Vituko vya Air Tanzania: The wings of kilimanjaro!

Teamo

JF-Expert Member
Jan 9, 2009
12,272
1,034
Habari zenu wakuu wangu..!well.nimeona ni vyema nikawajuza kinachoendelea hapa uwanja wa ndege wa kimataifa wa mwalimu j.k.nyerere.Kuna hii ndege ya shirika la kizawa la air tanzania iliyokuwa na safari ya kwenda kigoma tangu saa kumi na mbili.nimeshangazwa kuwakuta jamaa zangu wapo wapo tu hadi muda huu.Nimeingia ndani nimelegea.naiona ndege hapa inatengenezwa bado,na haijulikani itapona lini.hofu yangu ni usalama wa hawa abiria kama watapaa na hitilafu ikatokea huko maana hakuna muda wa kucheck.INASIKITISHA SANA TENA SANA kuona nchi iliyopigana vita miaka yote rwanda wanaleta ndege ya adabu tanzania.hapa naiona RwandaAir ina kula nyomi na kuchapa mwendo.nawatakia ijumaa njema!nawaacha jamaa zangu wa kigoma mimi na chapa raba.AMANI KWA REV KISHOKA "tumeuza uhuru wetu,na mali yetu tumeifuja".
 
Shirika lazima litasua sua kwasababu halina uongozi; Mwenyekiti wa bodi ya shirika yuko Kondoa anataka kurudia ubunge na Mkulu bado hajateua replacement ya Mattaka kwani aliyepo ni acting kwahiyo mambo ndio hivyo tena mwaka wa uchaguzi lakini WINGS OF KILIMANJARO ndio zinaanguka hivyo!!!! Somebody has to act.
 
Well sikuwapo nchini; Mattaka was removed? when?
 
......watu walianza kuutafuna utumbo ndani kwa ndani, sasa wanamalizia mifupa...scrapers......!
 
Mkuu, Geoff, hayo umeyaona ndani ya muda mfupi tu ambao uko hapo ukingoja kusafiri, lakini kuna wanaoona mambo hayo kila iitwapo siku, na yanachefua!...

Shirika hili ni kama kifaranga kilichokosa mama Mlezi!...Ndege hiyo uliyoiona inafanya kazi hadi inatia huruma!..Ikitoka hapo Dar inaenda huko KIGOMA, inarudi Dar, then Arusha, then Zanzibar, then Dar, na wakati mwingine iunganishe Mwanza, ndo ije kulala Dar...!

Actually NDEGE hIyo ni kama punda MWAMINIFU SANA anayefanya kazi bila ulalamishi, lakini aliyekosa malisho mema!...

Mungu Ibariki Tanzania ...Mungu ibariki Africa!
 
Jamani serikali ilinusuru shirika letu hili...ndege inappiga mziko hiyo hata huruma utaionea..mie ndio msafir hasa wa hiyo ndege kwenda kigoma na ni ndege ya shirika la ATC tu ndio inakuja Kigoma na isipokuja ni issue.....Jamani Kawambwa linisuru shirika hilo please!!!!!!!
 
mmmh hizo ndo zao mm niliganda moshi last week for 5hrs,wanasema ndege haijatoka dar,kumbe ipo kia haina mafuta!I HATE THEM
 
Huyu Shukuru Kawambwa atadunganyaje tena hapo?
Mashirika ya umma ndivyo yalivyo naomba serikali ibinafsishwe tu hakuna haja ya kuwa na matendaji mavivu.
 
Ndio tatizo la kuwa na raisi anayetoa vyeo kwa marafiki bila kuangalia uwezo wao ingawa wengi tayari walishashindwa kazi kwingineko.

Rwanda wanasonga mbele haraka kwani wanajali sana taaluma na uwezo wa mtu.

Tuiombee Mungu ATC isijefikwa na ajali kubwa kwani huo ndio utakuwa mwisho wake.
 
Masaki "mfianchi" uko wapi? njoo huku uone huu uzalendo upo wapi.No wonder tukishabikia vya wenzetu ni bora zaidi.
 
Bora n'nzi ibinafsishwe kwa wakoloni watuletee maendeleo upya hawa weusi wetu tumewachoka
 
Masaki "mfianchi" uko wapi? njoo huku uone huu uzalendo upo wapi.No wonder tukishabikia vya wenzetu ni bora zaidi.

kuna mambo yanatia hasira nchi hii jamani aaaaaaaaaaaaaaah!!!
 
Hivi tutalalamika kuhusu utendaji wa serikali hii mpaka lini? maana kila chetu ni cha hovyohovyo tu. Kila ukiangalia vya wenzetu ni vizuri hata kama sio 100% lakini vinatia moyo na unaona kuwa huko kwao kuna wanaojali.
Hivi hawa viongozi wetu wanatuonaje sisi? Hawajifunzi kwa yaliyotokea Ivory Coast, Romania na kwingineko na kujirekebisha mapema? Kwa kweli hali ya nchi ni mbaya kuliko tunavyo dhani kwa sasa.
 
Shirika lazima litasua sua kwasababu halina uongozi; Mwenyekiti wa bodi ya shirika yuko Kondoa anataka kurudia ubunge na Mkulu bado hajateua replacement ya Mattaka kwani aliyepo ni acting kwahiyo mambo ndio hivyo tena mwaka wa uchaguzi lakini WINGS OF KILIMANJARO ndio zinaanguka hivyo!!!! Somebody has to act.

management kwa kweli ni tatizo kubwa sana na hilo ndo linaua mashirika kibao hapa kwetu.....
mijitu inpachikwa pachikwa tu
haya huyo mwenyekiti mwenyewe mbunge sijui wa Kondoa, useless
bungeni alikwa toothless n speechless
huko ATC atafanya nini cha maana hasa?? Jimboni kwake kafanya nini cha maana??
agrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrr
 
Aibu kwa SERIKALI..Waziri Kawambwa awajibike.. Ukienda TRL ndio wako kwenye mazishi..
 
management kwa kweli ni tatizo kubwa sana na hilo ndo linaua mashirika kibao hapa kwetu.....
mijitu inpachikwa pachikwa tu
haya huyo mwenyekiti mwenyewe mbunge sijui wa Kondoa, useless
bungeni alikwa toothless n speechless
huko ATC atafanya nini cha maana hasa?? Jimboni kwake kafanya nini cha maana??
agrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrr

Heshima mbele bht, mwenyekiti wa ATCL ni Mustapha Nyang'anyi ambae aliwahi kuwa mbunge wa Kondoa kwa takribani miaka 25 hivi kabla ya kwenda ubalozini; sasa amestaafu anataka kurudia tena ubunge!! Hivyo kwa wakati huu hana muda wa kutosha kushuhulikia mambo ya ATCL yuko kwao anaweka mambo sawa!! Sio mbunge huyo wa Kondoa wa sasa kama ulivyodhania.
 
asante mkuu kwa ufafanuzi

all in all they are all useless
hakuna walichofanya ever since
damnmmmmmmmmmmmmmmmmmm!!!!
 
HIVI MMESAHAU KIREFU CHA ATC?!!!!!!!
A.T.C- ANY TIME CANCELLATION.
poleni.
 
Back
Top Bottom