Vituko Afrika Kusini: Wafungwa gerezani waletewa dada wavua nguo (strippers) ili watumbuizwe - picha

Hiz
Kila siku Afrika Kusini hukosi kusikia vituko na mambo ya ajabu. Safari hii maofisa wa gereza fulani huko Afrika Kusini, waliamua kuwatumbuiza wafungwa kwa kuwaletea wale kina dada wanaokata viuno na kuvua nguo (strippers) ili eti wafungwa watumbuizwe.

Nadhani Afrika Kusini imeanza kuona athari za kubadilisha wazungu na kuweka Waafrika hata wasio na sifa kwenye vile vyeo walivyokuwa wakishika wazungu. Kiongozi aliye elimika wa magereza hawezi kufikiria kufanya jambo kama hili. Athari hii inaonekana kuanzia ngazi za juu za uongozi wa nchi hadi chini, na inasemekana inaua taasisi na mashirika mengi nchini humo, watu kupewa vyeo vikubwa bila kuwa na uwezo kwa kuwa tu ni wazalendo.

Kwa wale wanaoelewa hali ya ukame gerezani, nadhani watajua wafungwa waliachwa katika hali gani. Maofisa kadhaa waliohusika na hili wamesimamishwa kazi.

View attachment 531340View attachment 531409
Source: iol
Hizi habari nlisikia juzi BBC
 
Back
Top Bottom