Vituo vya habari vyapigwa rungu na TCRA kwa kurusha maudhui katika muda ambao watoto hawapaswi kuangalia ama kusikiliza

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,495
9,275
MAMLAKA ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imevitoza faini ya Sh milioni 30 vyombo vya habari sita, kwa kukiuka kanuni na maadili ya utangazaji ikiwamo redio ya Clouds FM kuzungumzia supu ya pweza kuimarisha tendo la ndoa katika muda ambao wasikilizaji wanaweza kuwa watoto.

Mbali ya Clouds FM, vyombo vingine vilivyoadhibiwa ni East Africa Radio, na televisheni za Star, Sibuka, na Global Tv na Duma Tv.

Akisoma uamuzi huo jana jijini Dar es Salaam, Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Maudhui ya TCRA, Joseph Mapunda alisema vyombo hivyo vilikiuka kanuni za mawasiliano kwa nyakati tofauti.

Mapunda alisema redio ya Clouds FM kupitia kipindi chake cha Jahazi, walihamasisha vitendo vya ngono, kwa kutumia supu ya pweza katika kuimarisha tendo la ndoa kwa muda ambao wasikilizaji wanaweza kuwa watoto.

Alisema baada ya kusikiliza utetezi wao, wanatozwa faini ya Sh milioni saba na kupewa onyo kali baada ya kuwatia hatiani kwa kosa hilo.

Katika shauri lingine, kituo cha Duma TV kimetozwa faini ya Sh milioni saba na kufungiwa kuchapisha maudhui kwa muda wa mwezi mmoja ili wajipange na kuzifahamu kanuni na kuzingatia weledi na maadili ya utangazaji.

Mapunda alisema Duma ilikutwa na hatia ya kukiuka kanuni kwa kuchapisha na kutangaza maudhui yenye lugha isiyo na staha na iliyo na udhalilishaji wa kijinsia kwa wanaume na wanawake.

Alisema redio ya East Africa imetozwa faini ya Sh milioni tatu na kupewa onyo kali kwa kukiuka kanuni hiyo, kwa kurusha maudhui ya kukashifu utendaji wa serikali kupitia uteuzi wa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) na kutumia lugha ya kashfa dhidi ya utendaji wake.

Vilevile Global Tv imetozwa Sh milioni saba na kupewa onyo kali, baada ya kupatikana na hatia ya kuchapisha picha ya mnato na kutangaza maudhui yasiyokuwa na lugha ya staha na yenye kushabikia vitendo vya mahusiano ya kimapenzi ya jinsia moja.

Mapunda alisema maudhui hayo, yangeweza kuwaumiza na kuwakwaza waumini wa dhebebu la Anglikana na Watanzania kwa ujumla. Pia, alisema Sibuka Tv inatozwa faini ya Sh milioni tatu baada ya kupatikana na hatia ya kushabikia mauaji ya kutisha katika muda, ambao watoto wanaweza kuwa sehemu kubwa ya watazamaji.
 
Hebu kwanza tutajie vituo hivyo saba!


TCRA YAVIPIGA FAINI YA MILIONI 30 BAADHI YA VYOMBO VYA HABARI

Mamlaka ya udhibiti wa Mawasiliano Tanzania(TCRA) Imevipiga Faini ya Jumla ya Shilingi milioni 30 vituo sita vya televisheni na kutoa onyo pamoja na kusitishiwa kwa muda uchapishaji wa maudhui, kwa kukiuka kanuni,taratibu na misingi ya Utoaji habari.

1: Kituo cha #CloudsRadio
Kimepatikana na hatia ya kurusha maudhui ya kuhamasisha ufanyaji wa vitendo vya ngono kwa utumiaji wa supu ya pweza, maudhui hayo yalirushwa hewani muda ambao wasikilizaji wanaweza kuwa ni watoto, hivyo wamepewa adhabu ya onyo kali pamoja na kutahadharishwa kuwa hatua kali zaidi za kisheria zitachukuliwa dhidi yao endapo watarudia makosa hayo na pia watalipa faini ya shilingi milioni 5.

2:Televisheni ya mtandaoni ya Duma #DumaTV Imepatikana na hatia ya kutangaza maufhui yasiyo na lugha ya staha na yenye uzalilishaji wa kijinsia kwa wanaume na wanawake na kupewa adhabu ya onyo kali pamoja na kufungiwa kurusha maudhui kwa muda wa mwezi mmoja ili ijipange vizuri kuzifahamu kanuni na kuzingatia weledi wa utangazaji na kutakiwa kulipa faini ya Shilingi milioni 7.

3: Kituo cha #EastAfricaRedio kimekutwa na hatia ya kurusha maudhui yenye kukashifu utendaji wa Serikali katika uteuzi wa mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za Serikali (CAG) na kupewa onyo kali pamoja na kutozwa faini ya Shilingi milioni 3.

