Vitu vizuri ambavyo madikteta 05 wamefanya na kuacha historia duniani

MSEZA MKULU

JF-Expert Member
Jul 22, 2011
3,763
5,591
1:ADOLF HITLER
129958-004-C9B8B89D.jpg

Pamoja na yote, Hitler atakumbukwa kama kiongozi wa kwanza kuanzisha harakati za Kuzuia Matumizi ya Sigara ili kuepusha madhara yake kwa raia (Anti-smocking compaign).

Ndie aliyehamasisha wanasayansi wake kufanya utafiti wa kisayansi wa madhara ya sigara. 1943 mwanasayansi wa kiNAZi aligundua sigara Inasababisha KANSA na Aliokoa maisha ya wanawake zaidi ya 20000. Sifa za ugunduzi huu ziliyoyoma maana vita vilipoanza mradi ukahafifishwa na kumpa sifa ya ugunduzi huo mmarekani baada ya anguko la wanazi.

2: Genghis Khan: ALIANZISHA SHERIA NA UHURU WA KIDINI
geng.jpg

Huyu jamaa aliua watu zaidi ya 40 Millioni karibu 12% ya watu wote waliokuwepo duniani maiti hao wanasadikika kudisturb kiwango cha carbon dioxide duniani miaka ya 1208.Pamoja na yote Huyu jamaa alianzisha Sheria(LEgal Code) zilizokuwa zinafanya kazi dola yake yote ya MONGOL na Hadi yeye akikosea ashughulikuwe. Pia aliweka uhuru wa dini na hata kuondoa taasisi za dini zisilipe kodi.

3:MUAMMAR GADDAFI: alianzisha Mradi Mkubwa wa umwagiliaji kuwahi kuwepo Duniani
Muammar-Gaddafi-Libya1.jpg

img_9770.jpeg

Mwaka 1969 huyu jamaa aliingia madarakani kwa mapinduzi na kuangamiza kila aliyempinga hata kutuma vikosi vya wauwaji kuwatafuta maadui zake nje ya nchi hiyo. Nchi nyingi za magaharibi zilimuona kama mtu hatari.

Lakini chini ya Utawala wake wa chuma, Watu walisoma bure, walitibiwa bure, Umeme bure, Wakati anaingia madarakani mji wa Benghazi ulikuwa hauna maji, akaanzisha Mradi wa kuchimba mto hadi huko uliowapa maji 70% ya walibya. ALikuwa na mpango wa kufanya jangwa lote liwe la kijani hadi pale figisu za wazungu zilipoanza miaka ya 90 na vikwazo pia kufuatiwa na mapinduzi ya 2011.

4:FIDEL KASTRO ALIFANYA MAPINDUZI YA AFYA NA ELIMU CUBA
Fidel-Castro.jpg

Alipoingia madarakani, alifanya nchi ya Cuba kuwa ya chama kimoja. Huku maelfu wakikimbilia uhamishoni, wengine wakifungwa na wapinzani wake kuuawa.

Cha ajabu, CUBA na US wote wana LIfe expectance sawa ingawa Marekani wametumia matrillion 20% zaidi. Akiingia madarakani 1959 1/4 ya Cuba walikuwa wajinga lakini leo Hakuna mtu mzima ambaye ni ILLITERATE/mjinga.

Aliweka mipango mikali kupambana na majanga ya kitaifa. Mfano Kimbunga GUSTAV hakikuua mtu hata mmoja Cuba lkn kilivyofika Marekani kiliua watu zaidi ya 26 jimbo la Louisiana.

5:AUGUSTO PINOCHET: "kafanya muujiza wa mapinduzi ya kiuchumi CHILE"
pinochet-democracyInBlood.jpg

Alipoingia madarakani watu 3000 walipotea hadi kesho, kafunga na kutesa watu zaidi ya 28,000 wakiwemo Rais wa sasa na mama yake. Mwaka 1973 aliingia madarakani Baada ya mporomoko wa uchumi kwa njia ya mapinduzi makali ya kivita.

Ndipo aliwaajiri kikundi cha vijana graduates na wataalamu wa uchumi kutoka Chuo kikuu cha Chicago "Chicago boys". kipindi hiki kinajulikana duniani kama "CHILEAN ECONOMIC MIRACLE" baada ya Mfumuko wa bei kushuka kutoka asilimia 375 hadi 9.9 ndani ya miaka 7. JAPO aliacha pengo kubwa kati ya maskini na matajiri.

Karibu kwa maoni, michango na changamoto.

Kila kibaya kina zuri lake.
 
Mhh hapo hakuna ushahidi maana hakuna Dictator duniani aliyewahi kukabidhi madaraka kirahisi,. Ingawa kila mtu anamaoni yake nimeona wengine wanamuita Benevolent Dictator lakini kiukweli Baba wa taifa mwisho wa siku atabaki kuheshimiwa kwa kuliunganisha taifa hili lenye makabila zaidi ya mia kuwa kama familia moja. Fikra na ubunifu wake umelijengea taifa misingi imara ya upendo na amani.
 
Ndio mana Mkapa alisema watu wawe wanasoma wanafanya analysis... Al Ghadafi hakuua hata nzi alipoingia madarakani...aliingia kwa amani kabisa na mambo mazuri aliyofanya yakamjemgea chuki na akina Hillary clinton wakaaamua auwawe...Castro hakua dikteta pia labda kama neno hilo mnalitumia ili kuwaridhisha wazungu ambao wana madikteta wengi sana anzia malkia elizabeth na wafalme kibao lakini hawasemi
 
Mhh hapo hakuna ushahidi maana hakuna Dictator duniani aliyewahi kukabidhi madaraka kirahisi,. Ingawa kila mtu anamaoni yake nimeona wengine wanamuita Benevolent Dictator lakini kiukweli Baba wa taifa mwisho wa siku atabaki kuheshimiwa kwa kuliunganisha taifa hili lenye makabila zaidi ya mia kuwa kama familia moja. Fikra na ubunifu wake umelijengea taifa misingi imara ya upendo na amani.
Ukitaja maovu yake tu JELA MIAKA 80
 
Kwani yeye alikuta mapigano ya kikabila?
 
Ndio mana Mkapa alisema watu wawe wanasoma wanafanya analysis...Gahadafi hakuua hata nzi alipoingia madarakani...aliingia kwa amani kabisa na mambo mazuri aliyofanya yakamjemgea chuki na akina Hillary clinton wakaaamua auwawe...Castro hakua dikteta pia labda kama neno hilo mnalitumia ili kuwaridhisha wazungu ambao wana madikteta wengi sana anzia malkia elizabeth na wafalme kibao lakini hawasemi
kwa mtazamo wangu unachanganya vitu na nyakati, 1969 kampindua sultan Idris. Hillal Clinton amekuwa waziri wa mambo ya nje miaka ya 2000 hakuna uhusiano hapo. Ni kweli ili aestablish regime (islamic socialism) yake ilibidi atumie Udicteta. Mfano kama amiri jeshi mkuu na Rais alianzisha General Peoples Committee (GPC) kama aina ya democrasia lakin mwisho wa siku maamuzi yote yalibaki kwake. Kuanzia miaka ya 80 hadi anauwawa hapo ndio hizo siasa za west zilipoanza kutaka kumdhoofisha kutokana na wivu wa rasilimali yake. Unadhani kwa nini amsupport Idd amin pamoja na unyama wote unaosemekana Idd amin aliwafanyia waganda lkn yeye apeleke hadi askari wake wa miguu. ikumbukwe hii ilikuwa ni miaka ya 70.
 
Mfalme Mbowe

Kwa kubadili gia angani na kuuza chama kwa mafisadi

Huu ufisadi ulioko CDM unakukera leo kiasi kila uzi unauwaza !!! Lakini ulipokuwa ndani ya Ccm na wengine waliopo huko hawakuwahi kukukera wala kuthubutu kuhoji (UNAFKI)

Pamoja na kasoro zake Mbowe ameonyesha leadership na kuikuza CDM
 
Ndio mana Mkapa alisema watu wawe wanasoma wanafanya analysis...Gahadafi hakuua hata nzi alipoingia madarakani...aliingia kwa amani kabisa na mambo mazuri aliyofanya yakamjemgea chuki na akina Hillary clinton wakaaamua auwawe...Castro hakua dikteta pia labda kama neno hilo mnalitumia ili kuwaridhisha wazungu ambao wana madikteta wengi sana anzia malkia elizabeth na wafalme kibao lakini hawasemi
Castro ni controversial pande mbili zote ni sawa, Dicteta au mkombozi wa wanyonge.
Ikumbukwe baada ya kumpindua kijeshi Fulgensio Batista 1959 Hakuwahi kuchaguliwa hadi alipomkabidhi ndugu yake madaraka. Magazeti yaliyopimpinga yalipigwa marufuku, hakuna kudai haki, maelfu ya wacuba walikimbilia frolida na miami us. Mfano mwaka 1980 aliwaita waje kuchukua ndugu zao, meli liyowaleta cuba wakati wa kurudi castro aliwajaza wagonjwa wa akili, wafungwa, watu wenye matatizo katika jamii akawajumuisha na ndgu zao wote wakapelekwa US bila hiyari yao.
Pamoja na Yote Africa na dunia kwa ujumla haiwezi kubeza mchango wa castro. Huyu ni kipaji cha aina yake.
 
Kama unavyosema Castrol ni issue nyingine. NI vigumu kusema kuwa Castrol in dikteta, tabia moja wapo ya madikteta ni kujilimbikizia mali na kutumia mamlaka walio nayo kwa faida yao. Wengi huwa wakiishi kama Mungu watu na kutumia njia mbali mbali kujaribu kuwaaminisha wananchi wao uhalali wa utawala wao. Ushahidi uliopo hata kwa kutumia vyombo vya habari vya maadui wake vinasema wazi kuwa Castrol hajajilimbikizia mali wala kutumia rasilimali ya taifa kwa manufaa yake. Ni kweli hakujawahi kuwa na uchaguzi Cuba, si yeye Fidel au mrithi wake Raul walichagulia kwa kura. Unaweza sema huo ni udikiteta. Wengi wanasema wakati akiwa Rais, Castrol alikuwa anatawala kila Nyanja na sekta katika maisha ya Cuba. Nchi ya Cuba ni nchi ya kimapinduzi na hawajawahi ficha hilo. Walitekeleza mapinduzi ndani ya Cuba tena mapinduzi ya Kijamaa na waliamini katika mapinduzi na walisaidia nchi au binadamu yo yote aliyekuwa katika harakati ya kuleta mapinduzi popote duniani. Cuba iko maili 90 tu kutoka Marekani nchi yenye nguvu kuliko zote duniani na yenye siasa za kibepari. Bila ulinzi madhubuti Mapinduzi ya Cuba yasingedumu kamwe. Katika hali kama hiyo isingewezakana kabisa kuwa na mfumo wa demokrasia Cuba. Castrol ameweka misingi mizuri sana Cuba kiasi hata haya mabadiriko yanayokuja sasa yataleta faida sana Cuba kwa kuwa Wa Cuba wana elimu sana na huduma nyingine za jamii ziko Zaidi hata ya nchi zilizoendelea hususani kwenye Nyanja ya huduma za afya. Dalili zote zinaonyesha Cuba itafanikiwa na mabadiriko kama China ilivyofanikiwa. Fidel alikuwa kiongozi mwenye kufuata kanuni sana haswa katika suala la kupinga kuonewa. Alipoulizwa jambo gani alilolifanya katika uongozi wake ambalo anajivunia Zaidi alitaja msaada wake katika kupambana na majeshi ya uvamizi ya makaburu Angola kama ndio jambo lililotukuka Zaidi ya yote. Afrika inatakiwa ijue vizuri mchango wa Cuba katika ukombozi wa kusini mwa Afrika. Majeshi ya Cuba Angola yalibadidirisha kabisa mizani ya nguvu za kijeshi kusini mwa Afrika. Jeshi la Afrika Kusini ya makaburu halikuwahi kushindwa hata siku moja kwenye uwanja wa vita mpaka pale lilipopaka pigo kule kusini mwa Angola kwenye mapambano ya Cuito Cuanavale mwaka 1986. Makaburu walikimbizwa mpaka Namibia, Angola kwa mara ya kwanza tangu Uhuru wake wakawa hawana majeshi ya uvamizi kwenye ardhi yao, uhuru wa Namibia ukapatika, na ajenda ya haki za mtu mweusi ndani ya Afrika Kusini zikaanza kusikilizwa ndani ya chama cha wazungu kilichokuwa kinatawala wakati huo. Ndipo vyama vya siasa vya watu weusi kuruhusiwa na wapigania uhuru kama wakina Mandela kuachiwa huru. Cuba ilitoa msaada wa wanajeshi na vifaa vya kivita zikiwemo ndege, vifaru na makombora ya kisasa kabisa ya kutungulia ndege ilikufanikisha adhma ya kumtoa kaburu na kumfunndisha adabu pale Angola. Na Cuba haikulipwa kitu, ilisaidia katika misingi ya kibinadamu. Tunaweza sema mengi sana hapa, lakini naamini historia itakuja kutuambia kama tunaweza kumweka Fidel Castrol kwenye kundi la madikteta au la...!!!

Inapokuja kwenye suala la wale Wa Cuba walikimbilia Miami, USA, hakuna MCuba alielazimishwa kwenda serikali ya Marekani katika kuikomoa Cuba ilitangaza kuwapa haki za ukimbiza haraka sana Wa Cuba wote wanaoikimbia nchi yao. Wananchi wengine wa Cuba wakata kuondoka Castrol akasema anaetaka kwenda na aende na wapo wengi waliokuwa magerezani waliotaka kwenda wakaruhusiwa kwenda kwa HIYARI YAO wala si kwa kulazimishwa. Haya wanayasema wenyewe Wa Cuba waliokimbia Cuba ambao kwa sasa wanaishi Marekani.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom