Vitu ambavyo huwavutia wanaume wamwonapo mwanamke zaidi ya muonekano...!


Mtambuzi

Mtambuzi

Platinum Member
Joined
Oct 29, 2008
Messages
8,809
Likes
1,336
Points
280
Mtambuzi

Mtambuzi

Platinum Member
Joined Oct 29, 2008
8,809 1,336 280


Mwanamke, je umeshawahi kushitukizwa mtoko (dating) na mwanaume wakati wala ulikuwa huna mpango wa kutoka siku hiyo? Lakini pia umeshawahi kujikuta ukiwa unamvutia kila mwanaume unayekutana naye pamoja na kwamba hujajikwatua na urembo (Make Ups) kama ufanyavyo siku zote?

Ngoja niwamegee siri, Kuna baadhi ya vitu wanaume huvi-notice haraka sana wamuanapo mwanamke zaidi ya muonekano wa wake wa kawaida. Vitu hivi vinaweza kufunika maeneo ambayo hayakufanyiwa utanashati kwa siku hiyo, kwa mfano mwanamke anaweza akawa hajatengeneza nywele zake kwa muda mrefu au hajatengeneza kucha zale kwa muda mrefu, lakini inatokea pamoja na udhaifu huo wanaume wakawa wanamkodolea macho kwa kuvutiwa naye mpaka hata yeye mwenyewe akashangaa.

Ukweli ni kwamba pale mwanamke anapotoka salon au anapotumia muda mwingi kujipamba akitoka anatarajia watu wamuone na waonyeshe kuvutiwa naye au hata kuambiwa tu na watu anaokutana nao kwamba amependeza, wengi hutarajia hivyo na ikitokea hakuna mwanaume anaye-notice kazi aliyoifanya ya kujiremba hujiuliza maswali mengi sana na anaweza kurudi kwenye kioo kujitazama upya ili kuona kama kuna mahali alipokosea.

Lakini pale ambapo hajajiremba yuko kawaida tu halafu ikatokea kila mwanaume anayekutana naye anaonesha kuvutiwa naye na hata kuombwa mtoko wa ghafla bila kutarajia, jambo hilo pia litamshangaza. Hapa chini nitaeleza sababu.1. Usafi: haijalishi kama nywele zako ziko vululu vululu au nguo uliyovaa sio nzuri sana na haifai kwa mtoko, usafi wa mwili kwa ujumla huleta mvuto wa pekee. Mwanamke kuwa msafi bila kuweka vikorombwezo vingine inatosha kumvutia mwanaume kiasi cha kuombwa mtoko.2. Jifunze na shiriki michezo mbalimbali: Unaweza kuwa mcheza mziki mzuri na mtu wa kujichanganya au unaweza kuwa mshabiki wa mpira wa miguu na unazijua ligi mbalimbali au unaweza kuwa mcheza pool au Dats mzuri, yaani jitahidi uwe mshiriki wa mchezo wowote utakaokukutanisha na watu mbalimbali na kushiriki mijadala inayohusiana na michezo, jambo hilo litakufanya uwavutie wanaume na kila mwanaume atamani kuwa karibu na wewe au utakuwa unapata mialiko ya mtoko kutoka kwa wanaume mbalimbali kwa sababu kuna kitu kinawavutia ukiwa nao karibu.3. Jiweke kisichana: Mavazi humbadilisha mtu kwa kiwango kikubwa, kuna baadhi ya mavazi huwaweka wanawake kuwa kama watu wazima na kuna mavazi huwapa muonekano wa kisichana. Kuna baadhi ya wanawake wana shida ya kuchagua nguo za kuvaa, yaani hawajui ni nguo gani huwapendeza wao wakiona mwanamke mwenzao kavaa nguo fulani na imempendeza na wao wanakimbilia kununua na kuvaa bila kujua kama umbo lake linaendana na nguo hiyo. Ni vyema wakati mwingie mwanamke akavaa nguo zinazomfanya aonekane msichana zaidi na hivyo kwa na mvuto wa kipekee. Lakini ni vyema zikiwa ni za heshima na zisiwe za kihuni zitakazokuvunjia heshima.4. Kujitegemea: Je wewe ni aina ya mwanamke ambaye unasubiri msichana wako wa kazi akusogezee kila kitu miguuni? Au wewe ni aina ya mwanamke unayependa kutuma tuma na sio kufanya mwenywe? Kwa kawaida wanaume hupenda wanawake wanaojitegemea, mwanamke ambaye hasubiri kila kitu afanyiwe.5. Kuwa na staha, subira na kuwavumilia wengine: Wanaume huwa wana-notice kama mwanamke hana staha wala subira na ha wezi kuwavumilia wengine. Mwanamke anaweza kuwa na mtoko na mwanaume lakini akifika kwenye mghahawa anakuwa hana staka anapoongea na wahudumu lugha yake inakuwa si ya kungwana na ni mwepesi kulaumu pale anapocheleweshewa huduma. Hakuna mwanaume anayeweza kuomba mtoko na mwanamke wa aina hii. Lakini mwanamke anapkuwa na staha, subira na wepesi wa kuwavumilia wengine anakuwa na mvuto wa kipekee kwani lugha atakayokuwa anatumia katika kuomba huduma itakuw ani ya kubembeleza na hata akichaleweshewa huduma haonyeshi kisirani sana sana atauliza kwa upole huku akitabasamu.6. Wepesi wa kusaidia:Kusaidia hapa haina maana ya vitu au fedha, bali kuwatia moyo wengine, au kutoa msaada wa mawazo, ushauri nasaha au kitu chochote kitakachomfanya mwingie ajisikie vizuri. Wanaume huwa wanaangalia eneo hilo kwa makini, kama mwanamke ni mtu wa kujipenda yeye zaidi yaani kila kitu anataka yeye awe wa kwanza na si mwepesi wa kusaidia wengine inapoteza mvuto hata kama awe mzuri kiasi gani au ajipambe kiasi gani. Mwanamke ambaye ni mwepesi kusaidia wengine na anayependa wengine wajisikie vizuri wanapokuwa karibu naye anakuwa na mvuto wa kipekee na kila mwanaume atavutiwa naye na kutaka kuwa naye karibu7. Tabasamu: Jambo hili nimelizungumza sana, hakuna kitu kinachomfanya mwanamke awe namvuto kama tabasamu. Mwanamke anaweza asiwe mzuri wa sura na umbo au anaweza asiwe na mavazi mazuri wala mapambo ya kuvutia, lakini tabasamu pekee linaweza kumpa nafasi ya kumvuto kwa kila mtu atakayekutana naye.
8. Shiriki mazungumzo: Kama unatafuta mwanaume wa maisha yako, basi shiriki mazungumzo, ni ajabu kwa baadhi ya wanawake wanaomba mtoko lakini wanapokuwa kwenye mtoko wanakuwa wakimya na hawashiriki mazungumzo, ni vyema kushiriki mazungumzo hata kama ni kupinga jambo fanya hivyo kwa hekima na kwa kujiamini, yaani kuwa wewe, usiwe mtu wa kuitikia tu kila mwanaume analosema, itakupotezea point. Wanaume wanapenda kuwa na mwanamke anayesimamia kile anachokiamini na anayeonekana kuwa na mwerevu.9. Manukato: Hili halina mjadala, manukato kwa mwanamke ni muhimu lakini yasiwe makali sana kiasi cha kuwakera wengine.10. Ukaribu na marafiki zako:
Hakuna mwanaume ambaye anaweza kuvutiwa na mwanamke asiyewathamini marafiki zake. Mwanamke ambaye utafuiki wake na marafiki zake ni ule wa maji kupwa maji kujaa. Mwanamke anaweza kuwa na marafiki wengi lakini si wote atakuwa na ukaribu nao lakini inaweza kutokea akawa na angalau rafiki mmoja atakayekuwa na ukaribu naye ambaye atakuw aakimshikikisha pale atakapohitaji ushauri kuhusu jambo fulani linalomtatiza.11. Kuwa mdadisi:
Wanawake wengi wanadhani kwamba wanaume ndio wenye jukumu la kuwashawishi ili wawapende, na hivyo hukaa kimya tu na kusubiri wanaume waanze kujiongelesha na kujipigia debe. Wasichojua ni kwamba hata wanaume wanapenda kuona wanawawake wakiwa na shauku ya kutaka kujua mambo fulani fulani kuhusu yanayohusu maisha yao, hivyo hutarajia kuona mwanamke akiwa mdadisi. Iwapo mwanamke atakuwa mdadisi na kuonyesha kuvutiwa na maelezo ya mwanaume, atakuwa ametengeneza mazingira ya kufanya mtoko uwe mzuri na usiyo chosha. Kuna baadhi ya wanawake wao hukaa kimya tu na kusikiliza kama mwanaume ataongea nini na hata kama mwanaume akiongea wao watakuw wanaitikia tu na hivyo kumfanya mwanume asijue kama anachozungumza kinamvutia mwanamke huyo au anamchopsha.....
12. Jipende mwenyewe:
hakuna binadamu mkamilifu na wanaume huwa hawatafuti mwanamke aliyekamilika, bali wanatafuna mwanamke atakayewakubali na anayejipenda mwenyewe kwani kama mtu akijipenda mwenyewe, ni dhahiri atawapenda wengine.

Mwanamke jipende mwenyewe..............
 
charminglady

charminglady

JF-Expert Member
Joined
Apr 16, 2012
Messages
18,160
Likes
1,613
Points
280
charminglady

charminglady

JF-Expert Member
Joined Apr 16, 2012
18,160 1,613 280
Mmmh.... Hapo kwenye namba 7 ni soo, make wengine tukitabasamu utadhani tunalia. Any way nitajitahidi hata kwa tabasamu feki!!!!
 
