Vituo vyagoma kushuhsa bei ;ewura mmeamua nini?? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Vituo vyagoma kushuhsa bei ;ewura mmeamua nini??

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Pdidy, Sep 12, 2011.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Sep 12, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,499
  Likes Received: 5,725
  Trophy Points: 280
  WAKATI EWURA WAMETANGAZA BEI KUSHUKA KAMA WALIVYOONYESHA HAPO CHINI ASILIMIA 80 YS VITUO VYA MAFUTA WAMEGOMA KUSHUSHA BEI NA KUACHA KAMA ZAMANI ;;NDUGU ZANGU EWURA MNATUAMBIA NINI KWA HILI AMA NDIO MNAENDELEZA USANII WENU KUTANGAZA HUKU MNASHINDWA KUSIMAMIA WATU WATEKELEZE MLICHOTANGAZA


  Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura) imeendelea kushusha bei za bidhaa za petroli, ambapo safari hii mafuta ya petroli kwa Dar es Salaam yatakuwa yakiuzwa kwa Sh. 2,031 katika kipindi cha wiki mbili zijazo yakiwa yameshuka kutoka Sh. 2,070, bei ambayo ilishia kutumika jana.
  Akizungumzia kushuka kwa bei huko, Mkuu wa Idara ya Mawasiliano na Uhusiano ya Ewura, Titus Kaguo, alisema bei ya mafuta ya dizeli kwa Dar es Salaam itakuwa ni Sh. 1,954 ikiwa imeshuka kutoka Sh. 1,999 na mafuta ya taa itakuwa ni Sh. 1,933 ikiwa imeshuka kutoka Sh. 1,980 bei iliyokuwa ikitumika hadi jana.
  Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kaguo, kushuka kwa bei ni mfululizo wa kushuka kwa bei tangu kuanza kwa matumizi ya kanuni mpya iliyoanza rasmi kutumika Agosti 1, 2011.

  “Bei za rejareja kwa aina zote za mafuta zimeshuka ikilinganishwa na bei zilizoanza kutumika kuanzia tarehe 29 Agosti 2011. Bei hizi zimeshuka kwa viwango mbalimbali ambapo Petroli imeshuka kwa Sh. 38.03 sawa na asilimia 1.84, Dizeli Shilingi 45.15 sawa na asilimia 2.26 na Mafuta ya taa bei zimeshuka kwa Shilingi 46.15 sawa na asilimia 2.33,” alisema.

  Kaguo alisema mabadiliko ya bei yametokana na kushuka kwa bei ya mafuta katika soko la dunia ambapo Petroli imeshuka kwa asilimia 2.54, Dizeli asilimia 3.78 na Mafuta ya taa yameshuka kwa asilimia 3.50.

  Hata hivyo, Kaguo alisema bei za mafuta katika soko la ndani zingeshuka zaidi kama Shilingi ya Tanzania isingeendelea kushuka thamani dhidi ya dola ya Marekani (Exchange Rate), sarafu ambayo hutumika kununulia bidhaa za mafuta kutoka soko la dunia.

  Kaguo alisema katika kipindi hicho, thamani ya Shilingi ya Tanzania imeshuka kwa asilimia 0.20 ikilinganishwa na Dola ya Marekani.

  Akizungumzia faida ya matumizi ya kanuni mpya, Kaguo alisema bei za rejareja zingepanda zaidi endapo kanuni ya zamani ingeendelea kutumika, ambapo badala ya kushuka hadi Shilingi 2,031 kwa petroli, bei hiyo ingepanda hadi kufikia Shilingi 2,205 huku dizeli ikipanda hadi kufikia Shilingi 2,126 badala ya Shilingi 1,954 wakati mafuta ya taa bei yake ingepanda hadi kufikia Shilingi 2,108 badala ya Shilingi 1,933.
   
 2. Sajenti

  Sajenti JF-Expert Member

  #2
  Sep 12, 2011
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 3,673
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Acha wagome si wanajua nchi wameikamata wao...wataenda kupigiwa magoti tu na viranja wetu vihiyo!!!...
   
Loading...