4: #GlobalTV nayo imepatikana na hatia ya kuchapisha taarifa ya picha mnato na kutangaza maudhui yasiyo ya lugha ya staha na yenye kushabikia vitendo vya uhusiano wa jinsia moja, Televisheni hiyo ya mtandaoni imepewa onyo kali na kutakiwa kulipa faini ya Shilingi milioni 7.

5: #SibukaTV imepatikana na hatia ya kurusha maudhui yasiyo na staha yenye kushabikia vitendo vya mauaji ya kutisha katika muda ambao watoto ni sehemu kubwa ya watazamaji na hivyo kusababisha athari za kiakili, kutokana na kosa hilo wamepewa onyo na kutakiwa kulipa faini yaShilingi milioni 3.

6: Kituo cha #StarTV chenyewe kimepatikana na hatia ya kukashifu Viongozi wa Wilaya ya Kisarawe na Waziri wa Tamisemi na hivyo wanatakiwa kuomba radhi kwa siku tatu mfululizo kwa Watazamaji wake na kulipa faini ya Shilingi milioni 5.

Uamuzi mwingine wa kutolewa kwa adhabu umegusa vituo vya Aboud Radio, Mo FM Radio, Planet Radio, EFM, Clouds TV na Ayo TV.

Vituo vilivyotozwa faini ni pamoja na Clouds Fm, Duma Tv, East Africa Radio, Global Tv, Sibuka Televisheni pamoja na Star Tv ambapo kila kituo kimetozwa faini kulingana na kosa lake

Akizungumza jijini Dar es salaam wakati akitoa hukumu hiyo Makamu Mwenyekiti kamati ya Maudhui Joseph Mapunda amesema kabla ya hukumu hiyo waliitwa wahusika na kamati ya maudhui na kujiridhisha kwa vituo hivyo kwa makosa ya ukiukaji wa kanuni za utangazaji.

Mapunda amesema kua katika hukumu hiyo kituo cha Duma Tv kimefungwa kwa kipindi cha mwezi mmoja kuanzia Leo ambapo faini yake shilingi milioni saba.

Aidha emefafanua kua kwa watu wasioridhika na uamuzi huo wanaweza kukata rufaa kwa siku ishirini na moja kuanzia leo.

Faini hizo kama ifuatavyo Clouds Intertainment Radio sh.milioni 5,Duma online TV sh.milioni 7,East Africa Radio sh.milioni 3,Global Tv sh.milioni 7,Sibuka Televisheni sh.3.Star Tv sh.milioni 5.

Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Maudhui wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Joseph Mapunda akisoma hukumu kwa vyombo sita vya habari vya utangazaji kwa kukiuka maudhui ya utangazaji.
 
Wasafi Chama lao tupo kimya tunawachora tu huku tunakunywa pepsi bariiiiidi na kuskiliza Playlist ya Amaboko🙉😂🤣
 
3: Kituo cha #EastAfricaRedio kimekutwa na hatia ya kurusha maudhui yenye kukashifu utendaji wa Serikali katika uteuzi wa mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za Serikali (CAG) na kupewa onyo kali pamoja na kutozwa faini ya Shilingi milioni 3.

Sielewi hili linakuwaje kosa kwa minajili ya kutoa maoni kinzani. Kama kuna aliyeathirika na kashfa tajwa, alipaswa tu kwenda mahakamani dhidi ya kituo.

Tusipoangalia haya kwa upana wake, ziko siku chochote kitakachofanywa na serikali kitaonekana kizuri hata kama kulikuwa na mawazo mbadala au ya kukifanya kuwa kizuri zaidi. Kuoneshana mawazo yetu tofauti kwa kubeza, kupinga ni muhimu sana!! Mambo hayo ndio huleta majadiliano na makubaliano.

Hatuishi katika dunia yetu pekee iliyo safi!!
 
Sielewi hili linakuwaje kosa kwa minajili ya kutoa maoni kinzani. Kama kuna aliyeathirika na kashfa tajwa, alipaswa tu kwenda mahakamani dhidi ya kituo.

Tusipoangalia haya kwa upana wake, ziko siku chochote kitakachofanywa na serikali kitaonekana kizuri hata kama kulikuwa na mawazo mbadala au ya kukifanya kuwa kizuri zaidi. Kuoneshana mawazo yetu tofauti kwa kubeza, kupinga ni muhimu sana!! Mambo hayo ndio huleta majadiliano na makubaliano.

Hatuishi katika dunia yetu pekee iliyo safi!!
Serikali ya CCM inataka kutukuzwa na kuabudiwa tu.
 
Back
Top Bottom