Vitu vya msingi ambavyo ilitakiwa tufundishwe polepole tangu utotoni lakini haikuwa hivyo

Apollo one spaceship

JF-Expert Member
Jan 28, 2021
242
431
Elimu ya kompyuta.
Sote tunaufahamu umuhimu wa kompyuta katika dunia ya leo.Tumefundishwa vitu vya ajabu kwa muda mrefu,tumepoteza nguvu&muda bila kusaidia taifa letu.
Ilitakiwa tufundishwe vitu Kama web design, freelance,how to surf the web,usalama wa mtandao,jinsi ya kutumia mitandao ya kijamii Kama Facebook kwa ajili ya uzalishaji
Kinachosikitisha ni kwamba watoto wanatumia muda mwingi kucheza game,kupost&vituko vingi.

Elimu ya fedha.
Kuna baadhi ya wazazi wanaamini watoto hawatakiwi kuwa na pesa,hivyo huamini wakikua ndipo waitafute pesa.Kumpa mtoto pesa kunamjengea uzoefu,akiitumia vibaya atajifunza.Mtu aliyeshika pesa tangu utotoni ni vigumu kufilisika kwani anao uzoefu wa kutosha.
Inasikitisha mtu unakua hujui hata kutumia ATM mpaka umuite mlinzi akusaidie,wakati wewe umemaliza kidato cha sita,mtu hajui credit au debit card,hajui payment methods za mtandaoni.Kuna watu hawajui hata kujaza documents za fedha wakiwa benki hadi amuite muhudumu.Wazazi&walimu wafundishe banking in practice,wahamasishe watoto wawe na account bank,wajue ishu za riba,ishu za pesa ya kidijitali.Hii itasaidia watu wengi kuwa na ufahamu wa fedha hivyo kulisaidia taifa kwa namna mbalimbali

Saikolojia sahihi ya mapenzi.
Vijana wengi wanateswa na mapenzi.Hii ni kwa sababu hakuna mwongozo wa kitaifa wa kuwaelewesha kuhusu mapenzi.Mapenzi ni swala la experience au uzoefu lakini tungepewa maarifa sahihi ingekuwa vizuri zaidi.
Silabasi ya mapenzi ipo kwenye love story za kikorea au kifilipino ambazo watoto huangalia (hasa watoto wa kike) ambapo hujifunza mapenzi ya kweli,usaliti nk.Kwenye mapenzi ya kweli huwa wanaona wahusika wa filamu wanaopendana kwelikweli kwa kupeana zawadi za birthday za gharama,wanatoana outing za gharama (wanakula bata sehemu nzurinzuri),wanakunywa pombe,misosi safi,wanaogelea,safari nzuri nk.Mtu huyu akishakua Saikolojia yake inakuwa imeshaathiriwa na hizo movie.Hivyo atatamani maisha ya gharama,kwa hiyo atachagua mchumba mwenye hela ili akidhi tamanio lake analoliona kwenye filamu.Hivyo huamua kutafuta masponsa waume za watu wakidhi matakwa yake,na hii hupelekea wengi wao kupatiwa magonjwa &mimba zisizotarajiwa.
Kwa kugundua hili kundi kubwa la vijana wa kiume ambao asilimia kubwa ni makapuku huamua kufake maisha ili kuwatafuna wadada
Vijana wengi wanawaza sana mapenzi.Hii ni kwa sababu hawapewi ushauri wa kisaikolojia namna gani wakabiliane nayo.Mfano,unakuta kijana anamuwaza crush wake,je hajui kuwa Kuna wanawake wengi na wazuri zaidi ya huyo?je, ana pesa kuhudumia?
Kwa nini vijana hawajitengi na ngono zembe? Psychology
Kijana wa kiume unaamini mapenzi ya kweli?na unalalamika mademu wanakukataa?Elewa uhalisia acha kulialiaInapendwa pesa sio wewe.Wekeza nguvu zako uitafute.Labda Kama una mvuto wa wanawake itasaidia sana.
Psychology! Psychology! psychology!

Kuna vitu vingi vingine tumevikosa!

#Thanks.
 
Ndo mana mimi sikubaliani na ile synopsis ya ulaya kuhus magonjwa ya akili afrika. Malez y watoto wa kiafrika huwa tofaut sana na nchi nyingine... Mtoto wa miaka 4 akilia sana wanaita njuguyugu' mwishoni anaambulia kichapo pamoja na kulia kwake kwa madai ana nongwa. Kuna ugonjwa unaitwa bipolar na baadhi ya vigezo ni kuongea sana, kutumia hela hovyo, kukosana na watu wa karibu na kujigamba mda wote!! Hii afrika kwa mm inawez kuwa 'fully problematic' sabb mazingira ya vijana wa kiafrika na 'reaction' yao katika 'abnomal situation' inwez kuwafanya wote kuonekana wagonjwa wa akili... Ykiangalia jinsi ya wanaomaliz chuo kurud mtaani wanawez kuwa wagonjwa takriban wote.
Kama kuna mtu hajaelewa aje dm ntamuelewsha
 
Hapo kwenye fedha wanakufundisha hasa kwenye suala la usiwe na fedha, yaani ikiwezekana uendeleze umaskini wa ukoo, na maneno ya ajabu kama fedha haioti kwenye miti, wakati ukweli fedha ni karatasi na karatasi inatokana na miti, na maneno mengi ya kukufanya usiwaze wala usione ni fahari kuwa na fedha. Kila mwenye fedha naitwa maneno magumu magumu tu mara beberu, bwenyenye, freemason, mchawi, mtoa kafara alimradi tu usisogelee kwenye kutafuta fedha. Mbaya zaidi haya yanafanyika ukiwa bado unatengeneza subconcise mind ndio wanaijaza ujinga huo wote maana ukishavuka miaka saba tayari subconcise mind yako imejaa unakuwa na kuongeza vichache kwa tabu sana, ndio maana hata ukiwa mkubwa unatamani lakini unatumia nguvu sana kwa sababu subconcise mind yako imeelemewa na ujinga wa jamii waliokuwa wanakufeed ukiwa mdogo.

hayo hapo juu yana fanyika ila wewe unapokuwa mtu mzima unapaswa kuchagua kutengeneza upya unachokijua kama ukweli unaachana na ujinga uliomezeshwa unatengeneza vya kwako, maana kati ya wote wa rika lako mlimezeshwa ujinga huo huo, lakini wapo walioamuamua kuandika vya kwao baada ya kugundua ujinga aliomezeshwa kimya kimya na kubadilisha maisha yao na ya watoto wao.

Ukirudi kwenye jamii hiyo uliyotoka na kujaribu kurekebisha unakutana anachokiita Plato allegory of the cave, utakuwa kama achezae ngoma mbele yao ukiwaambia wanalishana matango pori, wanavyoviona ni vivuli tu wala sio vitu halisi
 
Hakika ni kweli kwabisa, ndiyo maana mataifa yaliyoendelea yanatuacha mbali sana...
 
Tumeliwa Sana Ndugu Zangu
Tumechelewa Sana Ndugu Zangu
Tumelaliwa Sana Ndugu Zangu
Tumehomolwa Sana Ndugu Zangu

Najua Mmenielewa Ndugu Zangu
Mabeberu Yametuchelewesha Mno
Tanzania Ni Tajiri
Tutaanza Kuzalisha Nguo Zetu Halafu Tutavaa Na Kuwauzia Ulaya Mitumba.

Haa Haa.......
Nawa~Zoom!!!!!
 
Back
Top Bottom