Vituo 800 vya kupiga kura Jamhuri ya Afrika ya Kati havifunguliwa siku ya Uchaguzi Mkuu

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Tume ya uchaguzi katika Jamhuri ya Afrika ya kati imesema zaidi ya asilimia 14 ya vituo vya kupigia kura nchini humo, vilishindwa kuendesha zoezi la kura ya urais na bunge kutokana na waasi kuwavamia wapiga kura na maafisa wa uchaguzi. Takribani vituo 800 kati ya 5,408 vya kupigia kura nchi nzima, havikufunguliwa siku ya uchaguzi uliofanyika jumapili.

Kulingana na mwenyekiti wa tume ya uchaguzi Theophile Momokouama, baadhi ya wapiga kura walipigwa na kutishiwa kuuawa. Jamhuri ya afrika ya Kati iliyo na utajiri wa almasi na dhahabu imekuwa ikikabiliana na wimbi la machafuko ya wanamgambo tangu mwaka 2013, ambayo yamewaua maelfu ya raia na kuwalazimisha zaidi ya milioni kuyakimbia makaazi yao.

Kampeni za uchaguzi ziligubikwa na ghasia kutoka makundi ya waasi ambayo yaliapa kuvuruga uchaguzi.
 
Dhahabu & almasi vimekuwa na thamani kubwa kuliko uhai wa mwanadamu --- hii ni HATARI sana kwa sayari dunia.
 
Tume ya uchaguzi katika Jamhuri ya Afrika ya kati imesema zaidi ya asilimia 14 ya vituo vya kupigia kura nchini humo, vilishindwa kuendesha zoezi la kura ya urais na bunge kutokana na waasi kuwavamia wapiga kura na maafisa wa uchaguzi. Takribani vituo 800 kati ya 5,408 vya kupigia kura nchi nzima, havikufunguliwa siku ya uchaguzi uliofanyika jumapili.

Kulingana na mwenyekiti wa tume ya uchaguzi Theophile Momokouama, baadhi ya wapiga kura walipigwa na kutishiwa kuuawa. Jamhuri ya afrika ya Kati iliyo na utajiri wa almasi na dhahabu imekuwa ikikabiliana na wimbi la machafuko ya wanamgambo tangu mwaka 2013, ambayo yamewaua maelfu ya raia na kuwalazimisha zaidi ya milioni kuyakimbia makaazi yao.

Kampeni za uchaguzi ziligubikwa na ghasia kutoka makundi ya waasi ambayo yaliapa kuvuruga uchaguzi.
Nilitegemea kupata vionjo vya jeshi huru la kagame hapa, sijaona
 
800/5408×100%=14.7%

So kura zimepigwa kwny 85% ya vituo vyote vilivyoko CAR,imeishaaaaaaa hio na mshindi atangazwe sasa.
 
Back
Top Bottom