Vituko vya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mulongo aliyejiwekea ulinzi kama wa Rais

Acheni majungu nyie watumishi wa jiji na halmashauri Mulongo ni jembe! tabia zenu za wizi na uzembe na uzembe atazikomesha nahisi mmeanza kuona cheche zake waulizeni wenzenu wa arusha aliwabana mpaka wakashindwa kupumua! Mulongo kwenye masuala ya maendeleo na matumizi mabaya ya fedha za umma habari mchezo na watumishi wanaokwamisha mambo hayo!

Mulongo amekuwa kiongozi bora anayetumia muda m

Wewe zwazwa unakumbuka nan alienda kuomba rushwa ya m100? Kwa Zipora Liama???
 
Huyu magesa ninamchukia sana anaongea kwa dharau sana kujiwekea ulinzi mkubwa inaonyesha kiasi wananchi hawapendi anaogopa kutembea mwenyewe wananchi wanaweza kumpiga hata mawe lakini akisikia jina la Lema anatetemeka mwili mzima kama yule mbunge wa monduli
 
Acheni majungu nyie watumishi wa jiji na halmashauri ! Mulongo ni jembe! tabia zenu za wizi na uzembe atazikomesha nahisi mmeanza kuona cheche zake waulizeni wenzenu wa arusha aliwabana mpaka wakashindwa kupumua! Mulongo kwenye masuala ya maendeleo na matumizi mabaya ya fedha za umma hana mchezo na watumishi wanaokwamisha mambo hayo anawa shughuli kila ipasavyo!

Mulongo amekuwa kiongozi bora anayetumia muda wake mwingi kuhakikisha ulinzi na usalama unaimalishwa katika eneo lake la utawala! Wote mnakumbuka Arusha ilivyokuwa na sasa ilivyo! Hivyo tumpe ushirikiano Mulongo awaletee maendeleo na ulinzi na usalama watu wa mwanza!
Mulongo ana mengi ya kukumbuka alipokuwa arusha,mojawapo ni sekeseke alilokutana nalo dhidi ya Godbless Lema,pili ni kutibuliwa dili lake la mabango ya barabarani aliloliunda na kampuni ya skytel,baadaye aliishia kuingia kwenye mgogoro na baraza la madiwani(bila kujali itikadi zao)pamoja na mkurugenzi wa jiji mama Sipora liana,huku akimtuhumu mkurugenzi kuwa anamchonganisha na madiwani,hali hiyo ilimpelekea kumtusi mama huyo mzalendo kila mara,huku akimtishia kuwa yeye (muhongo)ndiye Rais wa arusha!!na atahakikisha anamwondoa hapo arusha,jambo ambalo kweli alilifanikisha!!kwani mama Sipor hakuweza kudumu hapo arusha,hapo hapo uhusiano wake na madiwani pamoja na wananchi wa arusha ukawa mbaya kupindukia,hasa baada ya issue ile ya chuo cha uhasibu na tabia yake ya kuwatumia polisi kukamata watu hovyo,mfano siku moja alikuwa pale Arusha city park akiwa na wenzake,mara wakaingia akina Lema na rafiki zao,ghafla mkuu huyo wa mkoa alianza kukosa utulivu ghafla!! Na baada ya muda alipiga simu polisi(kutoka hapo hadi central police ni kama mita 50 tu kutoka hapo,polisi walipokuja aliwaamuru kumkamata Lema na wenzake bila sababu yoyote ya msingi,kitendo kilichoamsha hasira kwa watu wengi waliokuwa eneo hilo na zoezi hilo lilishindikana,in fact Arusha imekuwa tulivu baada ya kuondoka huyo shetani mtu!! Hata zoezi hili lililolalamikiwa sana na watu la ruti za hiace limeenda vizuri kutokana na pande zinazohusika kutumia hekima zaidi tofauti na huyo mulongo ambaye jeuri yake yote ni kukimbilia kutumia miguvu,jazba,majivuno,na mitutu ya polisi wajinga,poleni wana mwanza.
 
