Vituko vya bodi ya mikopo Tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Vituko vya bodi ya mikopo Tanzania

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by Mzito Kabwela, May 29, 2010.

 1. Mzito Kabwela

  Mzito Kabwela JF-Expert Member

  #1
  May 29, 2010
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 17,520
  Likes Received: 1,691
  Trophy Points: 280
  Ukifika board ya mikopo kwa lengo la kurejesha form zako/za ndugu/jamaa/rafiki/mpenzi wako utakura rundo la watumishi wa board hiyo wakiwa chini ya vivuli kuhudumia wateja (warejesha form) kwa lengo la kuondoa msongamano (nawapongeza)

  Ukishapokelewa wanaitazama form yako, wanaangalia attachments na sehemu zinazopaswa kugongwa mihuri ya mahakama.

  Cheti chako cha kuzaliwa kipo (kina mhuri wa mahakama)
  Vyeti vya sekondari/diploma vipo (navyo vimegongwa mhuri wa mahakama)
  Form zako zina mhuri na kila kitu hadi serikali za mitaa wamepitisha
  Watakuuliza affidavit ya babako na mamako vipo wapi? Utajibu sina (kama huna), watakuambia kavifuate.
  Ukiileta, (tufanye ni kesho yake) watakuuuliza tena mbona hujaleta copy ya kikadi cha kupigia kura cha wazazi? Utakimbizana, utaleta copy zake...sasa itokee katika viambatanisho hivyo ukajisahau kugonga mhuri wa mahakama....
  Watakujibu...nenda nje ya geti yupo wakili. Lengo letu ni kuthibitisha kama wewe ni Raia wa Tanzania.
  Wakili anaitwa Nanyaro.....kila karatasi ni shilingi 6000/= ikipungua sana (discount iwapo una karatasi nyingi) ni shilingi 2500/=

  Wakili yule ana certify kabisa kuwa hii ni copy ya original document hata kama original document hujaende nayo......unampa hela yake, risiti hupewi, unaondoka zako unawapelekea karatasi zao wanaridhika kuwa wewe ni Mtanzania.

  Inasemekana kuwa wakili huyo ni jamaa wa mkubwa mmoja na kila akipatacho wanagawana na wakubwa wa board.

  Utahangaishwa weeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee mwishowe unakuja kupata asilimia 30! Sabini, tafuta mwenyewe!

  Tanzania ni Tambarareeeeeeee

  MZI
   
 2. mpuuzi

  mpuuzi Member

  #2
  May 29, 2010
  Joined: May 29, 2010
  Messages: 99
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mzitto, hata mimi mdogo wangu alikutana na kadhia hiyo. Ni deal wamecheza maofisa wa board. Wanapata 10%
   
 3. e

  eddy JF-Expert Member

  #3
  Jun 14, 2010
  Joined: Dec 26, 2007
  Messages: 9,373
  Likes Received: 3,774
  Trophy Points: 280
  Nashangaa sana hawa bodi ya mikopo wanatoaje mikopo wakati wao sio saccos wala benki? hivi kibali cha BOT cha kuendesha huu upatu walipata wapi? nadhani umefika wakati tugome tuishinikize serikali kazi hii ifanywe na taasisi za fedha hizo ndo zenye uzoefu wa kukopesha na kukusanya madeni. Niwakati sasa wa kuanzisha jumuia huru ya wazazi itakayoshughulikia matatizo ya watoto ikiwemo mikopo ya masomo. Zamani tulikuwa na jumuia iliyoitwa TAPA sijui ilifia wapi?
   
 4. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #4
  Jun 14, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,186
  Trophy Points: 280
  Hivi Tanzania siku hizi kupiga kura ni lazima?
   
 5. e

  eddy JF-Expert Member

  #5
  Jun 14, 2010
  Joined: Dec 26, 2007
  Messages: 9,373
  Likes Received: 3,774
  Trophy Points: 280
  Shangaa! ada ya shule na kura wapi na wapi? ilimradi watoto wahangaike tu!
   
 6. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #6
  Jun 14, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,186
  Trophy Points: 280
  Hapa kuna lawsuit. Kuna watanzania wengine hawaamini katika kupiga kura, kwa lugha ya mkato wanaona ni miyayusho tu.Sasa kulazimisha wao na familia zao wasipate mikopo kwa sababu za imani zao za kisiasa kwa maana ya kadi za kura ni kinyume na katiba.

  Hii haina tofauti na kutoa sharti kwamba kila mtu anayetaka kupata mkopo atoe kadi ya CCM. Hakuna tofauti kabisa.


  In essence, unataka kufanya political affiliation kuwa factor katika kutoa mkopo.

  Hivi hawa watu wanavuta madawa gani ya kulevya?
   
 7. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #7
  Jun 16, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  waacheni tu.. mbona tumeimba huu wimbo wa bodi ya mikopo kwa miaka minne sasa?
   
 8. N

  Nicko Member

  #8
  Jun 19, 2010
  Joined: Aug 13, 2009
  Messages: 24
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Mwenyewe ilinishangaza kuona huyo jamaa anagonga mihuri nje wakati hata maofisa wa bodi wanamuona..Tanzania bwana
   
 9. Lukolo

  Lukolo JF-Expert Member

  #9
  Jun 19, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 5,137
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Binafsi sioni msingi wa lawama hapa. Hivi hata kama umepeleka hizo document zote zikiwa na mihuri ya mahakama bado watataka ukaongeze mwingine kwa huyo bwana? Au kwa mfano umekwenda kupeleka form, baadhi ya document hazijakamilika, sasa akikuambia ukalete unaona kwamba hujatendewa haki? Kuepusha usumbufu ni bora, hapo atakapokwambia ukalete document hizo nyingine muulize kabisa akwambie document zote zinazohitajika na zote zinazohitaji certification. Sidhani kama umepeleka document zenye vielelezo vyote bado utaambiwa umpelekee huyo Nanyaro. Haya mambo hata UDSM yapo ukitaka kuchukua vyeti vyako utaambiwa ukagonge mhuri kwa wakili pale sheria, sasa tuseme wale mawakili wa pale sheria wanakula na wakubwa? Watanzania tumezidi sana kwa lawama bwana!!
   
 10. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #10
  Jun 19, 2010
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,196
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  Tusiwalaumu kabisa, matatizo ni yetu wenyewe, kewa sababu:

  1. Sincerly hakuna huduma ya uhakika kwenye ofisi yoyote ya serikali au agencies.

  2. Na sisi wenyewe tunalea hii tabia, hakuna akiyesoma sheria ya bodi ya mikopomna regulations zake.

  3. Kwa sababu hiyo ( kutosoma hiyo sheria) wengi hawajui wapi kupata haki yao.
   
Loading...