Beacon, mawe yanayopandwa ardhini kwa lengo la kuonesha mipaka ya eneo lililopimwa

Surveyor JA

Member
Jun 4, 2016
72
45
BEACON NI NINI?

Haya ni mawe yanayopandwa ardhini kwa lengo la kuonyesha mipaka ya eneo ambalo tayari limeshapimwa.
Kikawaida uwa yanapewa herufi na namba kwa mfano ZEY 215.

NINI INAPASWA UJUE PINDI UIONAPO BEACON
Si kila beacon inayopandwa ardhini imepandwa ikimaanisha eneo husika limepimwa.
Nyingine hazina hiyo maana

Hii utakutana nayo pindi unapotaka kununua ardhi.

NOTE;
HIVO BASI TUSHIRIKISHE WATAALAM KWENYE UNUNUZI WA ARDHI ILI UNUNUE ARDHI SALAMA..

Imeandaliwa na
Surveyor James Aloyce
https://m.facebook.com/goldlandcoltd/
1471864112736.jpg
 
OFA INAISHA MWEZI WA 8 HUU CHANGAMKIA

Hayo ni moja kati ya majibu tuliyoweza kuyapata kwa baadhi tu ya maeneo ambayo tumeweza kuyakagua baada ya OFA yetu..
Mstari MWEKUNDU ni eneo la mteja
Mstari BLUE ni ya mipango miji

Hivyo basi kama bado hujajua ardhi yako unayomiliki imepangiwa nini
Wasiliana moja kwa moja na Surveyor wako mpendwa

Surveyor James Aloyce Aweze kukusaidia
WhattsApp 0713778937
Call 0754619189
Call 0785779111

1471883351148.jpg
 
Mkuu ahsante kwa taarifa, ungeweka wazi mnafanya kazi kwa maeneo gani? Kama unavyojua Dar es Salaam sio maeneo yote yana ramani, hayapo kwenye mpango. Sasa hata kama mkipima mtalinganisha na ramani ipi kujua kama kiwanja kipo kwenye eneo sahihi? Sukrani.
 
Mkuu ahsante kwa taarifa, ungeweka wazi mnafanya kazi kwa maeneo gani? Kama unavyojua Dar es Salaam sio maeneo yote yana ramani, hayapo kwenye mpango. Sasa hata kama mkipima mtalinganisha na ramani ipi kujua kama kiwanja kipo kwenye eneo sahihi? Sukrani.
Eneo husika kama tayar limeshaandaliwa ramani ya mipango miji basi raman hiyo inaweza patikana na tukapata majibu ya hilo eneo kuwa limepangiwa matumiz gani..
Ahsante
 
TUJADILI KIDOGO HAPA, CHANGAMOTO GANI HADI LEO ZIMEKUFANYA UKAWA HUNA HATI YA ENEO LAKO?

1. Gharama kubwa za upimaji na umiliki ardhi?

2. Umekosa mda wa kufuatilia zoezi zima la upimaji na umiliki ardhi?

3. Hujawai ona/hujui umuhimu wa kupima na kumiliki ardhi?

4. Umekwamisha na wataalam katika zoezi zima la upimaji na umiliki ardhi?

5. Hujawai jua uanzie wapi ili uweze kupima na kumiliki ardhi?

By Surveyor Aloyce
Contact;
WhattsApp 0713778937
Call 0754619189

20190612_091805.jpeg
 
VITU NANE (8) MUHIMU VYA KUWA NAVYO ILI UWEZE KUPATA HATI MILIKI YA KIWANJA/SHAMBA LAKO

Surveyor Aloyce,

1. RAMANI YA UPIMAJI,
Eneo husika lazima liwe na ramani ya upimaji ambayo imeizinishwa na wizara ya ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi, iwe na mhuri na sahihi ya mkurugenzi wa ramani na upimaji.

2. RAMANI YA MIPANGO MIJI,
Eneo husika lazima liwe nar ramani ya mipango miji yenye kuonyesha matumizi husika ya eneo lako. Lazima iwe imeizinishwa na wizara na ina mhuri na sahihi ya mkurugenzi wa mipango miji.

3. MKATABA WA UMILIKI,
Lazima uwe na mkataba wa umiliki wa eneo lako, kama ulinununa, ulipewa zawadi, ulirithi n.k, Uwe na mhuri wa mwanasheria.

4. FOMU YA MIPAKA (SF 92),
Lazima uwe na fomu ya mipaka ambayo itaonyesha majirani unaopakana nao pande zote wakisaini kukubaliana na mipaka, itasainiwa pia na viongozi wa serikali yako ya mtaa.

5. FOMU YA MAOMBI YA HATI (SF. 19)
Fomu kwa ajili ya maombi ya hati, unajaza taarifa zako mfano jina, anuani, sahihi n.k

6. KITAMBULISHO CHA UTAIFA,
7. HATI YA UTAMBULISHO (AFFIDAVIT)
8. PICHA (PASSPORT SIZE)
NB; Muhtasari unahitajika kwenye baazi ya mikoa, pamoja na hati za mashamba

By Surveyor Aloyce
Contact;
WhattsApp, 0713778937
Call 0754619189
 
Back
Top Bottom