Vitu gani unazingatia, wewe binafsi kabla ya kuingia kwenye mahusiano?

Meshacky Allyson

Senior Member
Oct 29, 2020
124
246
Habari wana JF,

Natumaini mu wazima wa afya ni Dua na maombi yangu kwa mola ,azidi kuwalinda na kuwapa maarifa na hekima ili tuzidi kufundishana na kupeana mawazo, Narudi kwenye mada.

Binafsi nipo single na huwa nikikutana na marafiki au washkaji zangu, wengi huwa nikiwauliza why umeingia kwenye mahusiano na huyu binti ,majibu.

Ninayopata huwa nikiyatafakari ninaona hayana uzito kwa upande wangu ,mtu anasema tu cjui nipo lonely sana, mwingine mm nataka nipige na kusepa, mwingine ni mkumbo tu nae awe na demu, nikaja kugundua ndio maana mahusiano mengi hayadumu now dayz, kwa sababu mtu haelewi mahusiano ni ,nini..?

Na How , unayaendeshaje hayo mahusiano ,na kwa nini upo kwenye mahusiano, What, How, bWhy..?? Binafsi kitu cha kwanza ninachopenda kukitazama kabla sijaingia kwenye mahusiano ni UTAYARI WANGU..

How about you?

Nini unapenda kuzingatia kabla hujazama humo..

Uzi nawasilisha
 
Binafsi kitu cha kwanza ninachopenda kukitazama kabla sijaingia kwenye mahusiano ni UTAYARI WANGU..

How about you...??

Nini unapenda kuzingatia kabla hujazama humo..

Uzi nawasilisha
OP utayari wako unamaanisha nini?
Kwamba kuna wakati unakuwa hauingii kwenye mahusiano kwa sababu haupo tayari kuwa kwa relationship?
Hata kama ukimpata mtu sahihi kwasababu haupo tayari unaacha aende?

Kuhusu mimi, Nilizingatia haya, sisi ni marafiki na ninahisi kuwa comfortable around him. Tunashare baadhi ya hobbies hata kama sio zote lakini hata kama sio hobby yake ni yangu isiwe yeye inamchukiza (mfano kama napenda kuimba na sio hobby yake, basi ibaki kwamba sio hobby yake lakini sio jambo analolichukia). Hii itafanya ani-support au mimi nim-support na tuwe na maelewano mazuri.

Hivyo tu vinatosha.
 
Nilikuwa na mtu akinikuta naangalia tamthilia ananuuna eti anauliza sinaga vitu vingine vya kufanya. Mara kaniandalie hiki mara hiki hata kama havina ulazima muda huo, mara weka taarifa ya habari. Tuliachana ila hiyo haikuwa sababu.

Panchito wangu ndio kwaaaanza ananiambia nihadithie basi na yeye akiangalia mpira naangalia nae nakuwa timu pinzani. Sio unapata jitu linachukia kila unchopenda.
 
You dodged a bullet Hannah.
 
Hata huyo uliyonae kuna siku utamuita jitu
 
Nilikuwa na mtu akinikuta naangalia tamthilia ananuuna eti anauliza sinaga vitu vingine vya kufanya. Mara kaniandalie hiki mara hiki hata kama havina ulazima muda huo, mara weka taarifa ya habari. Tuliachana ila hiyo haikuwa sababu.
Panchito wangu ndio kwaaaanza ananiambia nihadithie basi na yeye akiangalia mpira naangalia nae nakuwa timu pinzani. Sio unapata jitu linachukia kila unchopenda.
Kitu ambacho najivunia katika maisha yangu ni kuwafanya vipenzi wangu wapende ninacho kipenda,hiki huwa namshukuru sana Mola muumba wa mbingu na ardhi na vyote vilivyomo.

Ajabu huwa wanakuja kupenda kwa hiari tena mpaka baadhi ya nyakati kunizidi mimi.
 
Hivi kuna tofauti kati ya mahusiano na kuoa?

Nisije kukosea katika kuchangia.
 
Nilikuwa na mtu akinikuta naangalia tamthilia ananuuna eti anauliza sinaga vitu vingine vya kufanya. Mara kaniandalie hiki mara hiki hata kama havina ulazima muda huo, mara weka taarifa ya habari. Tuliachana ila hiyo haikuwa sababu.
Panchito wangu ndio kwaaaanza ananiambia nihadithie basi na yeye akiangalia mpira naangalia nae nakuwa timu pinzani. Sio unapata jitu linachukia kila unchopenda.
Mywangu hebu nihadithie ile tamthilia ya Jana dear
Wewe hata ukiangalia matangazo ya vifo kwangu unatosha kabisa
Hannah
 
Kwa kifupi tuu kabla haujaingia ktk mahusiano inatakiwa wewe mwenyewe ujitathimini ni uhusiano wacaina Gani unahitaji kwa sasa

Kwa maana aina tano ya mahusiano
.ll
 
Aisee ishu ni uhai tu kuna mmoja kasema huku. Ukianza kutafuta mambo mnayopenda katika mahusiano mtajikuta mnaachana. Naona ni kila mtu kujielewa ana handle vipi hali ya mwenzie na anachezaje sehemu yake kama mwenza.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom