mitale na midimu
JF-Expert Member
- Aug 26, 2015
- 10,420
- 17,722
Draft ni mchezo ulioanzia India miaka ya 500AD.
1. Jinsi ya KUFIKIRI kwa Logic (Thinking Logically) na Kimkakati(Strategically)
Mwanzoni DRAFT ulibuniwa kama mchezo wa kijeshi ambao ulisaidia kunoa akili za wanajeshi katika kabla ya kupanga mikakati. Watu wengi wanaanza kufikiri kwa mikakati na kwa logic wakiwa watu wazima. Tofauti na michezo na games nyingi za watoto, Draft itawasaidia darasani na katika maisha yao ya kila siku.
2. UMUHIMU WA MASHINDANO
Maisha ya kila siku ni ushindani kuanzia darasani hadi kwenye biashara. Hapo hatujazungumzia siasa. Mzizi wa maisha na mafanikio ni kujaribu hadi ufanikiwe na ndilo somo atakalojifunza kwenye draft maana lazima ashindane ili ashinde.
3. ANAJIFUNZA NI WAKATI GANI AKUBALI KUSHINDWA NA KUJIFUNZA KUTOKANA NA MAKOSA
Drafti ni mchezo wa mbinu, mipango na mikakati na ni mchezo uliojaa uhalisia. Kila unapopoteza mchezo kwenye drafti unajifunza ulikosea wapi ili usikosee. Hii itamjenga mtoto awe makini na makosa na itamsaidia awe bora sana kwa baadae.
Kumbuka Drafti inapaswa ichukuliwe kama michezo tu wa kumfurahisha mwanao ingawa anafaidika kimyakimya.
Tukumbuke kiasi ni muhimu..
Karibu kwa maoni.
Appreciation:Lifehack