VITUKO VYA BONGE LA JAMHURI YA MUUNGANO YA BONGO VYA MWAKA 2050

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,316
33,125
VITUKO VYA BUNGENI BONGO.jpg


Vichekesho vya baadhi ya Wabunge wa CCM Bungeni
“Mheshimiwa Spika, kabla sijaingia kuchangia bajeti hii, nataka niseme kuwa naona upinzani wamefikia pabaya sana, wanaikashifu serikali sikivu ya CCM.
Chama kimefanya mengi sana,
maendeleo makubwa tumepata,
shule za msingi, sekondari na vyuo viko vingi sana
tofauti na zamani,
barabara za lami, umeme nchi nzima mpaka vijijini, lakini wapinzani wanakebehi.
Naipongeza sana serikali ya Chama Cha Mapinduzi.
Mheshimiwa Spika, bila kupoteza muda sasa niingie kwenye jimbo langu, naomba nielezee kwa kifupi
matatizo ya jimbo langu.
Kule hatuna shule za sekondari katika kata sita, maji ni ndoto, tunategemea mvua za msimu. Shule zilizopo hazina ubora wala walimu wa kutosha.
Rais (Kipanya) alikuja sasa ni miaka sita akatuahidi umeme lakini mpaka
leo hakuna lolote.
Barabara ni mbovu hazipitiki.
Nauliza ni lini serikali hii ITATUSIKIA NA KUTULETEA
MAENDELEO?” (Wab unge Makofi)
kwa! Kwa! Kwa!.
Naombeni sana tena sana jimbo langu liangaliwe kwa jicho la
Huruma.
Baada ya kusema hayo
Mheshimiwa Spika, naunga mkono bajeti kwa 100%
Vipi wewe mbunge wako anawateteaje bungeni?
 
Back
Top Bottom