Vitu vinavyoirudisha nyuma nchi yetu Tanzania

raymbilinyi

Member
May 25, 2016
13
11
VITU VINAVYOIRUDISHA NYUMA NCHI YETU TANZANIA

Nchi yangu Tanzaniai ni tajiri sana katika rasilimali lakini bado nchi yetu ni miongoni mwa nchi masikini duniani. Kuna baadhi ya vitu ambavyo vinasababisha sana nchi yetu kuendeleea kuwa nyuma licha ya kuwa na uongozi imara na dhabiti katika awamu hii ya tano chini ya Mheshimiwa Rais Dr. John Pombe Magufuli. Nimeonelea leo ni jikite katika kuonesha baadhi ya maeneo ambayo yakitiliwa mkazo na serikali hii ya awamu ya tano na kuyarekebisha kwa haraka sana, itasaidia sana kuifanya nchi yetu Tanzania kuwa ya uchumi wa kati. Nimegusa baadhi tu ya maeneo tu ambayo serikali hii ya awamu ya tano tayari ishayafanyia kazi na bado inaendelea kuyafanyia kazi.

1. Mawasiliano (Communication) ndani ya serikali.
Sababu kubwa ambayo inaendelea kuikwamisha serikali yetu ni mawasiliano baina ya taasisi za serikali katika utekelezaji wa miradi au mipango serikali. Coordination na communication ni muhimu sana hasa inapofikia kipindi ambacho taasisi za serikali zinashindwa kufanya kazi kwa ushirikiano katika kutekeleza mambo muhimu ya serikali. Mfano wa kwanza tuanzie kwenye ufunguzi wa kiwanda kikubwa cha Juisi cha Bakresa, mawasiliano kati ya wizara ya nishati (Umeme) na wizara ya viwanda maana mpaka kiwanda kinafunguliwa umeme ulikuwa bado hauwekwa mpaka akanunua majenereta. Mfano mwingine vyuo vikuu kufunguka hata kabla bodi ya mikopo haijazitoa pesa za wanafunzi. mifano ni mingi sana ila niiombe serikali iusishe taasisi au wizara zote kabla mradi kufanyika au kuanza iliupate inputs za mashirika yote lengo likiwa ni kufanikisha mpango.

2. Ufisadi na tabia za wiziwizi (Dili).
Ni wazi nchi yetu ilikuwa imefikia pabaya sana hasa kwenye eneo la rushwa na tabia za wizi na kugeuza kila mradi wa serikali kuwa dili ya watu wachache. Serikali ya awamu hii ya tano chini ya Mh. Rais Dr. John Pombe Magufuli ameendelee kupambana na rushwa kwa vitendo. Watanzania wenye fursa aidha serikalini au kwenye mashirika waligeuza kila mradi wa serikali kuwa dili yao ya kujipatia pesa kitu ambacho miradi ilikuwa haitekelezi kwa wakati na tena kuwa chini ya kiwango. Hii vita isibaki ya mheshimiwa Rais wananchi wanahitajika sana katika vita hii kwa kukataa, kuvichua uovu hasa kwa vitendo ya rushwa. Walarushwa wafikishwe mahakamani na sheria ichukue mkndo wake na pia kuwaondoa wala rushwa serikalini itasaidia kupunguza kama sio kuondoa kabisa. Dili za wizi wizi uliwafanya nchi ya DRC Congo kuacha kuitumia bandari ya Dar es Salaam na kuhamia ya Beira Port.

3. Sheria za bodi ya manunuzi (PPRA).
Mapato mengi serikali yamekuwa yakitumika zaidi katika kufanya manunuzi ya bidhaa mbalimbali na hata kugharamia huduma za kitaalamu. Hiki ndio kichaka cha watu kujipatia pesa kwa mtindo wa ten percent (10%) na kusababisha bidhaa au huduma kununuliwa kwa bei kubwa sana na tena kupata bidhaa na huduma iliyo chini ya kiwango au kutokukamilika kabisa. Hapa niwazi serikali inahitaji sana kuzipitia upya sheria za manunuzi maana ndio mchwa kuu wa kula pesa za serikali maaana huduma yoyote au bidhaa yoyote ikipitia mchakato huu wa manunuzi (ppra) lazima bei itakuwa juu sana na hata ubora utakuwa wa chini na hata muda wa kupata huduma au bidhaa lazima itachukua muda mrefu sana. Mfano Mh. Rais kawatumia Mamlaka ya Ujenzi (TBA) bila ya kutumia Tenda au PPRA na gharama ya ujezi wa majengo 20 ya ghorofa 4 yanajengwa kwa shs billion 11 tu na tena kwa miezi mitatu tu wakati angetumia sheria za manunuzi gharama ingekuwa kubwa na ingechukua muda mrefu sana. Zipitiwe upya sheria hizi za manunuzi na kuwabana maofisa wote wa manunuzi kwakuwafuatilia mienendo yao kwakutumia vyombo vya usalama.

4. Makato mengi hasa kwenye mishahara ya watumishi.
Serikali ipitie upya makato hasa kwenye eneo la mishahara maana mtumishi anakatwa pesa nyingi sana katika mshahara wake kitu kinachowafanya aingie kwenye kutafuta dili na kujihusisha ma masuala ya rushwa ili waweze kujikimu kimaisha maana makato yamekuwa mengi sana. Mfano watumishi ambao walisoma vyuo vikuu kwa mkopo makato yao ya mshahara huwa karibu nusu ya kile anacho kipata kama mshahara. Mfano vyama vya wafanyakazi kama TUCTA, CHODAWU, CWT hawa nao hukata asilimia kubwa sana ya mshahara wa mtumishi wakati hata mrejesho wa hiyo fedha haijulikani inatumika wapi. Kazi kubwa ya pesa amabzo huenda kwa hivi vyama vya wafanyakazi huishia kulipana posho nyingi wakati wa vikao vyao kitu ambacho huumiza wananchi sana maana kinachokatwa ni kikubwa sana. Niiombe serikali kuondoa kabisa makato haya ikiwezekana haya ya vyama vya wafanyakazi iwe elfu mbili tu badala hii ya sasa ya asilimia tatu ili kumpunguzia wa mtumishi wa serikali mzigo huu ambao unamelemea sana na kumfanya atengeneze dili za rushwa ili tuajilipe mshahara.

5. Vyeti feki vya elimu husababisha wataalum feki.
Zoezi hili la ukaguzi wa vyeti vya elimu naomba liwe endelevu ili kupata watu wenye ujuzi na maarifa sahihi ambao watasaidia katika kuboresha hudumu za serikali. Hii pia husababisha serikali kupata watu ambao hawajakizi vigezo kwa nafasi walizo nazo kitu ambacho kinaweza kusababisha huduma mbovu, maamuzi mabovu, mipango miovu, miradi ya ovyo n.k. Serikali iendelee na hili zoezi na tuendelee kumpongeza Mh Rais Dr. John Pombe Magufuli kwakuamua kuanzisha huu ukaguzi katika taasisi zote za serikali maaana ni hatari kukaa na mtu aliefoji cheti cha taaluma ambayo kihalisia hajasomea.

6.Ukweli na Uwazi ndani na nje ya serikali.
Serikali iendelee kuwapa taarifa wananchi wote na kuweka wazi miradi na michanganuo yake ya matumizi ya pesa ambazo inatenga na kuzitumia. Kuhusisha pia waandishi wa habari, wahariri na kuwa karibu nao na kuwapa uhuru wakufanya kazi kwa uwazi na ukweli. Ukweli na uwazi uwepo katika mahakama zetu, miradi yetu, mipango yetu na mengineyo.

7. Siasa na Propaganda.
Ni waz sasa watu wamekuwa wakigeuza kila kitu kuwa siasa na kuendelee kuponda au kutengeneza propaganda tu ili mradi kumkwamisha Rais au miradi ambayo imepangwa kutekelezwa. Mfano ishu ya nchi yetu kununua ndege mbili za Bombadia watu wasiotutakia mazuri walikuwa wanajenga taswira kwa wananchi kuonesha serikali imechemka kutekeleza hili licha ya kutokuwa na ndege apo awali. Eneo lingine ni popaganda kwenye ishu ya bodi ya mikopo kutokuwapa wanafunzi elfu 66,0000 mikopo wakati ukweli ni kuwa wote wenye sifa watapata mkopo.

8. Kutoamini vitu vyetu vya nyumbani iwe pesa yetu, bidhaa zetu, wataalum wetu, viwanda vyetu, wasomi yetu, viongozi wetu n.k. Kasumba hiii ni kubwa sana maana watanzania kila kitu cha nyumbani hukosoa hata kama ni kizuri na hata kutotaka kununua bidhaa zinazo zalishwa nyumbani kwetu na kutegemea bidhaa ya nje. Mfano ni pale ambapo Mh. Rais Dr JPM anavyoirudisha nchi katika misingi bora na imara lakini bado watanzania hawamuapriciate wakati nchi zingine wanamtamani awe kiongozi wao wa nchi zao. Tubadilike sana maana tukiendelee na hii tabia hali haitakuwa nzuri maana hata tukianzisha viwanda vingi nyumbani lakini tukawabado hatuthamini vya nyumbani bado ni kazi bure.

9. Kutumia Mawakala aidha wa ndani au nje katika kila shughuli nyeti au makusanyo ya serikali yenye pesa.
Ni muhimu sana serikali kuongeza uwezo wa watumishi wake katika kufanya kazi zake hasa sehemu nyeti kuliko kubakia kuwapatia mawakala kwa kazi ambazo serikali inaweza kuzifanya yenyewe. Hii husababisha watumishi wa serikali kubakia watazamaji tu na kutoona wanaweza kwa kila jambo. Mfano ni bandarini kazi zote nyeti hukusanywa na mawakala aidha wa nje au wa ndani huku watumishi wa bandari wakibaki bila kazi na kuishia kuwa watazamazi. Mfano mwingine kwenye ukusanyaji wa kodi kweneye halmashari zetu, vituo vya basi, maji, umeme, mabango n.k hufanywa na mawakala kitu ambacho husababisha gharama kwa mtumiaji au mraji wa mwisho ambae ni mwananchi. Serikali ianze kuona umuhimu wa kutumia teknolojia katika kusimamia na kuthibiti rasilimali zetu na makusanyo kama ya "Web Based GIS" na mingine.

10. Kutoa elimu kila mara ya kuwafanya wananchi wanajituma, hamasa ya maendeleo, bidii ya kufanya kazi, nidhamu katika kazi, heshima kwa boss wako na mengineyo. Mfano hata kulipa kodi, kutumia mashine za EFD, Elimu inahitajika sana tena kila mara ilikuwafanya watu wanakuwa na uelewa.

Naomba kwa leo niishie hapa maana vitu ni vingi sana ambavyo vinatukwamisha sana kama nchi kusonga mbele kama nch katika kufikia uchumi wa kati. Niwaombe watanzania wenzangu tumuunge mkono Mh. Rais wetu Dr. John Pombe Magufuli na team yake ya uongozi maana kazi wanayo katika kurekebisha hali ya nchi yetu. Nimuombe kila Mtanzania tuungane sote kwa pamoja katika kukikisha nchi yetu inakwenda mbele kimaendeleo.....Asanteni..........TANZANIA KWANZA.
By
RRM.
Richard Mbilinyi
 
Ndege ilikuwa tayari about ku-take off, sasa tatizo rubani mpya kaja na equation hii hapa chini. Tunajaribu kuita maprofesa waje wa-solve, tukipata solution tutakuja kuangalia ushauri wako.

Hcl(aq) + KoH(aq)→H2O (l ) + KCl (aq )+Ct+Mt+l+K(t+1)=A,f(k)+ Mt/(1+r)
 
Naunga mkono hoja
Pasco
 
Tumbuatumbua nayo inarudisha nchi yetu nyumaa kwa maana unawalipa watu wawili kwa mujibu ya sheria ya kazi

Kwa hyo unamlipa aliye ofisini na aliye nje ya ofisi(aliyetumbuliwa) ndo maana mishahara imepanda Mara dufu na huku serikali haijawaongezea mishahara wake!

Namshauri Mh Rais akishatumbua bas atumbue na mshahara,
 
Mkuu yote uliyoyaandika ni tisa, warudishaji nyuma wa maendeleo ya nchi yetu ni hawa wahuni, mafisadi, wezi, wapokea rushwa, wasaini mikataba ya rasilimali za nchi ambayo haina maslahi kwa Tanzania na Watanzania. Wenyewe hupenda kujiita CCM.
 
Ndio mana tumeanza kuwatoa kwny nyumba za umma kwa sababu wamezidi ufisadi wizi ujambazi na ukwepaji kodi
 
Unahangaika bure. Tatizo la Tanzania ni UONGOZI MBOVU NA SIASA CHAFU!. Hakuna nyongeza!.
 
Baba umesahau mikataba ya madini, gesi, IPTL na kulinda maslahi ya mtu binafs kuliko ya Taifa
 
Tatizo kuu ni: Unapojaribu kuondoa/kukomesha ugonjwa wa malaria huku wakati huohuo ukitumia nguvu zote kuwalinda na kuwatetea mbu waenezao malaria!
 
Tumbuatumbua nayo inarudisha nchi yetu nyumaa kwa maana unawalipa watu wawili kwa mujibu ya sheria ya kazi

Kwa hyo unamlipa aliye ofisini na aliye nje ya ofisi(aliyetumbuliwa) ndo maana mishahara imepanda Mara dufu na huku serikali haijawaongezea mishahara wake!

Namshauri Mh Rais akishatumbua bas atumbue na mshahara,
Enzi zile mlikuwa mkilalamika kuwa hakuna hatua zinzochukuliwa, leo hatua za haraka na za makusudi zinachukuliwa imekuwa shida. TATIZO KUBWA LA NCHI HII NI WANANCHI KUTOJITAMBUA, NA WENGINE KUONA WANAJITAMBUA KUMBE NDO WAKO KWENYE TOPE KABISA.
 
Nchi itaendeleaje wakati wengine wanajiona ni bora kuliko wengine? Jonh Maken aliwekwa na Obama kua mshauri wake kuhusu mambo ya ulinzi japo wote waligombea urais.

Uku kwetu anapambana na Lissu ili ampoteze katika kutetea wananchi wake, eti wengine wanateuliwa kimkakati kuwathibiti wengine
 
Mkuu yote uliyoyaandika ni tisa, warudishaji nyuma wa maendeleo ya nchi yetu ni hawa wahuni, mafisadi, wezi, wapokea rushwa, wasaini mikataba ya rasilimali za nchi ambayo haina maslahi kwa Tanzania na Watanzania. Wenyewe hupenda kujiita CCM.
Uko sahihi 100%
 
Back
Top Bottom