Vitu vitano (5) vya kuvifahamu kwa mpenzi wako ili uishi naye vyema

Ben Zen Tarot

JF-Expert Member
Dec 13, 2014
3,900
6,657
1. HAKIKISHA UNAFAHAMU HASIRA ZAKE ZIKOJE

Kila mtu huwa anakasirika hivyo ili uweze kuishi na mpenzi wako vizuri Unatakiwa ujue hasira yake ikoje? Je! Huwa anakasirika haraka au anachelewa kukasirika? Na Kama akikasirika huwa anaonekanaje? Akikasirika huwa anakuwa na lugha ya Aina gani? Hapo utaishi naye vyema.

2. TAMBUA VIPAUMBELE VYAKE

Kila mwanadamu ana vipaumbele vyake, Mimi Nina vipaumbele vyangu na wewe una vipaumbele vyako kwa maana hiyo unapaswa ujue mpenzi wako anapendelea vitu gani hasa kwenye maisha yake, hiyo itakusaidia kujua namna ya kuishi naye kulingana na vipaumbele vyake

3. IMANI YAKE JUU YA MAISHA

Imani ni kitu kinachoendesha maisha ya watu kwa maana hiyo huyo mpenzi wako naye ana Imani juu ya maisha na Imani hiyo lazima uitambue. Kwahiyo kazi yako ni kuhakikisha unatambua kwamba yeye kwenye maisha ana amini nini? Moyo wake una Amini Nini juu ya wanawake/wanaume katika maisha?

4. JUA VITU ANAVYO VIPENDA NA ASIVYO VIPENDA

Kila mwanadamu Kuna vitu hutamani afanyiwe na mwanadamu mwenzake. Kwahiyo unapaswa ujue mpenzi wako vitu gani hapendi wewe uvifanye na anapenda vitu gani uvifanye. Hii itasaidia kuokoa migogoro isiyokuwa na tija yoyote ile.

5. FAHAMU MADHAIFU YAKE JAPO KWA SEHEMU TU

Hakuna aliye mkamilifu hilo twajua, kumbe hata mpenzi uliye naye ana MADHAIFU yake na kwa kawaida MADHAIFU hukera kwahiyo ili uweze kuepuka unatakiwa ujue Kuwa mwenzako ana shida hapa na hapa ili ikitokea amefanya tofauti wewe usipate tabu Bali uwe na moyo wa kumwombea ili Mungu amsaidie kwenye MADHAIFU yake.
 
1. HAKIKISHA UNAFAHAMU HASIRA ZAKE ZIKOJE

Kila mtu huwa anakasirika hivyo ili uweze kuishi na mpenzi wako vizuri Unatakiwa ujue hasira yake ikoje? Je! Huwa anakasirika haraka au anachelewa kukasirika? Na Kama akikasirika huwa anaonekanaje? Akikasirika huwa anakuwa na lugha ya Aina gani? Hapo utaishi naye vyema.
Njooni wajuvi
 
Wanawake wengi wanapenda hela Tu

Yaani hela Tu

Vyote hivyo vitano vina pesa au kukosa pesa

na wale waliochomewa nyumba walikuwa hawajui ivo vitu vitano(formula).hawa wanawake ni kuishi nao kwa akili tu
kila siku wa toa update za maisha kwa iyo ni muhimu ku download ili kuendana na maisha ya kila siku.
 
Jamaa
 
Kuna uzi wangu unaelezea hasira za wanawake hao waliochomewa nyumba watakuwa Wana base kwenye kundi mojawapo LA hasira za wanawake
 
Similar Discussions

8 Reactions
Reply
Back
Top Bottom