mediaman
JF-Expert Member
- Mar 20, 2011
- 451
- 687
Je, unapenda kuishi maisha marefu? Kwa ujumla, hakuna mtu asiyetaka kuishi miaka mingi na kuwa na afya njema. Wanasayansi na wataalamu mbalimbali wamethibitisha kuwa ukizingatia mambo yafuatayo unaweza kujiongezea miaka au umri wa kuishi duniani:
1. Hakikisha unakula vyakula vyenye virutubisho vyote muhimu
2. Epuka unene uliopitiliza. Uzito wa mwili wako usizidi viwango vya uzito vinavyokubalika kiafya
3. Usivute sigara
4. Fanya mazoezi ya mwili angalau dakika 30 kila siku na unywe maji ya kutosha
5. Usikae kivivuvivu - uchangamshe mwili wako kwa kufanya kazi
6. Epuka msongo wa mawazo; ishi na wenzako kwa furaha
7. Zingatia sheria za usalama barabarani
8. Jitahidi mara kwa mara kwenda hospitali kupimwa afya yako
9. Epuka ulevi
10. Pata muda wa kutosha wa kulala usingizi.
Wasomi wa Maandiko matakatifu, wamegundua jambo jingine linaloweza kumfanya mtu aishi miaka mingi. Jambo hili tunalisoma katika kitabu cha Waefeso 6:2-3(BHN). Imeandikwa hivi: “Waheshimu Baba na mama yako,” hii ndiyo amri ya kwanza ambayo imeongezewa ahadi, yaani, “Upate fanaka na kuishi miaka mingi duniani.”
Kwakuwa ahadi hiyo imetolewa na Mungu mwenyewe, ni hakika kwamba tukitekeleza agizo hilo - tukiwaheshimu wazazi wetu, Mungu atafanya kama alivyoahidi - atatupatia maisha ya heri na kutuwezesha kuishi miaka mingi duniani.
Hiyo ni siri iliyofichika kwa wengi, lakini leo imefunuliwa kwetu!
Na niaminivyo mimi ni kwamba, baba na mama sio wale tu waliotuzaa, ni pamoja na wote wenye umri unaozidi au unaolingana na umri wa wazazi wetu. Tuwaheshimu wote. Tusikwaruzane nao.
Tusiwanyooshee vidole. Tusiwakaripie. Tusiwadharau hata kama tunaona wamepitwa na wakati.