Vituko haviishi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Vituko haviishi

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Kimbweka, Dec 12, 2010.

 1. Kimbweka

  Kimbweka JF-Expert Member

  #1
  Dec 12, 2010
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 8,608
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Kuna mambo yanashangaza sana na kukupelekea uwaze sana na hupati jibu

  Ilikuwa hivi: Jamaa amempeleka mkewe hosp na ikabidi alazwe na vipimo vilionyesha kuwa ana upungufu wa damu. Hivyo ikabidi wacheki kama group ya mumewe inaendana na ya mkewe ili amchangie damu, kwa bahati siyo nzuri haikuendana, Katika hangaika akakutana na rafikie ambaye yeye alikuwa anajitambua ni group gani na itamfaa mkewe, cha msingi ni kupima ngoma kama hana aweze kutoa damu kwa ajili ya mke wa rafikie. Cha ajabu jamaa akakataa katakata kwamba hataki damu ya rafikie iingie kwa mkewe, hivyo aliendelea kutafuta mpaka akampata rafiki wa kike wa mkewe ndipo akatoa damu na kufanikisha kuwekewa mkewe

  Sasa nimekuwa nikijiuliza huyu jamaa alihisi nini mpaka kukataa rafikie asimtolee damu mkewe mpaka akatafuta mwanamke rafiki wa mkewe
  Nimekuwa nikijiuliza sipati jibu
  Kama huyo jamaa yupo hapa JF anisamehe sana au kama ana jibu anipe
  Bado nawaza.............
   
 2. Preta

  Preta JF-Expert Member

  #2
  Dec 12, 2010
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 24,113
  Likes Received: 3,036
  Trophy Points: 280
  kweli vituko havitakaa viishe.......je kama ilikuwa imebaki dakika chache wife afe....angekataa jamaa asimwekee damu
   
 3. Kimbweka

  Kimbweka JF-Expert Member

  #3
  Dec 12, 2010
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 8,608
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  sijapata jibu na sijajua mpaka sasa huyu jamaa alihisi au fikiri nini?
   
 4. St. Paka Mweusi

  St. Paka Mweusi JF-Expert Member

  #4
  Dec 12, 2010
  Joined: Sep 3, 2010
  Messages: 5,900
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 145
  Wivu tu unamsumbua huyo jamaa,naona alijua rafiki yake akitoa damu yake iko siku ataomba naye achangamshwe damu yake iliyobaki.
   
 5. Kimbweka

  Kimbweka JF-Expert Member

  #5
  Dec 12, 2010
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 8,608
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Achangiwe vip kwani yeye ana upungufu?
   
 6. Mtego wa Noti

  Mtego wa Noti JF-Expert Member

  #6
  Dec 12, 2010
  Joined: Nov 27, 2010
  Messages: 2,230
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 160
  aliogopa kuwa angempa damu ingekuwa ndio nji ya huyo rafikiye kumpata mkewe...labda alishahisi kuwa mshikaji anammega mkewe ndio maana kakataa damu yake.
   
 7. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #7
  Dec 12, 2010
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Wivu hauleti maendeleo!Angekufa je?
   
 8. Tausi Mzalendo

  Tausi Mzalendo JF-Expert Member

  #8
  Dec 12, 2010
  Joined: May 23, 2010
  Messages: 1,471
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Ama kweli sikio/jicho halilali na njaa!
  Kwanza huyo jamaa ni ujinga na ushamba tu vinamsumbua kwa sababu haina maana damu iliyogemwa saa hiyo ndio hiyohiyo inaenda kutundikwa kwa mkewe! Damu hiyo ingingia kwenye bank ya damu ili kuziba pengo na haiyumkini mke angewekewa ya mtu mwingine tu.
  Vile vile, kama angekuwa na akili na uwezo wa kuwa na kibri cha wivu, basi wenziwe wanachofanya ni kujiwekea akiba zao ziweze kutumika itakapobidi!
   
 9. St. Paka Mweusi

  St. Paka Mweusi JF-Expert Member

  #9
  Dec 12, 2010
  Joined: Sep 3, 2010
  Messages: 5,900
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 145
  Mkuu punguza haraka katika kusoma nimesema achangamshwe sio achangiwe,kwani wewe hujui maana ya kuchangamsha damu?
   
 10. Kimbweka

  Kimbweka JF-Expert Member

  #10
  Dec 12, 2010
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 8,608
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Hili pia nafikiri hakulijua
   
 11. Kimbweka

  Kimbweka JF-Expert Member

  #11
  Dec 12, 2010
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 8,608
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Nimekusoma mkuu
   
 12. TANMO

  TANMO JF-Expert Member

  #12
  Dec 12, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 8,919
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 160
  Hehe, huyo alidhani kuwa damu in sumaku hivyo damu ya mkewe na ya jamaa zitavutana na matokeo yake wata-du....
   
 13. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #13
  Dec 12, 2010
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 444
  Trophy Points: 180
  Anadhani damu inachembechembe inayotengeneza mimba.
   
 14. Kisima

  Kisima JF-Expert Member

  #14
  Dec 12, 2010
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 3,768
  Likes Received: 2,228
  Trophy Points: 280
  Hiyo nimeipenda!
  Jamaa alikuwaright na aliona mbali wanawake wengi wao niwepesi wa kulipa fadhira so yangeweza kujitokeza mengine km jamaa angeaccept zawadi toka kwa shemejiye na nauhakika shemeji mtu angeombwa TUNDI bila shaka angesaula si unajua tena wanawake huruma yao huwa njenje hata km ni risk!
   
 15. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #15
  Dec 12, 2010
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,754
  Likes Received: 82,702
  Trophy Points: 280
  Shemeji ahsante sana kwa kunichangai damu nilipokuwa na upungufu damu. Nakushukuru sana. Ahsante sana shemeji ukishapata nafuu basi tutaongea zaidi kuhusu hili kusanya nguvu kwanza.

  Njemba ilikuwa na wasiwasi labda rafiki amekuwa akimsifiasifia shemeji yake kwa uzuri mara nyingi tu hivyo akahofia kwamba anaweza kulitumia hili la kumchangia damu ili ajisogeze karibu naye zaidi. Marafiki wengine ndivyo walivyo.
   
Loading...