Watoto wa siku hizi hawajui kabisa enzi zetu uliweza kuchapwa kwa sababu zifuatazo...

NI MTAZAMO TU

JF-Expert Member
Feb 20, 2014
1,203
998
Watoto wa siku hizi hawajui kabisa enzi zetu unaweza kuchapwa kwa sababu zifuatazo:

1. Unalia sababu umechapwa, utachapwa tena
2. Umechapwa ukulia utachapwa tena
3. Ukijililia tu bila kupigwa, utachapwa
4. Kusimama wakati wazee wameketi, utachapwa
5. Ukiketi wakati wazee wamesimama. utachapwa
6. Kujipitishapitisha mahali ambapo wazee wamekaa, utachapwa .
7. Kuwajibujibu watu wazima, utachapwa
8. Usipomjibu mtu mzima, utachapwa
9. Kujifanya sugu wakati wa unachapwa, utaendelea kuchapwa.
10. Ukitoka kuchapwa, ukaimba au kupiga mruzi, utachapwa tena.
11. Usiposalimia wageni, utachapwa
12. Ukila chakula cha wageni, utachapwa.
13. Kuwalilia wageni wanapo ondoka, utachapwa.
14. Ukikataa kula, utachapwa.
15. Kuchelewa kurudi nyumbani baada ya jua kutua, utachapwa
16. Kula nyumba ya jirani, utachapwa.
17. Kujitia kisirani, utachapwa.
18. Kujitia kujuwa juwa sana, utachapwa.
19. Ukipigana na mtoto mwenzio, akakupiga ukirudi nyumbani, utachapwa.
20. Ukipigana na mtoto mwenzio, ukampiga ukirudi nyumbani, utachapwa.
21. Ukiwa unakula chakula polepole, utachapwa.
22. Ukiwa unakula haraka haraka, utachapwa.
23. Ukiwa unakula sana, utachapwa.
24. Kuendelea kulala wakati wazee wamesha amka tayari, utachapwa.
25. Ukiwa unawaangalia wageni wakati wanakula, utachapwa.
26. Ukitembea na mtu mzima, ukajikwaa na ukaanguka, utachapwa.
27. Ukitembea na mtu mzima, akajikwaa ukamcheka, utachapwa.
28. Ukijamba mbele ya wakubwa, utachapwa.
29. Mtu mzima akijamba, ukamwangalia, utachapwa.
30. Ukila na wakubwa ukachukua nyama bila kupewa, utachapwa.
31. Ukinawa kabla ya wakubwa, utachapwa.
32. Ukimaliza kula ukanyanyuka kabla ya wakubwa, utachapwa.
33. Umechelewa kurudi dukani, utachapwa.
 
Vp tabia za wakubwa kuchafua hewa na kutusingizia watoto?
sisi enz hizo miaka ya mwanzo 70s tukiwa wadogo mzee akijamba yan faster tunawahi na kusisitiza ni sisi kuokoa jahaz ila baada ya hapo maumiv makal sana tunakabiziwa. Sasa itokee kwa mitoto mijinga ya siku hiz kama Cmiyu ye2 yani inawahi kusema ni wewe mzee boo lembor ndiye umejamba
 
Mkiwa mnakula samaki we hutoi mifupa unakula minofu tu..utachapwa sana..
 
  • Thanks
Reactions: e2n
Watoto wa siku hizi hawajui kabisa enzi zetu unaweza kuchapwa kwa sababu zifuatazo:

1. Unalia sababu umechapwa, utachapwa tena
2. Umechapwa ukulia utachapwa tena
3. Ukijililia tu bila kupigwa, utachapwa
4. Kusimama wakati wazee wameketi, utachapwa
5. Ukiketi wakati wazee wamesimama. utachapwa
6. Kujipitishapitisha mahali ambapo wazee wamekaa, utachapwa .
7. Kuwajibujibu watu wazima, utachapwa
8. Usipomjibu mtu mzima, utachapwa
9. Kujifanya sugu wakati wa unachapwa, utaendelea kuchapwa.
10. Ukitoka kuchapwa, ukaimba au kupiga mruzi, utachapwa tena.
11. Usiposalimia wageni, utachapwa
12. Ukila chakula cha wageni, utachapwa.
13. Kuwalilia wageni wanapo ondoka, utachapwa.
14. Ukikataa kula, utachapwa.
15. Kuchelewa kurudi nyumbani baada ya jua kutua, utachapwa
16. Kula nyumba ya jirani, utachapwa.
17. Kujitia kisirani, utachapwa.
18. Kujitia kujuwa juwa sana, utachapwa.
19. Ukipigana na mtoto mwenzio, akakupiga ukirudi nyumbani, utachapwa.
20. Ukipigana na mtoto mwenzio, ukampiga ukirudi nyumbani, utachapwa.
21. Ukiwa unakula chakula polepole, utachapwa.
22. Ukiwa unakula haraka haraka, utachapwa.
23. Ukiwa unakula sana, utachapwa.
24. Kuendelea kulala wakati wazee wamesha amka tayari, utachapwa.
25. Ukiwa unawaangalia wageni wakati wanakula, utachapwa.
26. Ukitembea na mtu mzima, ukajikwaa na ukaanguka, utachapwa.
27. Ukitembea na mtu mzima, akajikwaa ukamcheka, utachapwa.
28. Ukijamba mbele ya wakubwa, utachapwa.
29. Mtu mzima akijamba, ukamwangalia, utachapwa.
30. Ukila na wakubwa ukachukua nyama bila kupewa, utachapwa.
31. Ukinawa kabla ya wakubwa, utachapwa.
32. Ukimaliza kula ukanyanyuka kabla ya wakubwa, utachapwa.
33. Umechelewa kurudi dukani, utachapwa.
Dah.. kama ingekuwa ilikuwa hivi basi zaidi ya nusu ya watu wazima wangekuwa walemavu
 
Hawa wetu wa siku hizi ukifanya kama tulivyo fanyiwa sisi jela inakungoja mayai si mayai matoy si matoy watu tulikuwa manunda kweli kulikuwa na mchezo mbaya sana unachukua jiwe la mviringo kama mpira unalivisha soksi yaani kama chandimu vile kisha unamlia timing jamaa unamwambia piga jamaa anajikunjua huko ule ulikuwa uuwaji.
 
  • Thanks
Reactions: e2n
Ukikojoa kitandni unachapwa
Me nakumbuka mzee alinichapa nikamtegea sindano ktk kochi lake analopenda kukaa.wee ilikuw shida ingawa sikujulikana hd leo.
 
Back
Top Bottom