Vituko vya watoto wa wakubwa

mkama

Member
Oct 19, 2007
67
10
Wakili mtoto wa Karume azusha tafrani kortini

Tanzania Daima,22.11.07
na Happiness Katabazi na Nuru Yanga



WAKILI wa Kujitegemea, Fatma Karume, jana alitoa maneno makali dhidi ya Hakimu Addy Lyamuya wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam hali iliyosababisha hakimu huyo ajitoe kuendelea kusikiliza kesi inayomhusu mwanasheria huyo.
Tukio hilo la aina yake lilitokea katika chumba cha mahakama, wakati hakimu huyo alipotaka kuanza kusikiliza kesi ya madai namba 60/2006 ambayo ilianza kujadiliwa na hakimu huyo jana kwa mara ya kwanza tangu apewe jalada hilo.

Katika kesi hiyo, Fatma ambaye pia ni mtoto wa Rais wa Zanzibar, Amani Abeid Karume, anamwakilisha Sadiq Walji ambaye ni mdaiwa katika kesi hiyo ya madai ya mtoto. Mdai katika kesi hiyo namba 60/2006 ni Saeeda Hassam.

Kabla Hakimu Lyamuya kuanza kusikiliza kesi hiyo, Wakili Fatma, aliiomba mahakama kuahirisha kesi hiyo hadi kesho, kwa ajili ya kuanza kusikilizwa kwa shauri hilo.

Kutokana na hali hiyo, hakimu alimtaka karani wake kuangalia kwenye kitabu cha kumbukumbu (diary) kama siku hiyo itafaa kusikilizwa kwa shauri hilo. Hata hivyo, karani alimweleza hakimu kuwa siku hiyo zimepangwa kesi nyingi za kusikilizwa, labda waipange Januari 13, mwakani.

Hakimu Lyamuya alikubaliana na maelezo ya karani wake na kumweleza wakili huyo kwamba kesi hiyo itasikilizwa tarehe hiyo.

Baada ya hakimu kupanga tarehe hiyo, Wakili Fatma alianza kufoka kwa sauti ya juu akitaka mahakama isikilize kesi hiyo kesho, jambo ambalo Hakimu Lyamuya alilikataa kwa kueleza kuwa hakuwa na nafasi.

Wakili huyo aliendelea kuomba mahakama kupanga kesi hiyo Januari 2 mwakani, ombi ambalo hakimu huyo alilikataa na kumweleza tarehe hiyo mahakimu watakuwa mapumziko, ndipo wakili huyo alipoanza kutoa kauli kali dhidi ya hakimu huyo.

"Kwanza wewe hujui kazi na ni mara yako ya kwanza kuniona mimi… hunijui ni nani sasa nitakuonyesha… nitaandika barua kwa wakubwa wako wa kazi na kuwaeleza kwamba hujui kazi," alisema Fatma.

Baada ya kauli hiyo ya wakili Fatma, Hakimu Lyamuya alitangaza kujitoa kwenye kesi hiyo, ili kuwapisha mahakimu wenye nafasi ya kusikiliza kesi ya tarehe anayotaka wakili huyo.

Baada ya hakimu huyo kutangaza kujitoa, wakili huyo alimfuata alipokuwa amekaa na kuendelea kupinga uamuzi wake hali iliyosababisha karani na wakili wa utetezi katika kesi hiyo, Jerome Msemwa na watu wengine waliokuwepo mahakamani hapo kuingilia kati mvutano huo.

Kutokana na tafrani hiyo, mahakama ilishindwa kuendelea kusikiliza shauri hilo wala kulipangia tarehe na badala yake jalada la kesi lilirudishwa kwa uongozi wa mahakama hiyo, ili limpangie hakimu mwingine kusikiliza kesi hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya tafrani hiyo, Hakimu Lyamuya, alisema ameshangazwa na vitendo vya utovu wa maadili vilivyoonyeshwa na wakili huyo na kueleza hajafikiria kuchukua uamuzi wa kumfungulia kesi.

Licha ya vurugu hizo kutokea mahakamani, wakili huyo aliondoka eneo la mahakamani hapo bila kuchukuliwa hatua zozote na polisi wanaoangalia usalama mahakamani.

Kesi hiyo ya madai, awali ilikuwa ikisikilizwa na Hakimu Adolf Mahayi ambaye alijitoa kuisikiliza Septemba 6, mwaka huu, baada ya kutofoutiana na Wakili Fatma wakati kesi hiyo ikiendelea kusikilizwa.

Pia kesi hiyo iliwahi kupangiwa Hakimu Euphemia Mingi ambaye naye alishindwa kuendelea kuisikiliza baada ya wakili huyo kutofautiana naye mbele ya mahakama na kumtaka ajitoe. Hakimu Mingi alijitoa kuendesha kesi hiyo Oktoba 18 mwaka huu.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti, Hakimu Mingi na Mahayi walikiri kujitoa kwenye kesi hiyo kwa sababu walitofautiana na wakili huyo wakati wa kuisikiliza.

Hakimu Mkuu Mfawaidhi wa Mahakama ya Kisutu, Sivangilwa Mwangesi, alikiri kupokea taarifa za kutokea kwa vurugu hizo pamoja na barua ya kujitoa kwa Hakimu Lyamuya na kusema kuwa, amesikitishwa na kitendo hicho kwa kuwa kinakwenda kinyume cha sheria. Aliahidi kulifanyia uchunguzi tukio hilo, ili hatua za kisheria zichukuliwe.

Wananchi waliokuwepo mahakamani hapo ambao walizungumza na Tanzania Daima, walieleza kulalaani kitendo hicho, wakisema kimeidhalilisha mahakama na kuingilia uhuru wake.

"Hata kama yeye ni mtoto wa rais, anapaswa kufuata sheria na taratibu za mahakama husika… na tunashangazwa mahakama hii ina polisi wengi, lakini wameshindwa kumkamata na kumfungulia kesi ya kudharau mahakama… polisi wameshindwa kufanya hivyo kwa sababu wanaogopa kuwa wakili huyu baba yake ni Rais wa Zanzibar.

"Hivi angekuwa mtoto wa mlalahoi amefanya hivyo polisi wangemuachia? Jibu ni jepesi, wasingemwacha. Tunakuja hapa kutafuta haki kwa kuwa tuna imani na mahakama zetu, sasa mtoto wa kigogo anapofanya vitendo vya kuidhalilisha mahakama na polisi wanamuachia, unafikiri tutaamini kwamba haki inapatikana hapa?" alisema mmoja wa watu waliokuwepo mahakamani hapo.

Wananchi wengine waliwatupia lawama mahakimu na uongozi wa mahakama hiyo kuendelea kuvifumbia macho vitendo vya utovu wa nidhamu vinavyofanywa na wakili huyo dhidi ya mahakimu ambao wamekuwa wakipangiwa kusikiliza kesi hiyo


Baada ya kusoama habari hii,nimejiuliza maswali mengi ambayo hakika skupata majibu ya moja kwa moja;

1.Hivi mimi mtu wa kawaida mkama nikifanya kama huyu mtoto wa mhe;Rais mbele ya mheshimiwa hakimu nitaachwa tu niondoke mahakamani bila hata ya neno lolote kutoka wahusika wa mahakama?

2.Hivi kama mahakama nazo zinwasitahi watu wa kundi hili,je haki mahakamani ipo kwa wote au nikwa makabwela tu.

3.Nilipata kusoma kitabu cha Animal Farm,mwandishi aliweka Amri saba zilizotungwa na mkuu wa wanyama mara tu baada ya kumpindua mwenye shamba,amri mojawapo ilisomeka Wanyama wote ni sawa.Baada ya wanyama kupinduana wenyewe kwa wenyewe,amri ile iliongezewa maneno mengine mbele yake na kusomeka, Wanyama wote ni sawa lakini wengine ni sawa zaidi.Je haya si ndio yanyotokea sasa?Enzi ya Mwl.JK Nyerere vituko kama hivi vilikuwepo


4.Inawezekana imani ya wananchi dhidi ya mahakama na polisi kupungua(viashiria-kujichukulia hatua mikonon,uvamizi wa vituo vya polisi)matukio kama haya yanachangia

5.Hayo nimahakamani,na ile list ya watoto wa BOT wakitutia hasara tutaweza kuwakemea kweli?

5.Wananchi tufanye nini basi ili mambo yawe sawa?uh!nimechoka kabisa
 
Wanasheria sio watu wa kuchezewa kwasababu wanajua sheria. Polisi na mahakama wote wanalijua hili. Wewe mwenzangu na mimi endelea kuleta siasa tu humu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom