Vituko vya abunuasi ni noma

omari msuya

Member
Sep 7, 2011
10
2
siku moja Abunuas kamkodishia muhindi moja vyumba kwenye ghorofa yake ila yeye anakaa chin muhind juu.sasa abunuas akataka kuuza ile ghorofa muhind akakubal kununua juu tu na hivyo abunuas kumfanya muhind anunue yote akaanza kumfanyia vituko mara abomoe ngaz za kupandia muhind akajenga zake,abunuas akafanya vituko ving muhimd anunue ghorofa ya chin ikashindikana mwishowe akamwita muhind akamwambia nimewaita mafundi wabomoe ghorofa yangu ya chin shika yako ya juu usije ukasema sikukwambia.muhind hoi kwa presha
 
vitabu vile nitavipata wapi wana jf?hakuna website yenye hadithi zile?
 
hata mie napenda vitabu vya zamani, kitabu cha
alfu lela ulela nilipata book shop ya mlimani city
nitaenda kutazama na hiki cha abunuasi ili nicheke vizuri.
 
Vitabu vya zamani sio siri ndiyo mpango mzima Nimewahi kusoma elfulela ulela 1, 2, and 3 yaani ni noma!
 
Nahisi hadith yake inatufundisha tukitaka kuuza vitu tutishie kuvibomoa,kwa mtindo huo tutapata wateja haraka
 
Nilikutana na jamaa anauza vitabu hivi ktk kivutko pale GEITA ninazo copy ni vizuri ingawa enzi hizo sikuwahi visoma
 
Huyu si ndo aliyekua akikata tawi huku kakalia upande utakaodondoka?
 
na mimi natafuta vitabu vyake, nakumbuka mwalim wetu mmoja alikuwa akitupia stori zake manake pindi la mchana watu walikua wakilala sana
 
Ile kali zaidi ya Abunuwasi ni pale alipokuwa na shida na Sultani. Kufika mlangoni kwa sultani wale mlinzi akakataa kumruhusu aingie kumwona. Abunuwasi akaomba sana aruhusiwe kumwona Sultani maana alikuwa na shida kubwa. Mlinzii alijuwa kuwa abunuwasi akiingia kwa sulatani atapata anachotaka maana alipendwa sana na sultani. Mkwara aliompa ni kwamba aahidi kuwa atakachopata kwa sultani wagawane nusu kwa nusu na mlinzi wa sultani, abunuwasi akakubali na akaingia kwa sultani. Kufika ndani sulatani anamuuliza sema shida yako abunuwasi maaana leo unaonyesha una huzuni. Abunawasi akasema Seyidina wangu naomba unichape viboko mia, Sultani akashangaa, kwa kosa gani? Abunuwasi akasema nichape tu Seyidina wangu na akasisitiza kuwa haondoki mpaka achapwe. Sulatani akaamura askari pale kwenye kiti cha enzi amtandike Abunuwasi taratibu sana viboko mia. Walipomchapa mpaka viboko hamsini Abunuwasi akasema vimetosha maana mlinzi wa pale getini tumekubaliana kuwa nitakachopata humu ndani kwa sultani lazima na yeye apate nusu yake kwa hiyo hivyo hamsini vilivyobaki atandikwe mlinzi. Sulatani kusikia hivyo akaghadhabika sana na kuamuru mlinzi aletew apigwe viboko hamsini tena vya uhakika. Mlinzi alijuta kuzaliwa, na hakurudia tena kuomba rushwa
 
Samahani kwa kwenda kinyume jamani nina shida naomba tuwasiliane kwa e mail <a href="mailto:joseph.eric86@yahoo.co.uk">joseph.eric86@yahoo.co.uk</a> au kwa 0715005450.naomba msada tuwasiliane kwa njia hizo samahan kwa usumbufu

Sasa nawe hebu dadavua japo kidogo tukuelewe. Huo Msaada sana unaohitaji ni kuhusu hizi hadithi za abunuwas au nini?? Maana umeingia tu gafla hata hueleweki.
.
 
Back
Top Bottom