Vitu vidogo tu lakini..

Jaguar

JF-Expert Member
Mar 6, 2011
3,438
1,025
Chungwa linauzwa sh.100 na Embe linauzwa sh.200.Nimenunua chungwa kwa sh.100.Mkononi mwangu nina chungwa lenye thamani ya sh.100,muuzaji nimemkabidhi sh.100 yangu.Nikimpa chungwa,atakuwa na sh.100 yangu niliyompa mwanzo pamoja na chungwa langu ambavyo thamani yake jumla ni sh.200.Je ninastahili kupewa embe lenye thamani ya sh.200?
 
Muuzaji ana sh.100 yangu na nimempa pia chungwa langu lenye thamani ya sh.100 jumla sh.200.

chungwa lako limeoza, thamani yake ni sh. 0/=.
Huwezi kupata embe, hebu jaribu kupiga mzinga kwa wanunuzi wanaokuja kununu bidhaa nyingine ili waku boost upate embe, ei kei bichwa lako
 
usivamie fani za watu. kawaulize wachaga watakufahamisha vzr
I know where the knot is,i'm the one who tied it and i know how to undo it,you just don't know how to argue and you better keep mum!
 
umempa 100 kakupa chungwa la 100 ukalimrudishia tena that means hujanunua kitu tena hapo so bado atakua na 100 yako na unastahili kitu cha 100 na si embe la 200....................................sorry kama cjakuelewa
 
exchange for commodity ilikua kipindi cha wakoloni.................hebu toa ankara
 
umempa 100 kakupa chungwa la 100 ukalimrudishia tena that means hujanunua kitu tena hapo so bado atakua na 100 yako na unastahili kitu cha 100 na si embe la 200....................................sorry kama cjakuelewa
Nashukuru umenielewa!
 
No hatoweza kukupa embe la sh200 7bu analo chungwa lako lenye thamani ya sh100 tu na sio 200
 
we niaje baada ya kuchukua chungwa ile mia sio yako tena...

'when the good are in unconditional sales in deliverable state property of goods in ownership passes to buyer when the contact is made'
 
Chungwa linauzwa sh.100 na Embe linauzwa sh.200.Nimenunua chungwa kwa sh.100.Mkononi mwangu nina chungwa lenye thamani ya sh.100,muuzaji nimemkabidhi sh.100 yangu.Nikimpa chungwa,atakuwa na sh.100 yangu niliyompa mwanzo pamoja na chungwa langu ambavyo thamani yake jumla ni sh.200.Je ninastahili kupewa embe lenye thamani ya sh.200?
Ni simple tu, umenunua chungwa lenye thamani ya Tshs 100, ukarirudisha kwa muuzaji inabidi muuzaji akurudishie hiyo Tshs 100 na ukitaka embe itabidi uongeze Tshs 100 na si vinginevyo. Ila siku nyingine usilete maswali mtori humu JF kama kuwauliza hivi mji mkuu wa Burundi ni upi? Halafu mwenyewe unajiona umetega.
 
Poa nisamehe mkuu,hamna shida bcoz database yangu ina mawe mengi tu,sema huwa ninahofu kuyaleta hapa bcoz thread itapata 0 replies.
 
Poa nisamehe mkuu,hamna shida bcoz database yangu ina mawe mengi tu,sema huwa ninahofu kuyaleta hapa bcoz thread itapata 0 replies.

yalete hayo nondo mkuu.ndo reply zitakuwa nyingi kuliko unavyodhani.
 
Rafiki yangu haustahili Chungwa...coz jamaa alipokuuzia chungwa aliweka na faida yake let us say huenda chungwa shambani kanunua kwa 50 so akakuuzia 100 ...ukimpa Chungwa na kumwachia 100 bado hatakubali coz shambani anapata chungwa hili hunda kwa 50 so utakuwa umenunua Embe kwa 150......
 
Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom