Wanafunzi wengi wanapokwenda chuo, huwa na mitazamo chanya kabisa juu ya maisha yao ya chuo yatakavyokuwa ikiwa ni pamoja na ndoto hadithi za ndugu na jamaaa marafiki waliowahi kuwa wanachuo kabla yao.
Vijana wengi wafikapo vyuoni huwa na adabu na tabia njema, ikiwa ni pamoja na kuhudhuria vipindi, kusoma kwa bidii na pia kumkumbuka Muumba wao. Tatizo linaanza pale atakapo kutana na kuzoeana na watu wengi zaidi, hapo ndipo mambo huanza kubadilika.
Vifuatavyo ni vitu vinavyo wafanya wanachuo wengi kubadili tabia zao ;
1.Marafiki
2.Kuiga
3. Uhuru
4.Tamaa
1.Marafiki
kwa mfano mtu amepata rafiki mzuri mcha Mungu na mwenye bidii katika masomo yake, lazima atapata mafanikio makubwa sana ila akipata rafiki mbaya mwenye tabia mbaya kama ni wa kike amfundishe kujiuza na kila aina ya starehe, hapo lazima maisha ya huyo dada yatakuwa hatarini.
2.Kuiga
Wengi wafikapo chuoni, hutamani na kuanza kuiga maisha ya wengine jambo ambalo linasababisha mtu huyo kutokuwa na imani na kujiamini ndani yake kuanzia mavazi vyakula na kila kitu.
3.Uhuru
Kama tunavyojua chuoni hakuna mtu anaye kushurutisha kufanya jambo.Uhuru huu unafanya wengi wao kupotea na kujikuta wanabafili kabisa mienendo yao.
4.Tamaa
kutamani vitu wasivyokuwa na uwezo navyo, mfano; Iphone na vinginevyo, tamaa hii itampelekea mtu huyu kuchukua maamiz magumu yatakayo ibadili tabia yake kabisa.
MADHARA
Kutokana na marafiki,kuiga,uhuru na tamaa wengi wao hujikuta wanapata madhara makubwa kamavile kutumia madawa ya kulevya, kufeli masomo, kupata virusi vya UKIMWI na vingine vingi.
KIPI KIFANYIKE
Yawapasa wanachuo wote kuwa makini na ndoto zao, na pia kuwa makini wakati wa kuchagua marafiki, kutumia uhuru wao vizuri na pia kuacha tamaa mbaya.