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Magesa Mulongo, ambaye ni mwakilishi wa Rais Jakaya Kikwete mkoani hapo, amebuni aina mpya ya ulinzi wake binafsi pamoja na msafara wa magari unaoambatana naye anapokuwa katika ziara zake za kikazi.

Aina hiyo ya ulinzi na msafara wake wa magari unaofanana kwa kiwango kikubwa na ule wanaopewa viongozi wakuu wa kitaifa, akiwemo Rais na Waziri Mkuu, ni wa kwanza kushuhudiwa na wakazi wa mkoani hapa na umedaiwa kugharimu kiasi kikubwa cha fedha.
attachment.php


Msafara wake umekuwa ukiwajumuisha pia askari wa usalama barabarani ambao kazi yao ni kujipanga barabarani na kuwazuia watumiaji wengine wa barabara wenye magari ili kusitisha kwanza safari zao mpaka hapo Mulongo na msafara wake wanapopita.

Katika msafara wake, Mulongo huambatana na Mkuu wa Polisi wa wilaya husika, maofisa usalama wa wilaya na mkoa, magari kadhaa ya watumishi wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza pamoja na maofisa wa wilaya anazozitembelea.

Sambamba na msafara huo wa magari, Mulongo pia analindwa na makundi matatu ya wanausalama ambao ni askari polisi wa kawaida, askari kanzu na maofisa usalama wa taifa.

attachment.php


Ingawa amekuwa akitumia aina hii ya ulinzi na usafiri hata katika safari zake za kawaida asubuhi anapotoka katika hoteli ya kitalii anayoishi kwenda ofisini wake, katika ziara yake ya kujitambulisha kwa wakazi wa Mkoa wa Mwanza aliyoianzia Wilaya ya Ilemela, ulinzi wake ulionekana kuimarishwa zaidi, huku idadi ya magari kwenye msafara wake nayo ikiongezeka.

Watu wa makundi mbalimbali waliozungumza na kuhusu aina hiyo mpya ya msafara na ulinzi wa Mulongo, wameeleza kushangazwa na jinsi mkuu huyo wa mkoa anavyojikweza na kudai kuwa una chembechembe za vitisho.

Wakizungumza kwa sharti la majina yao kutoandikwa mtandaoni kwa kile walichodai kuwa ni kuhofia kushughulikiwa na Mulongo, walisema wana mashaka na mwenendo wa kiongozi huyo na kubashiri kuwa unaweza kuwa na athari mbaya kwa serikali na hata Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Katika baadhi ya maeneo ambayo Mulongo alifika kujitambulisha na kuzungumza na wananchi alionya kuwa serikali itawachukulia hatua wale ambao wamekuwa wakijitokeza kwenda kulinda kura za wagombea wao nyakati za uchaguzi.


“Nimekuja kwenu kujitambulisha kama Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, hilo ndilo lengo la ziara yangu hii ambayo ni ya kwanza tangu nifike mkoani hapa. Nataka mtambue kuwa jukumu lenu la kwanza ni kukomesha uhalifu, niwasihi toeni taarifa za uhalifu polisi. Lakini naambiwa na ninyi mna tabia ya kubeba mawe na silaha za jadi kwa madai ya kwenda kulinda kura katika maeneo ya vituo vya kupigia kura, sasa nawatahadharisha kuwa watakaobainika na kukamatwa watajuta na waliowatuma tutawashughulikia,” alionya Mulongo.

Kabla ya kutoa onyo hilo, wakazi wa Wilaya ya Nyamagana waliohudhuria mkutano wa kujitambulisha ulioitishwa na Mulongo, walitumia fursa hiyo kutoa kero zao kwa kumueleza kuwa wakazi wa maeneo ya Bugando na Igogo wamekuwa wakivamiwa na kuporwa mali zao na vijana wa genge la kihalifu la Panya Road.

“Kuna wimbi la vijana wanaowavizia watu nyakati za usiku na kuwanyang’anya simu za mkononi na wanawake wamekuwa wakikabwa na kuchukuliwa mikoba na vito vya thamani, tunaomba msaada wa askari polisi kufanya doria maeneo mbalimbali hapa Igogo ili kuondoa kero hii,” alisema mmoja wa wakazi wa maeneo hayo.

Baadaye Mulongo na msafara wake walielekea Kata ya Butimba na kuzungumza na wananchi katika eneo la Stendi Kuu ya Mabasi ambako alielezwa kuwa eneo hilo halina miundombinu ya uhakika ya maji taka na vyoo vinahitaji ukarabati.

Mmoja wa maofisa wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza, Mhandisi Ezekiel Kunyaranyara, ambaye alitakiwa na Mulongo kutolea maelezo suala hilo, alisema taratibu za manunuzi ndizo zinazochelewesha ukarabati huo, lakini tayari mkandarasi yupo eneo la stendi akiendelea na kazi.

Majibu hayo yalionekana kumkera Mulongo, ambaye alimkaripia Kunyaranyara kwa kumtaka asikilize maagizo yake kwa sababu akiagiza kitu lazima kitekelezwe haraka.

Alisema amehamishiwa mkoani Mwanza kwa ajili ya kufanya kazi kwa maelekezo maalumu, kwa hivyo watendaji wasiotimiza wajibu wao wajue watapoteza kazi.

Katika ziara yake hiyo, Mulongo alitembelea Kata za Nyamagana, Igogo, Butimba, Buhongwa, Mirongo, Pamba na Igoma kwa upande wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza (Nyamagana) na Ilemela alitembelea Kata za Sangabuye, Bugogwa, Kirumba, Pasiansi na Busweru.
View attachment 225431 View attachment 225432

Sasa labda afuge mbwa wengi sana wamlinde kwani hao vijana wetu hawezi kupata hata mmoja!
 
Kama unaikumbuka Ahadi ya Tano ya Mwana TANU kwamba "Cheo ni dhamana sitakitumia cheo changu wala cha mtu mwingine kwa faida yangu". Hapa maneno yanajidhihiri bila shaka yeyote, huyu bwana alipewa cheo akakitumia ndivyo sivyo.
 
Acheni majungu nyie watumishi wa jiji na halmashauri Mulongo ni jembe! tabia zenu za wizi na uzembe na uzembe atazikomesha nahisi mmeanza kuona cheche zake waulizeni wenzenu wa arusha aliwabana mpaka wakashindwa kupumua! Mulongo kwenye masuala ya maendeleo na matumizi mabaya ya fedha za umma habari mchezo na watumishi wanaokwamisha mambo hayo!

Mulongo amekuwa kiongozi bora anayetumia muda m
Mbona uteuzi wake umetenguliwa kabla hata hajamaliza miezi 6?
 
Acheni majungu nyie watumishi wa jiji na halmashauri Mulongo ni jembe! tabia zenu za wizi na uzembe na uzembe atazikomesha nahisi mmeanza kuona cheche zake waulizeni wenzenu wa arusha aliwabana mpaka wakashindwa kupumua! Mulongo kwenye masuala ya maendeleo na matumizi mabaya ya fedha za umma habari mchezo na watumishi wanaokwamisha mambo hayo!

Mulongo amekuwa kiongozi bora anayetumia muda m
Hahaa...nimejikuta nakupa like za kejeli, any way Mungu akusamehe bure mdogo wangu.
 
He is a smart guy and someone needed, uvivu wa Watanzania ni mkubwa sana hawataki kwenda na wakati, majira na muda wao hujisukuma huku dunia ikisonga mbele katika kuleta maendeleo ya kisasa. Akipatikana mtu mtendaji na makini utasikia anataka kugombea ubunge au anataka cheo uvivu uvivu tu badilikeni piga kazi na wanaofanya kazi. KEEP IT UP MULOGO.
kweli aisee, naunga mukono hojaaaa....phaaa phaaaa..
 
Back
Top Bottom