Vitu viwili vinavyokinzana kuhusu mafanikio yako

Galacha Maestro

JF-Expert Member
Sep 29, 2011
1,334
2,000
VITU VIWILI VINAVYOKINZANA KUHUSU MAFANIKIO YAKO.

Watu wengi wanafeli, watu wengi wanashindwa kufikia ndoto zao na hata kuanza hatua ya kwanza kuelekea ndoto zao kwa asilimia kubwa ni kutokana na ukinzani mkubwa unaoendelea ndani ya mtu mwenyewe.....Kuna kitu ndani ya mtu kinapenda sana mafanikio na kipo tayari kufanya kila kitu ili kuyaleta hayo mafanikio lakini pia kuna kitu ambacho ndani ya mtu kinapenda mafanikio lakini hakipo tayari kulipa gharama za mafanikio.....Ukinzani huu mkubwa unaoendelea kwa mtu ndiyo huzalisha washindi au watu walioshindwa. yaani ukiona mtu kafanikiwa basi jua kuwa kuna mapambano makubwa yaliendelea ndani yake na akayashinda na aliyefeli basi jua kwenye hayo mapambano ndani yake alishindwa......Biblia inasema "MWILI HUSHINDANA NA ROHO".....Lakini pia inasema " ROHO I RADHI LAKINI MWILI U DHAIFU"

MWILI

Mwili umeumbwa kupenda kufanya vitu ambavyo vinaupa raha, na bahati mbaya au nzuri nisema vitu vinavyoleta mafanikio huwa vinaufanya mwili ukose raha kabisa.....Hivyo kwa tafsiri fupi kabisa tunaweza kusema "Mwili unafurahia sana mambo yanayosababisha kufeli kuliko kufaulu"

Nina ujasili mkubwa wa kusema "MWILI umesababisha masikini wengi na failures nyingi duniani kuliko kitu kingine chochote duniani"..... Ukiona mtu ni mvivu jua ni MWILI, ukiona mtu hasomi vitabu basi jua ni MWILI unasababisha, ukiona mtu analala masaa mengi basi jua ni MWILI unamuendesha, ukiona mtu anapenda sana SEX na ana wapenzi zaidi ya mmoja basi jua amekubali kuendeshwa na MWILI, ukiona mtu weekend anashinda clubs kujirusha wakati wenzake wapo kupambana dhidi ya ndoto zao basi jua kuwa huyo mtu anaendeshwa na MWILI......Ukiona mtu amepata HIV kwa aslimia kubwa ni watu waliokubali kutumikishwa na MWILI.

MWILI unapenda Raha, MWILI unataka muda wote ukae na marafiki kupiga story za udaku na skendo za wasanii hauko tayari kusoma vitabu na makala za kuongea maarif, MWILI unazifurahia dhambi kuliko matendo mema.....HAKIKA MWILI NI CHANZO CHA UOVU WOTE NA FAILURES ZOTE DUNIANI!!

" Kumbuka kuwa Ukiamua kuufuata MWILI basi jua kuwa utakuwa umeamua kujiweka kwenye lile kundi la masikini wa kutupwa na Failures.

ROHO.

Huku ndiko mahali ambalo chemichemi za uzima zinatoka au kwa lugha nyepesi tungeweza kusema "Mahala ambapo chemichemi za mafanikio zinatoka"...... Roho ipo radhi kuifikia miisho mikubwa ya ndoto yako, Roho ipo radhi kufanya vitu vinavyoumiza, Roho ipo radhi kufanya mambo ambayo ni makubwa yakuushangaza ulimwengu.....ROHO ipo tayari kuumia, kuteseka, kwa ajili ya jambo jema la badae.....Roho huangalia potential halisi ambayo Mungu ameweka ndani yetu, na ndiyo maana hata leo ukiazimia kuwa unataka kupambana uwe Raisi wa Tanzania basi Roho ndiyo hukubali na kusema kuwa mbona hili ni suala dogo sana, lakini mwili huanza kuangalia watu walioshindwa, utasikia mwili ukimnong'oneza Roho kuwa "Lowassa alikuwa waziri mkuu lakini alishindwa kuwa Rais utaweza wewe mtoto wa mchimba chumvi??".

NINI KIFANYIKE??

Inachokitaka ROHO sikuzote MWILI huwa unapingana nacho.....ROHO siku zote huwa inapenda kufanya vitu ambavyo ni Muhimu viwe vinaumiza au vinafurahisha ROHO yenyewe iko tayari kivifanya, na kama tunavojua kuwa sikuzote vitu vinavyoleta mafanikio huwa ni vigumu, vinaumiza na vinaunyima mwili raha......Lakini MWILI wenyewe unapenda na kufaurahia kufanya vitu vinavyoupa raha tuu, MWILI haujawahi kuwa tayari kufanya vitu ambavyo ni vigumu, vinautesa, vinaumiza wala vinaunyima raha.....Na kwa bahati mbaya au nzuri ni kuwa Mafanikio yamejificha kwenye vitu ambavyo ni vigumu, vinaumiza, vinatesa mwili na vinavyokosesha raha......HAPA NDIPO HUTENGANISHA KATI YA WATU WANAOFANIKIWA NA WATU WASIOFANIKIWA......KWANI WATU WANAOFANIKIWA HUISHI KWA KUITII ROHO NA WATU WASIOFANIKIWA (FAILURES) HUISHI KWA KUUTII MWILI.

Sasa ili ufanikiwe ni lazima uwe mtu wa kutokukubaliana sana na MWILII.....MWILI hauwezi kukufanya ufanikiwe ila upo tayari 100% kukufanya ushindwe na kuwa failure..... Ndiyo maana unaweza kulala saa kumi na mbili jioni ukaamka asubuhi saa mbili lakini bado mwili ukawa unakutaka uendelee kulala, utasikia "Lala kidogo kama nusu saa, jana ulichelewa sana kulala", usijitese maisha ni simple tuu, kulala ni muhimu kwa afya..... na maneno mengine kama hayo huwa yanatoka kwenye mwili ambao huwaga haupendi shuruba.

Mafanikio ni nini?? Mafanikio ni uwezo wa kuufanya MWILI utii matakwa ya ROHO.....Sasa ili uwe miongoni mwa watu watakaofanikiwa kwa kiwango cha hali ya juu ni lazima kwa asilimia kubwa uishi kwa kuupa MWILI comands au amri zitokazo kwenye ROHO ambayo yenyewe ipo radhi kwa Mafanikio yako 100%.

Kumbuka Mafanikio siyo kitu rahisi, Wale walio tayari kujitesa na kuamua kuongozwa na ROHO na kupuuzia kile ambacho MWILI unakitaka basi hao ndio Wanaofanikiwa!!

C&p

Sent using Jamii Forums mobile app
 

BabaMorgan

JF-Expert Member
Dec 18, 2017
1,365
2,000
Kweli kwa kuongeza maisha ya mafanikio yanahitaji discipline ya hali juu sana.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom