Vituo vya Television na Radio vinachangia mimba za utotoni nchini

kavulata

JF-Expert Member
Aug 2, 2012
12,293
12,593
Haingii akilini kusikia eti chombo cha habari kama Radio (hasa za FM) na television (hasa za vijana) vinaendesha kampeni ya kuzuia ngono na mimba kwa vijana wakati huohuo vinahamasisha vijana kufanya kijiingiza kwenye mapenzi.

Imefahamika kuwa watoto wengi huwa hawasikilizi na kuangalia Radio na Television za taifa na zile za mashirika ya kidini. Vijana wengi huwa wanasikiliza Radio na television binafsi zinazoendeshwa na vijana wenzao. Nyimbo zinazochezwa kwenye vituo hivi zinawalazimisha watoto na vijana watake kujaribu kufanya ngono.

Nyimbo hizi waziwazi zinasifia utamu wa tendo la ngono kwa lungha mbalimbali zisizohitaji mtaalam wa BAKITA (baraza la kiswahili) kutafsiri. Bahati mbaya nyimbo hizi hazina wakati wa kuchezwa zinachezwa muda wowote siku na juma.

Watoto wana tabia moja ya kupenda kujaribu na kuona (curiosity) kile wanachokisikia na kukiona. Sasa kila redio inaimba mapenzi ni sukari, asali, manukato, raha, chokoleti, manono, kaing'ang'ania, usitoe, weka yote, raha hadi kisogoni, ramba koni, weka mbolea, mwanga maji niwike, piga nyembe, nk.

Hivi waziri mwenye dhamana hazisikii nyimbo hizi, Watoto wetu wanajifunza nini wakisikiliza nyimbo hizi?

Ni unafiki mkubwa watu kujifanya wanapambana na mimba za utotoni huku wanachochea vitendo vya ngono kutokea.
 
Back
Top Bottom