Eiyer

Eiyer

JF-Expert Member
Joined
Apr 17, 2011
Messages
28,267
Likes
4,172
Points
280
Eiyer

Eiyer

JF-Expert Member
Joined Apr 17, 2011
28,267 4,172 280
Mkuu kabla sijasema chochote hiki kifaa ni hatariiiiiiiiii!!!!!!!!!!!!

Ngoja nikaangalie vile Man Untd wanavyochezea kichapo tena leo kutoka kwa Newcastle
Nitarudi!
 
mapanga3

mapanga3

JF-Expert Member
Joined
May 1, 2012
Messages
665
Likes
567
Points
180
Age
39
mapanga3

mapanga3

JF-Expert Member
Joined May 1, 2012
665 567 180
mmmh, wewe nae hukosi la kusema, kila ukipita inakuwa kuichangia.
 
Fadhili Paulo

Fadhili Paulo

Verified Member
Joined
Sep 1, 2011
Messages
3,235
Likes
87
Points
135
Fadhili Paulo

Fadhili Paulo

Verified Member
Joined Sep 1, 2011
3,235 87 135
Mkuu kabla sijasema chochote hiki kifaa ni hatariiiiiiiiii!!!!!!!!!!!!

Ngoja nikaangalie vile Man Untd wanavyochezea kichapo tena leo kutoka kwa Newcastle
Nitarudi!
Danger! muombe mleta uzi namba zake za simu ila uwe makini maana ni hatariiiii.
 
sister

sister

JF-Expert Member
Joined
Nov 23, 2011
Messages
9,031
Likes
4,001
Points
280
sister

sister

JF-Expert Member
Joined Nov 23, 2011
9,031 4,001 280
Kweli kabisa...unaweza kuona hivyo vitu ni vya kawaida kumbe vinaongeza maksi...Asante Mtambuzi nimejifunza sana...
 
Last edited by a moderator:
Karucee

Karucee

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2012
Messages
13,779
Likes
10,203
Points
280
Karucee

Karucee

JF-Expert Member
Joined Mar 11, 2012
13,779 10,203 280
Hizo glass take Martini zimenivutia. # my throat is dry!
 
nyumba kubwa

nyumba kubwa

JF-Expert Member
Joined
Oct 8, 2010
Messages
10,313
Likes
1,832
Points
280
nyumba kubwa

nyumba kubwa

JF-Expert Member
Joined Oct 8, 2010
10,313 1,832 280
Hiyo heading unasema wamwonapo; lakini point nyingi si za muonekano; ni za watu wanaojuana vizuri; mfano kutokutegemea house girl akusogezee kila kitu, kushiriki michezo etc ; watu wanaovutiwa na wewe kwa kukuangalia barabarani (love at first sight)watajuaje yote hayo?

Ila nakubali kuwa smile ni uchawi mkubwa sana...smile smile smile; hata kama una matatizo lukuki smile; hata ukiwa peke yako smile...hii inapunguza hata aging
 
ladyfurahia

ladyfurahia

JF-Expert Member
Joined
May 10, 2011
Messages
13,909
Likes
1,409
Points
280
ladyfurahia

ladyfurahia

JF-Expert Member
Joined May 10, 2011
13,909 1,409 280
asante bestito kwa kutujuza mambo muhimu kwetu sis wanawake

ila paliponivutia zaidi ni hapa nimepapesti: Mwanamke jipende mwenyewe..............

ila mm sijajijua niko upande gani hapo? nitumikishe nijue
 
Munkari

Munkari

JF-Expert Member
Joined
Feb 9, 2013
Messages
8,102
Likes
564
Points
280
Munkari

Munkari

JF-Expert Member
Joined Feb 9, 2013
8,102 564 280
Mkuu kabla sijasema chochote hiki kifaa ni hatariiiiiiiiii!!!!!!!!!!!!

Ngoja nikaangalie vile Man Untd wanavyochezea kichapo tena leo kutoka kwa Newcastle
Nitarudi!
mh! Kumbe na wewe huwa unatamani!
 
K

kihedemuswede

Senior Member
Joined
Nov 25, 2013
Messages
140
Likes
15
Points
35
K

kihedemuswede

Senior Member
Joined Nov 25, 2013
140 15 35
Asante kwa mada naamini itawasaidia wengi
 
K

Kababi

Senior Member
Joined
Dec 24, 2010
Messages
168
Likes
1
Points
0
K

Kababi

Senior Member
Joined Dec 24, 2010
168 1 0
Nakuja namalizia mpira mara moja..

Sent from my BlackBerry 9810 using JamiiForums
 

Forum statistics

Threads 1,273,091
Members 490,268
Posts 30,471,036