Vitu vinavyoitwa Home Work, Tuition na sasa Pre form One ni janga kwa mtoto

Ni kuuliza mbali na masomo yanauo tolewa mtihani na NECTA je kuna elimu nyingine mnawapa watoto? Internatuonal school wana hadi madarasa ya miziki na vyombo, wana michezo kila aina Je sisi?

Unazania labda kwa nini wahindi huwa wanaenda na watoto wao dukani? Unajua sababu?

Pale wana inject vitu kwa watoto wao nje shule
Embu tutajie mwana mziki unaemjua ambaye amesoma hizo international school unazozijua mana wanamziki wote wanajulikana
 
mleta mada kachanganyikiwa tu, shule ni shule, asilimia kubwa ya watu wanao pitia mazingira magumu ndio wanakua na akili za maisha mifano akina Steve Jobs aligundua Iphone leo ndio tunajitapa nazo bongo tu.
Stive job, bill gate, Zuckerburg wamesoma world class Universities acha kufananisha nasi.
Bill gate ni kama alianza 'twisheni'ya komputer mapema zaidi.Tofauti ni bill alisoma tuisheni ya teknolojia sisi tunasoma tuisheni ya General knowledge. Bill, Stive they were busy my dear!Soma historia ya Thomas Edson na Newton utagundua investment on time ni muhimu sana.No effort no achievements. Sasa chagua unataka mtoto awe busy na nini, hapo ndipo umahiri wake utakapojengeka.Bahati mbaya TZ hakuna tuisheni za kiteknojia.Etheopia wameanzisha center za 'after schools curriculum' wanafundisha Programming na robotics .Watoto wapo konki ingia you tube utawaona.
Suala hapa lisiwe mabishano Liwe nini tufanye, kipi kizuri/ kibaya.Wapi wanatoa nini, nani anatoa nini.Kuendelea kubishana ni kupoteza mda.
Hapa kuna wengi wanaoukubali mfumo uliopo na wachache wanaotaka mabadiriko.
Kwa kawaida wengi huwa ni watu wa kufuata mkumbo na wachache hulazimisha mawazo yao yakubaliwe.
 
Now unaingia kwenye silly stage.
Unaanza kuandika mambo ya kusikitisha au kutisha ili umtoe unayejadiliana nje ya mada ili akubaliane na wewe kwamba upo sahihi kitu ambacho kinajumuisha hisia.

Bahati mbaya mimi sio kidato cha nne na wala sisomi ili nifanye mitihiani.
Na mimi sipotezi muda humu sababu najua nini nakifanya humu jf na nini nakitafuta.

Mimi sio mmoja kati ya hao vijana wajinga unaowajua na ambao unawatetea.
Hivyo acha kugeneralize.

Najua nini nakiandika.
Sawa.
 
Back
Top Bottom