Vituko vya Suleiman “Mbwembwe”

Cesar Saint

JF-Expert Member
Nov 18, 2016
424
725
Wasalaam;

Kipindi cha utawala wa bendi Tanzania alikuwapo kijana machachari kutokea Tanga aliyeanza usanii akiwa kama mcheza show katika kumbi mbalimbali za starehe aliyejulikana kwa jina la Suleiman.

IMG_6731.JPG

Mzee Karenga mwenye gitaa na Mbwembwe kwenye Mic

IMG_6729.JPG

Mbwembwe,Shabaan Dede na Nasir lubuva

Uwezo wake wa kutunga na kuimba ulimpatia jina la Electronic Voice akipita katika bendi mbalimbali kama Tanzania Stars ,JKT Kimbunga,JUWATA,Vijana Jazz na OTTU (angalia kwenye nyimbo ya kilio cha mtu mzima baada ya verse ya TX Moshi)

IMG_6732.JPG

Dr Remy ,Mbwembwe na Kawalee Mutimwana

Licha ya kuishi uingereza kwa kipindi flani kituko kikubwa kilichompatia huyu bwana story midomoni mwa watu na wapenzi wa muziki ni kujipenda akitambulishwa kwa mbali na “Mustachi” yake malidhawa.

Adjustments.JPG

Suleiman Mbwembwe

Basi kuna kipindi aliyesemekana mpenzi wake wa wakati huo “Salome” aliugua maradhi flani wadau wanasema ilikuwa malaria basi huyu bwana akampeleka bibie Italy eeeh ndio “ITALY” kutibiwa malaria kisha kurejea nae bongo.

IMG_6730.JPG

Mbwembwe na Hamza Kalala


Huyo ndio Suleiman Mbwembwe .

Mungu amrehemu fundi huyu wa mziki.

Hebu leta kituko au kisa cha Star wa zamani unachokikumbuka.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom