Mphamvu
JF-Expert Member
- Jan 28, 2011
- 10,702
- 3,288
Haya mabanda yanayotumika kuchezesha game kwa kulipia yamekuwa mengi jiji hili na hata mikoani. Si mbaya kwani ni burudani kama zilivyo burudani zingine lakini ningeomba tuangalie suala hili kwa mtazamo tofauti.
Michezo ya kompyuta, au gemu kama wanavyoita ni kitu chene uraibu (addiction) karibu sawa na vitu vingine hatari kama kamari na pombe. Wachezaji wa michezo hii wanaweza kutoa shuhuda zao jinsi mtu mzima na akili zake anaposhindwa kukakamilisha mambo yake ya msingi kwa kuwa alikuwa anacheza game.
Sasa hali inakuwa tishio zaidi kwani wanaopatwa na uraibu wa hii michezo ya kompyuta ni watoto hasa chini ya umri wa miaka 15 ambao wengi bado wangali shule na bongo zao zina mengi ya kujifunza. Michezo hii ikitawala sana akili ya mtu hujenga uvivu wa kimwili, kitu ambacho kinaweka msingi mbaya sana kwa mtoto na ni hatari kwa taifa letu changa.
Imefika wakati watoto hawa hutoroka shule ili kwenda kucheza hii michezo katika game, hapo sijasema madhara ya kiafya ya kukaa muda mrefu sehemu moja, kama mjuavyo, mwili unahitaji kufanya vimazoezi vya hapa na pale.
Jambo la kuogofya zaidi ni kuwa kucheza hii michezo kunataka pesa, kwa minajili hii kunaleta vichocheo kwa watoto kuiba pesa kwa wazazi wao, au kurubuniwa na pengine kujikuta wakifanyiwa vitendo vichafu kama kulawitiwa.
Sisemi isiwepo, maana kila mtu na starehe yake, lakini serikali za mitaa kwa kushirikiana na jeshi la polisi wanaweza kuweka muda na siku maalumu wa kufungua hivi vituo, mfano iwe kila siku kuanzia saa 10 jioni mpaka saa mbili usiku.
Tufikiri kwa ajili ya mustakabali wetu.