Vituko vya uchaguzi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Vituko vya uchaguzi

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Lekanjobe Kubinika, Jul 28, 2010.

 1. Lekanjobe Kubinika

  Lekanjobe Kubinika JF-Expert Member

  #1
  Jul 28, 2010
  Joined: Dec 6, 2006
  Messages: 3,067
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Hapa sijaelewa kinachoendelea. CCM sio kwamba wanafanya kampeni ya kwelikweli jamani? Ahadi zinazosemwa haziwahusu wanaccm peke yao, kwani bahari inayoahidiwa kupelekwa jimboni kalenga watavua pweza waliomo mle wanaccm peke yao? Message is being sent everyday and is perfectly delivered. Wapinzani wa CCM wakifanya kama wafanyavyo wanaccm kweli wataachiwa?
   
 2. d

  dady2007 Member

  #2
  Jul 28, 2010
  Joined: Nov 23, 2009
  Messages: 10
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  wamefanya wakazuiwa? acheni utoto, someni rules na mfanye kazi sio midomo na malalamishi.
   
 3. Masikini_Jeuri

  Masikini_Jeuri JF-Expert Member

  #3
  Jul 28, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 6,809
  Likes Received: 364
  Trophy Points: 180
  Juzi nimekutana na Mama mmoja wa CCM hapa Dodoma amewakusanya machinga mojawapo ya mikakati yake ni kuwajengea Machinga Complex ; machinga wa Dodoma. NIkatambua kuwa kumekucha sasa....................asiye na mwana........................!
   
 4. N-handsome

  N-handsome JF-Expert Member

  #4
  Jul 28, 2010
  Joined: Jan 23, 2008
  Messages: 2,317
  Likes Received: 128
  Trophy Points: 160
  :A S angry:
   
 5. Lekanjobe Kubinika

  Lekanjobe Kubinika JF-Expert Member

  #5
  Jul 28, 2010
  Joined: Dec 6, 2006
  Messages: 3,067
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Sisi tuache utoto, haya. Lakini mbona wewe mawazo yako yamezeeka hata hayasomi nyakati ukutani? Mpaka punda aseme ndipo ujue kwamba haki sio sawa kwa wote? Wewe uko nchi gani hata huoni tofauti hiyo na hata JF haifiki kila mara kwako? Leo tu umeambiwa na mleta hoja mmoja mwenye akili inayofikiri haraka, akakuambia mshangao wake kwa nini TBC na Daily news wanabagua. Umeshaambiwa vyombo vya habari vya binafsi ndivyo vinavyotoa habari kuhusu kinachoendelea nchini na uchaguzi kwa wapinzani, vyombo vya serikali KIMYAAAAAAA!

  Kama huna taarifa, Dr Slaa amefanya maajabu ya kukusanyika watu pale Karatu wakati anachukuwa form. Watu walikuwa wengi wengi wengi sana. ITV jana tu wameonyesha kwenye taarifa ya habari. Lakini wiki nzima CCM wakati wanateuana Dodoma hata shughuli za Bunge hazikuwa na maana kwao tena vyombo vya habari vya serikali. lakini hadithi ya kusanyiko kuuuuuuubwa la Slaa kuanzia Arusha hadi Karatu halikuwa news. Wewe unauliza wamefanya wakazuiwa. Sawa. Kwa hiyo Tendwa alipokuwa anasema Polisi wanakiuka sheria kwakuwazuia vyama vya upinzani kufanya mikutano yao naye pia analalamika bila akili kwa tafsiri ya maneno yako?

  Wewe unaongea kiushabiki na unaashiria uccm kabisa. Hiyo sio siasa tunayoitaka Tanzania ya leo. Free and fair in practical definition ndicho tunataka sie. Kuongea kwa jazba hakuondoi ukweli halisi ulivyo. Watu wa aina yako ndio viongozi waliotufikisha hapa, ambao hawataki mtu ajue haki zake ili wasisumbuliwe kwa madai halali, wapate mwanya wa kuwatesa na kuwaonea wajinga. Ataendelea kuwashikisha adabu Mtikila mpaka mkome ubishi wale wote ambao hamtaki watu watumie uhuru wao wa kuongea na kufanya sawa na Katiba (viraka) inavyotaka.

  Wewe unataka yatokee waziwazi na wewe mwenyewe uone ndio utambue kwamba mambo sio sawa? Kizazi kilichopotea ndicho kinachodai ushahidi, ambao wasiobahatika watausikia kutoka futi sita ardhini. Aliyeshika madaraka kamwe Afrika hii yuko radhi kuona anaondoka, ndio maana hila ni nyingi. Angalia Chama kimojawapo kimekataa kabisa uchuro wa kusaini makaratasi yanayodai usawa wakati tayari uchafu unaosemwa tayari unafanyika hadharani na CCM na inakuwa vigumu hata tume ya uchaguzi yenyewe kukemea kwa sababu anayefanya madudu ndiye anayewapatia mkate wa kila siku. Hata waliosaini maridhiano hayo wamefanya hivyo kwa sababu hawana jinsi, kwani kugomea ni kuipa faida CCM iendelee na uchafu wake.

  Ndio maana tangu mambo ya vyama vingi yameanza, watu wengi nami nikiwemo, wanaona ugumu wa kujiunga na chama chochote cha siasa, kwa vile CCM sio mkweli na pia upinzani unabanwa na kubezwa wakisema kweli. Bora kuwa neutral, BP zinabaki neutral pia.
   
Loading...