekana kuwa baadhi ya wanawake wamedhamiria kumaliza hisia zao za kimapenzi wao kwa wao, biashara ya uuzwaji viungo bandia vya siri vya kiume, imeshamiri jijini Dar es Salaam.

  Mwananchi Jumapili lilifika hadi katika duka maarufu la vipodozi wilayani Kinondoni na kubahatika kuzungumza na muuzaji aliyejitambulisha kwa jina moja la Kelvin ambaye alisema, viungo hivyo bandia vimekuwa vikigombewa kwa kasi pindi vinafikishwa dukani hapo.

  Kelvin alisema, inamuwia vigumu mmiliki wa duka hilo kuwatosheleza wateja wake wengi, wanaoweka oda ya bidhaa hiyo, kutokana na idadi yao kuongezeka.

  “Akileta viungo 50, havikai kwa zaidi ya siku tatu, akileta 70 au 90, havimalizi wiki,” alisema Kelvin.

  Hata hivyo, muuzaji huyo alidai kuwa, kwa sasa hakuna viungo hivyo kwa sababu mzigo bado haujaingia jambo ambalo limesababisha wateja wengi kuulizia kila siku.

  “Kama jana amekuja msanii maarufu wa kike wa nyimbo za taaribu, alikuwa anahitaji viungo, na mbunge mmoja wa kike naye aliviulizia majuzi, lakini ndo hivyo mzigo bado haujaingia,” alisema Kelvin.

  Bei ya viungo hivyo
  Akizungumzia gharama za viungo hivyo, muuzaji huyo alisema, bei inategemea umbile akimaanisha, urefu au upana wa kiungo chenyewe.

  “Kuna uume wenye inchi sita, nane hadi 12, pamoja na ukubwa wa kiuno cha mvaaji, kila moja kina bei yake, lakini kiwango cha kawaida ni kuanzia Sh45,000 hadi Sh 80,000,” alisema muuzaji huyo.

  Kelvin aliwataja wateja wakubwa kuwa ni wanawake maarufu, raia wa kigeni na wanawake waliozoea maisha ya starehe.

  Alisema: “Wanaokuja kununua hapa ni wale watu wa ‘viwanja,’ wengine wale walioshindikana kabisa tunawajua wanavuta bangi na unga, lakini pia wanawake wa kizungu nao huviulizia.”

  Aidha alisema, duka hilo haliuzi viungo vinavyotumia umeme, (vibrator) kwa sababu vinasemekana kuwa na madhara.

  Mwananchi Jumapili lilipotaka kujua ni mahali gani pengine viungo hivyo vitapatikana, jijini Dar es Salaam, kijana huyo alisema, anaweza kwenda kuvipata kwa mama mmoja mkazi wa Msasani ingawa bei itaongezeka.

  Kelvin aliyataja maeneo mengine ambapo viungo hivyo vinaweza kupatikana kuwa ni katika maduka makubwa ya vipodozi ya Kariakoo na Sinza.

  Ili kupata uhakika wa ni lini viungo hivyo vitawasili, muuzaji huyo alitoa namba ya mmiliki wa duka hilo ambaye baada ya kupigiwa, alidai yeye huwa hauzi, lakini humtafutia wateja mwanamke mmoja mwenye asili ya kiarabu, mkazi wa Upanga ambaye ndiye muuzaji mkongwe.

  “Havijawasili hapa nchini siku nyingi, lakini mimi huwa siuzi, namtafutia wateja mama mmoja hivi mwarabu wa Upanga, hata hivyo bado nina bidhaa nyingine kama unahitahi dawa za kuongeza matiti, kuwa mweupe,” alisema mmiliki wa duka hilo.

  Wanawake wanasemaje?
  Baadhi ya wanawake waliohojiwa kuhusu kuongezeka kwa manunuzi ya viungo hivyo, walidai kuwa, hali hiyo inasababishwa na kukata tamaa katika mahusiano.

  Pendo Mallya mkazi wa Tabata jijini, Dar es Salaam, alitaja usaliti wa kimapenzi kuwa ndiyo chachu ya wanawake kuchukua uamuzi wa kununua viungo bandia.

  “Tumechoka kutendwa (heartbroken) , wanaume hawaaminiki, kwa hiyo ili kuepusha kubadili wanaume kila siku, ni bora ujitimizie haja zako mwenyewe,” alisema Pendo.

  Aliongeza kuwa licha ya kuepuka kutendwa na wanaume, lakini matumizi ya viungo hivyo yanakutoa katika hatari ya maambukizi ya magonjwa ya zinaa ukiwemo Ukimwi.

  “Kitu kingine, ni kuwa unakitumia kila unapokuwa na haja, tofauti na mwanaume atakuambia sipo, nimesafiri leo nimechoka na sababu nyingi,” alisema.

  Lakini Edwin Mnzeru alikuwa tofauti na Pendo ambapo yeye aliona wanawake wanaotumia viungo hivyo, wanashabikia ujinga.

  “Hizi ni athari za utandawazi, tujaribu kuiga mazuri, tuyaache mabaya, siyo kila kitu lazima tufanye,” alisema Aliongeza kuwa, serikali inatakiwa idhibiti uingizwaji wa bidhaa zote zinazoonekana kuvunja maadili.

  Mtaalam wa Saikolojia Mtaalamu wa masuala ya Saikolojia kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Richard Msambaiga, aliitaja sababu kuu inayowasababisha wanawake kununua viungo hivyo kuwa ni usaliti katika mapenzi.

  “Mwanamke anapoona anasalitiwa kimapenzi, anaona njia bora ni kujimalizia haja zake mwenyewe, kisaikolojia, anahisi ametibu majeraha kwa kujimiliki,” alisema.

  Aliongeza kuwa, wapo wenye hisia kuwa, kufanya mapenzi mwanamke na mwanaume, ni mfumo dume, hivyo anapopata nyenzo kama hizo, hudhani kuwa ametatua matatizo ya mfumo dume.

  Alizungumzia suala la utandawazi na kusema, umeruhusu kila taka kuingia, hivyo watu wamepata uhuru wa kujichagulia kile wakitakacho kiwe kibaya au kizuri.

  Alisema, wanawake kutumia viungo bandia vya kiume kufanya tendo la ndoa, ni suala la kina lenye sababu chekwa za kisaikolojia, kikubwa kikiwa ni wanawake kukata tamaa katika mahusiano na utandawazi. Nchi za Magharibi Katika nchi za magharibi, uuzwaji wa viungo bandia, umekuwa jambo la kawaida ambapo yapo maduka na kampuni mahususi kwa ajili ya bidhaa hizo tu.

  Hivi karibuni, kampuni za Magharibi ziliibuka na kuanza kuajiri watu watakaoweza kujaribu nyeti hizo bandia kabla ya kuziuza.

  Mmoja wa watu walioajiriwa ni Nat Garvey ambaye hulipwa kiasi cha Sh milioni 50 kwa mwezi kwa ajili ya kujaribu uwezo na ubora wa nyeti hizo bandia za kiume.

  Anachokifanya ni kujaribu, kisha kuitaarifu kampuni husika kasoro au ubora uliopo katika bidhaa hiyo.

  Takwimu zinaonyesha kuwa, kiasi cha viungo bandia vya siri milioni nne huuzwa barani Ulaya kila mwaka na huenda idadi hiyo ikaongezeka hadi kufikia milioni 400 katika siku za usoni. Hivi karibuni kumekuwapo taarifa za ongezeko la wanawake nchini, kufanya mapenzi wenyewe kwa wenyewe wakidaiwa kutumia nyeti bandia za kiume.
   
 2. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #2
  Mar 19, 2012
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,408
  Trophy Points: 280
  Ahahahahaaaa duuuh!! Dildos oyeeeeeeeee......
   
 3. Kobello

  Kobello JF-Expert Member

  #3
  Mar 19, 2012
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 5,674
  Likes Received: 628
  Trophy Points: 280
  Duh! za kike hazipo?
   
 4. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #4
  Mar 19, 2012
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,408
  Trophy Points: 280
  Blow up doll?
   
 5. Boflo

  Boflo JF-Expert Member

  #5
  Mar 19, 2012
  Joined: Jan 20, 2010
  Messages: 4,394
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  puchu, nyeto.....?
   
 6. k

  kaeso JF-Expert Member

  #6
  Mar 19, 2012
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 551
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Hii ni hatari kwa kweli.
   
 7. mzurimie

  mzurimie JF-Expert Member

  #7
  Mar 19, 2012
  Joined: Oct 16, 2011
  Messages: 6,151
  Likes Received: 1,604
  Trophy Points: 280
  si ndo maana wanaume wengine mnalia humu ampewi kumbe wanakuwa wameshajifurahisha...kwi kwi kwi
   
 8. Mtalingolo

  Mtalingolo JF-Expert Member

  #8
  Mar 19, 2012
  Joined: Aug 4, 2011
  Messages: 2,188
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Hatari mwanaumeeeeh.
   
 9. Babuu blessed

  Babuu blessed JF-Expert Member

  #9
  Mar 19, 2012
  Joined: Oct 14, 2010
  Messages: 1,340
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 145
  Hata ivyo wanawake wapo wengi acha wajipunguze wenyewe.
   
 10. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #10
  Mar 19, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,866
  Likes Received: 6,218
  Trophy Points: 280

  ama kweli wanawake mna hatari...nchi 12 zote za nini?
   
 11. Negrodemus

  Negrodemus JF Gold Member

  #11
  Mar 19, 2012
  Joined: Dec 30, 2010
  Messages: 2,119
  Likes Received: 101
  Trophy Points: 160
  dunia kushnei.
   
 12. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #12
  Mar 19, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Sasa wanaweza vipi kupiga vita mfumo dume kwa kwenda kununua kama njugu midoli yenye mfanano wa maumbile ya kiume? Siyo kwamba ndio wanauthibitisha mfumo huu?
   
 13. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #13
  Mar 19, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Kama wanaonekana kuvutiwa nazo, basi ni bora na sie tuzinunue ili kuwatoshelezea haja zao.....................
   
 14. mopaozi

  mopaozi JF-Expert Member

  #14
  Mar 19, 2012
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 3,290
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Raha iko nyama kwa nyama na c nyama kwa plastiki!!
   
 15. tz1

  tz1 JF-Expert Member

  #15
  Mar 19, 2012
  Joined: Mar 19, 2011
  Messages: 2,118
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 145
  Kama. Sababu ya wanawake kununua dildos ni kutowataka wanaume itatufanya wanaume thee na hela. Nyingi,maana hatutwa chunwa.
   
 16. Mchaka Mchaka

  Mchaka Mchaka JF Bronze Member

  #16
  Mar 19, 2012
  Joined: Jul 20, 2010
  Messages: 4,530
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0
  Habari imepikwa na shigongo!
   
 17. kibhopile

  kibhopile JF-Expert Member

  #17
  Mar 19, 2012
  Joined: Aug 5, 2010
  Messages: 1,303
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  duh, ngoja tu nitafute hela mengine yote ntazidishiwa,,,,
   
 18. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #18
  Mar 19, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Mambo ya kawaida sana, hivyo viungo ni faraja kwani bei za ndizi, matango na carrot zitashuka.
   
 19. HorsePower

  HorsePower JF-Expert Member

  #19
  Mar 19, 2012
  Joined: Aug 22, 2008
  Messages: 3,617
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  Inasikitisha, naona wazi sehemu ya jamii ya wadada wa Kitanzania sasa imepoteza dira, misingi ya imani, utu, mapenzi, uhusiano na ubinadamu inatoweka kwa kasi ....
   
 20. Ndetirima

  Ndetirima JF-Expert Member

  #20
  Mar 19, 2012
  Joined: Oct 4, 2011
  Messages: 893
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 60
  Kama kweli hizo plastic dildos zinaingizwa nchini za kutosha zitawasaidia sana hasa wanafunzi shule za wanawake za mbweni zilizoko mbali na miji kuliko wakiendelea kutumia mbizi, matango, karoti na sabuni wakati mwingine hukatika na kuingia kwenye mfuko wa uzazi na kuhatarisha maisha yao. Kwa wanaotumia madawa ya kulevya na bangi pia zitawasaidia sana kuepukana na ukimwi.
   
Loading...