Vituo vya runinga vya ndani (local channels) na baadhi za nje zitarusha mubashara mkutano mkuu wa CCM

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,616
141,447
Luninga zote za ndani yaani local channels na baadhi ya tv maarufu duniani zitarusha mubashara tukio la mkutano mkuu wa CCM.

Kadhalika online tv na mitandao karibia yote ya kijamii itakuwa mubashara kuripoti tukio hili la kihistoria.

Wananchi wote mnashauriwa kufuatilia mkutano huu muhimu kwa maendeleo ya taifa letu.

Wenyeviti wote wa vyama vya upinzani wapo Dodoma kushiriki mkutano huu.

Wabunge wote wa upinzani wamealikwa kushuhudia ukumbini.

Tafadhali kaa jirani na luninga yako.

Kazi Iendelee!
 
Kama wenyeviti na wabunge wa upinzani wamo basi sina shaka kuwa ile biashara pendwa ya mwendazake na genge lake ya kununua wabunge itaendelea kwa mtindo ule ule
 
Kuna Nini kipya,


Yanayofanyika ccm ambayo hayajulikani labda ya miaka 50 tofauti na hapo Kila kitu kinajulikana.
 
Mgombea ni mmoja,mnatumia mabilioni ya fedha kwenda dodoma kumchagua, kwanini msipige kura hata online au electronic kuepuka matumizi makubwa ya fedha wananchi ili fedha hizo zitumike kujenga barabara,kununulia madawa na kusomesha bure wanafunzu vyuo vikuu. Ushauri muhimu, kuna wimbi la covid-19 ,faeni barakoa.
CHAMA CHA MAZEZETA ni CHANZO CHA MATATIZO
 
Back
Top Bottom