Vituo vya watoto yatima vya Daily Bread Life Ministres na Tosamaganga Iringa, wapewa Msaada

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,483
54,853
WATOTO yatima wa kituo cha Daily Bread Life Ministres cha Mkimbizi katika Manispa ya Iringa na wale wa kituo cha Tosamaganga katika wilaya ya Iringa Iringa wapewa msaada wenye nguo na chakula msaada wenye thamamani ya Tsh milioni 3 kwa ajili ya sikukuu ya Chrismas na mwaka mpya .

pamoja na msaada huo wa chakula na mavazi pia Mungai aliahidi kuchangia Tsh milioni 1.5 kwa ajili ya ununuzi wa vyombo vya muziki katika kituo hicho na kufanya msaada wake kufikia Tsh milioni 4.5
Huku mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela pamoja na kumshukuru mfanyabiashara huyo kwa kukumbuka yatima bado ametoa onyo kali kwa wanawake wote wanaotupa watoto kuwa ikibainika watachukuliwa hatua kali .

Akizungumza baada ya kukabidhi msaada huo Geofrey Mungai alisema imekuwa ni kawaida ya familia yake kila mwaka kusherekea sikukuu mbali mbali pamoja na watoto yatima kama sehemu ya kuikumbusha jamii kuwa na utamaduni wa kuwatazama yatima hao ambao tegemeo lao kubwa ni jamii inayowazunguka.

Mungai alisema kuwa suala la kulea yatima linapaswa kuwa ni jukumu la watanzania wote na kuwa ili kuwawezesha watoto hao kujisikia ni sehemu ya familia zenye wazazi ni vema jitihada za vituo vya yatima hapa nchini kuendelea kuheshimika zaidi.

Hata hivyo Bw.Mungai alisifu kazi nzuri inayofanywa na kituo hicho cha DBL katika kuendelea kuwalea watoto ha kimwili na kiroho na kuendelea kuwa miongoni mwa vituo bora vya kulea yatima katika mkoa wa Iringa.

Aidha aliwataka wananchi wengine kuendelea kufika katika kituo hicho na kusaidia kulea watoto hao kwa kutoa misaada mbali mbali kama njia ya kuwafariji na kuwalea watoto hao kuliko kuwaachia walezi wao pekee.
Hivyo alisema kwa mwaka huu amelazimika kutoa msaada wa nguo na chakula kwa kila kituo msaada wenye thamani ya Tsh milioni 1.5 na kuwa ataendelea kufanya hivyo kwa ajili ya watoto hao ili siku ya sikukuu nao waweze kufafana na watoto wengine ambao wanawazazi wao wote wawili .


Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela (kushoto ) na mfanyabiashara Geofrey Mungai wakiwa wamewapakata watoto yatima wa kituo cha Daily Bread Life Ministres cha Mkimbizi katika Manispa ya Iringa waliokuwa wametupwa na wazazi wao na kuchukuliwa na kituo hicho jana wakati Mungai alipofika kukabidhi chakula na nguo za sikukuu ya Krismas na mwaka mpya kwa watoto hao

Mkuu wa wilaya ya Iringa Bw Kasesela akisalimiana na Geofrey Mungai kulia

Viongozi mbali mbali wakiwa katika picha ya pamoja na yatima wa kituo cha DBL kutoka kushoto ni mkurugenzi wa kituo hicho mchungaji Mpeli Mwaisumbe , mfadhili Geofrey Mungai , katibu wa CCM Iringa , mwenyekiti wa CCM Iringa mjini , mkuu wa wilaya ya Iringa Bw kasesela,mbunge viti maalum Iringa Ritta kabati ,diwani Dolla Nziku.

Na MatukiodaimaBlog .
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom