Kamukhm
JF-Expert Member
- Aug 30, 2015
- 2,799
- 4,195
Jiandaeni na wanasheria pamoja na wanamazingira na wataalamu wamipango miji nguli, thats money throughout and through... Sue .. sue ..sueTujiulize maswali haya
Je mipango miji inaruhusu vituo vya mafuta katikati ya miji na makazi ya watu?
Je sera ya mamlaka ya viwango na ubora inaruhusu vituo vya mafuta katikati ya miji na makazi ya watu?
Vipi wizara ya miundombinu?
Vipi wizara ya mazingira?
Jeshi la zimamoto je nalo haliwezi kuhusika hapa?
Kimsingi pamoja na tahadhari zote za usalama zinazochukuliwa lakini bado haishauriwi kuwa na vituo vya mafuta katikati ya miji na makazi ya watu... Na sheria ya vituo vya mafuta inasema kuwe na umbali USIOPUNGUA kilometer 5 kati ya kituo kimoja hadi kingine
Mafuta ni kitu kinachoweza kulipuka kwa haraka sana na kusababisha maafa makubwa ya watu na vitu kwa muda mfupi mno.. Hata magari yake na sehemu za kuhifadhia hayo mafuta zina alama kubwa za tahadhari ya hatari INFLAMMABLE (VILIPUZI)
Ni taasisi gani imeruhusu hili jambo la hatari kiasi hiki katikati ya mji na makazi ya watu na bila kuzingatia umbali kama sheria inavyotaka?
Kuna kampuni imeotesha vituo vya mafuta kila kona ya jiji ndani na nje, kwenye makazi ya watu, kwenye misongamano, kwenye maofisi na hata karibia kabisa na ofisi za mamlaka ya juu ama nyeti... Mtandao wa hivyo vituo unaleta mashaka na kutia hofu kubwa hasa katika kipindi hiki dunia inapopambana na ugaidi wa kila aina
Imagine itakuwaje kikatokea kikundi cha magaidi (Eeh Mungu tuepushe) kikakamata vituo vinne tu katikati ya jiji na kuvilipua... !? Ninini kitatokea?
Miundombinu yetu na vifaa vyetu kwenye kupambana na majanga makubwa ya moto bado sana... Tumewekeza kwa nguvu sana kwingine kote lakini sio kwenye kikosi cha zima moto... Tunaishi tu kwa kudra za mwenyezi Mungu...!
Kampuni husika iliyootesha vituo husika ndani katikati ya jiji la Dar imeishia kupigwa faini ya Tsh bilion tatu... Achilia mbali kama zitalipwa ama la ... Swali la kujiuliza je tuko tayari kuhatarisha maisha ya mamalioni ya watu na mali zao kwa ajili ya bilion 3? Maana baada ya kupigwa faini pengine ataruhusiwa aendelee na biashara.. NADHANI...!
Ni ngumu kumwambia abomoe kwakuwa pengine ana nyaraka zote muhimu za kumruhusu kufanya ujenzi na kufanya biashara..! Akizuiwa ndio mwanzo wa kushikana uchawi na pengine hakuna aliye tayari kufanya hivyo! Kwakuwa pengjne kila mmoja kala kwa urefu wa kamba yake!
Ni mpaka pale tutakapopigwa tukio moja baya kubwa na la kustukiza ndio akili zitatukaa sawa! Lakini tutaunda na tume? Jibu ni ndio kwakuwa huo sasa umekuwa utamaduni wetu...!