Vitu kumi (10) vya kuzingatia kwa usalama uwapo barabarani

Informer

JF-Expert Member
Jul 29, 2006
1,599
6,669
1. Kujifunza na kupata leseni inayostahili kwa kwa gari husika.

2. Kufunga mkanda wa usalama pamoja na abiria wako

3. Kuzingatia udereva kwa kujihami na mpanda pikipiki kuvaa kofia ngumu (hemet) na kutobeba abiria zaidi ya mmoja pia abiria kuvaa helmet.

4. Kuendesha kwa mwendo salama kwa kuzingatia hali ya barabara na alama za barabarani.

5. Kutoendesha ukiwa umetumia kilevi cha aina yeyote.

6. Kutotumia simu ya mkononi wakati unaendesha chombo cha moto.

7. Kuhakikisha unaonekana vizuri kila utumiapo barabara na kuendesha gari na sehemu salama nje ya barabara ambapo nitaweza kuonekana kwa urahisi kwa watumiaji wengine wa barabara.

8. Kujifunza na kufahamu kanuni zote za barabarani

9. Kuhakikisha unaendesha chombo chako kizima.

10. Kupunguza mwanga wa taa za chombo chako kila upishanapo au kuendesha nyuma ya chombo kingine.

Usiku mwema
 
Hakuna kitu cha muhimu kama kufanya kwanza ukaguzi wa gari au chombo chako cha moto ( pre start check), utakagua maji, oil zote (engine, hydraulic oil na black fluid), check tairi zako zote, hakikisha sign lights zote zilizo kwenye dashboard zinafanya kazi sawa sawa, washa chombo chako na ukiwach kingurume kwa dakiak kadhaa kabla ya kuanza kuendesha
 
safi sana wakuu. la muhimu pia tuwe makini na mafundi tunaowapa magari watufanyie service ikiwezekana nunua vifaa mwenyewe. Yeye kazi yake iwe kutengenza ukiwa unamfuatilia kwa karibu sana (usimpe upenyo) wengi wa mafundi wetu ni wezi wa pesa/vifaa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom