Vitu vitano(5) vya kuweka kwenye chakula cha kuku wako

Mp steve

Member
Feb 28, 2019
26
12
1.Protini.
2.Mafuta.
3. Wanga.
4. Madini.
5. Vitamini.

1.PROTINI
Ni aina ya vyakula ambavyo kazi yake kubwa ni kukuza mwili navyo ni kama ifuatavyo, Mtama, Dagaa, Alizeti na Soya. Hivi vyote inategemeana na maeneo uliko, nini kinapatikana kwa urahisi.

2.WANGA.
Ni aina ya vyakula ambavyo kazi yake ni kuupa mwili nguvu. Navyo ni kama ifuatavyo;mahindi yaliyo balazwa, pumba ya mahindi na pumba ya mpunga.

3.MAFUTA.
Ni aina ya vyakula ambavyo kazi yake kubwa ni kuupa mwili joto pamoja na kulainisha mmeng’enyo wa chakula mwilini. Kundi hili kuna vitu vifuatavyo;mashudu ya alizetinamashudu ya pamba.

4.MADINI
Hapa kuna madini ya aina mbalimbali ambayo kazi yake kubwa ni kuimarisha mifupa na ganda la juu la yai pia. Na haya madini ni muhimu sana, kwa sababu yanakazi kubwa katika mwili wa kuku. Yanamwezesha kuku kutembea vizuri na kwa ukakamavu.

Pia yai la kuku ili liwe imara lenye ganda gumu lazima apate madini ya kutosha. Bila kusahau madini yanasaidia kuku kutonyonyoka manyoya yake. Madini hayo ni kama ifuatavyo, mifupa,Chokaa ya kuku, D.C.P hizuia kudonoana, kula mayai, maganda malaini. Pia uimarisha maganda ya mayai, husaidia kuongeza mayai.

5.VITAMINI.
Ni aina ya vyakula ambavyo vinapatikana sana kwenye mbogamboga, lakini kazi yake kubwa ni kuimarisha mwili uwe vizuri kama vile kuona, kuwa na manyoya imara na afya bora. Kundi hili linavyakula kama vifuatavyo, mchicha, chainizi, spinachi na majani ya mpapai.

KUMBUKA:
Pia katika maduka ya mifugo kuna vitamini zinauzwa ambazo hutumika pia kama mbadala wa mazingira yetu yalivyo kuna baadhi ya maeneo kupata mbogamboga ni changamoto. Kuna “vitalyte” ni nzuri kwa kuku.

Asante

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu Mp Steve ungeweka na formula, ratio namna ya kuchanganya hicho chakula!
 
safi sana pia ungenifafanulia na ratio ya kuweka kwa chakula na idadi kuku wangapi, vipi kuhusu chakula cha bata na bata mzinga?
 
safi sana pia ungenifafanulia na ratio ya kuweka kwa chakula na idadi kuku wangapi, vipi kuhusu chakula cha bata na bata mzinga?
soon nitapost mkuu ila kuhus bata sina experience na hiyo mifugo, idadi ya kuku inategemea na ww mwenyew tu, kuku anaetaga anakula gram 80 had 130

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom