Vitu gani vya kuangalia hasa pale unapotaka kuoa (wadada watusaidie kwa hili)

Myahudi Jr II

JF-Expert Member
Jan 7, 2016
6,703
8,473
Ndugu zangu habarii za Jumamosiiii, naamini wikiend imekaa poa sana

Lengo la kuanzisha thread hii kusaidiana tu kimkakati hasa kwa wanaume amabo bado wanaamini katika ndoa, najua kuna wengine hawataki kusikia lolote kuhusu ndoa, Nimeleta mada hii humu ndani kwa kua naamini sana JF ni kisima cha mawazo na ukiyafanyia kazi kweli kweli utaapata mwanga wa jambo lako

kwanini? waswahili wanasema hivi "huwezi kutatua tatizo kwa akili iliyosababisha taizo, utahitaji akili mpya ili kutatua tatizo hilo" humu ndani akili mpya ni nyingi sana zenye mawazo chanya wakati wote japo kuna wengine za kwao wameamua kuvukia barabara tu.

niende kwenye mada sasa,

Unajua sisi wakaka/wanaume wakati mwingine huwa tunaogopa kuoa kwa kisingizio cha kujipanga kuwa badoo badooo badooo ila nia na malengo ya kuoa tunayo kabisaa tena ya dhati kabisa kutoka moyoni basi tu tunaogopa kwa kussema hatujajipanga.

Leo ninaomba Wadada/wanawake wa humu ndani mtuambie/mtupe ushauri kuwa mtu anapotaka kuoa "basic needs" anazotakiwa kuwa nazo ni zipi hasa katika maisha ya mwanzoni ya ndoa baada ya watu kula wali wakawaacha peke yenu.

Hapa naongelea kwa watu wenye vipato vya kawaida tu, mtu amemaliza shule akapata sehemu ya kujishikiza basi maisha yanaendele ila unakuta amefikia umri wa kuoa na anataka kuoa.

N.B nisamehewe kutokana na kutopangilia hoja zngu vizuri

FaizaFoxy Sky Eclat, ladyfurahia joanah Cajojo Miss Bantu Mis powers Miss Natafuta Hornet @
Super women 2 cariha Valentina aggyjay Heaven Sent Miss Curious

Najua JF ina wadada wengi sana kuwaita wote haiwezekani naamini mtainatana kusaidia hili
 
Ishi ki uhalisia wa hali yako, basic needs;
1. Regular source of income
2. A shelter
3. Chakula chenu wawili na u tayari wa kulea watoto.
4. Mavazi.
5. Uhakika wa huduma za afya.
6. Ukioa huku kwetu Uswazi kila shida ya ukweni jicho kitakua kwako.
 
Binafsi kabla ya ndoa naona ya msingi kuconsider ni kama
Kujua mapungufu ya mwenzi wako
Kujua family yake vizuri
Kuwa committed kwa kila mmoja
Uaminifu wake
Kupenda ndugu wa pande zote/asiwe mbinafsi
Uvumilivu na ajue kusamehe
Namna anavyokusupport katika issues zako
Msikivu/mwenye nidhamu....yapo mengi

Kuonjana (japo najua kuna wanaopinga hili ila kwangu mie ni muhimu sana)

Hapo ulipoandika katika maisha ya mwanzoni ya ndoa baada ya watu kula wali wakawaacha peke yenu watachangia wenye experience
 
Nimeona kauli moja hapo 'huwezi kutatua tatizo kwa kutumia akili iliosababisha tatizo'. Mbona kama ndio unachokifanya?
 
Binafsi kabla ya ndoa naona ya msingi kuconsider ni kama
Kujua mapungufu ya mwenzi wako
Kujua family yake vizuri
Kuwa committed kwa kila mmoja
Uaminifu wake
Kupenda ndugu wa pande zote/asiwe mbinafsi
Uvumilivu na ajue kusamehe
Namna anavyokusupport katika issues zako
Msikivu/mwenye nidhamu....yapo mengi

Kuonjana (japo najua kuna wanaopinga hili ila kwangu mie ni muhimu sana)

Hapo ulipoandika katika maisha ya mwanzoni ya ndoa baada ya watu kula wali wakawaacha peke yenu watachangia wenye experience

Nimekelewa vizuri mnnoo, ngoja tufanyie kazi haya
 

Similar Discussions

3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom