Vitu 5 vya kuzingatia ukiwa unataka kufanya udahili wa chuo au Chuo Kikuu

Kilenzi Jr

Member
Jul 29, 2021
13
245
Ni jambo moja kuamua usomee nini, na ni jambo la pili kuamua ukasomee wapi.

Tanzania Kuna vyuo vikuu na vyuo vya kati zaidi ya 100

Lakini utalazimika kuchagua kimoja tu katika hivyo vingi ili uweze kusomea unachotaka kusomea.

Hivyo ni muhimu sana kuwa na sababu ya kwanini unachagua chuo fulani na si chuo kingine

Wapo wanaochagua chuo kwasababu mbalimbali zisizojitosheleza kiumuhimu, kama vile kwasababu marafiki zao wanasoma hapo, au kwasababu ndicho pekee wanachokijua, kwasababu wamelazimishwa kusoma hapo na walezi, wazazi, ndugu,nk. Na wengine wapo tayari tu kusoma kitu chochote katika chuo chochote ilimradi wapate chuo.

Mimi nashauri uchague chuo ukiwa na sababu ya msingi kwanini unachagua hapo na siyo chuo kingine.

Vifuatavyo ni baadhi ya vitu vya kuzingatia unapochagua chuo cha kwenda kusoma;-

1. Uwepo wa Taaluma unayoitaka kuisoma.

Kwa kuzingatia malengo yako , TAALUMA unayoitaka kusomea ndiyo itakayokuongoza, maana itakulazimu kuchagua chuo ambacho wanafundisha Taaluma unayoitaka.

Hivyo,jambo la kwanza baada ya kujua ni Taaluma gani unahitaji, Angalia ni vyuo gani vinaifundisha ili katika orodha hiyo uamue ni chuo kipi uchague.

(Kama TAALUMA unayotaka inapatikana katika vyuo zaidi ya kimoja, Nashauri uapply zaidi ya chuo kimoja ili kuwa na wigo mpana wa kuchaguliwa kwasababu ya ushindani unaoweza kuwepo).

2. Zingatia Vigezo vya udahili. (Entry qualifications)

Vipo vigezo vya jumla vya kuanzia (“minimum qualifications” kulingana na MWONGOZO wa TCU, ambapo ni kwanzia Cut off points ya 6 kwa TAALUMA za Afya na 4 kwa taaluma zisizo za Afya) ili uweze kudahiliwa chuo kikuu katika Taaluma Yoyote.

Lakini kila chuo kina vigezo vyake ili wakudahili katika Taaluma husika . Hivyo ni muhimu kuzingatia hilo kwa kulinganisha na matokeo yako.

Ni vyema kufahamu kuwa Vigezo vya kudahiliwa kusomea TAALUMA hiyo hiyo katika chuo fulani vinaweza kuwa tofauti katika chuo kingine.

3. Vigezo vya kifedha. ( Financial reasons)

ADA NA MALIPO MENGINE.
- Vyuo vinatofautiana Ada kulingana na Taaluma husika, (japo vipo vinavyofanana ada.)
Pia kuna malipo mengine kama vile malazi (hostels), nk.

GHARAMA ZA MAISHA UWAPO CHUONI
-Ukiwa chuoni utakula, utasafiri, utanunua vitu mbalimbali kwa matumizi binafsi, Makazi kwa watakaoishi off campus,nk. Gharama za maisha hutofautiana katika vyuo (ndani ya chuo na hata mazingira ambapo chuo kipo). Kuna mahala ambapo vitu bei ziko juu sana, Kuna mahala huduma nyingi hazipo hivyo utalazimika kuzitafuta mbali.

Haya yote ni ya kuzingatia pia unapoamua kuchagua Chuo gani ukasome.
Chagua chuo ambacho unaweza kumudu gharama za kifedha.

4. Mahala chuo kilipo (Geographical Location ).
-Ni muhimu pia kuzingatia Mahali chuo kilipo, kwa kuzingatia hali yako, Mahitaji yako, malengo yako na hata mazingira rafiki kwako kitaaluma na kuishi.

Maeneo yanatofautiana katika Hali ya hewa, upatikanaji wa huduma, umbali na kufikia, nk.
Kuliko kuishi mahali usipopapenda ni heri kuchagua mahali ambapo utaridhia kuishi kwa kipindi chote uwapo chuoni

graduates_43157-17.jpg

(PICHA KUTOKA MTANDAONI)


5. Zingatia mifumo na taratibu za kitaaluma katika chuo husika

Fuatilia kujua ratiba za chuo husika zipoje

(Kuna vyuo ambavyo vinashift ya ratiba kwa masomo ya day time na evening, kuna vyenye shift za semester kutofautiana kulingana na miaka ya masomo.,nk.

Fuatilia kujua Taratibu za kimasomo zipoje katika chuo husika, ikiwemo mifumo yao ya kupima wanafunzi katika mitihani, misimamo (standards) zao katika Taaluma.

Pia Mifumo na taratibu za chuo husika katika kusupport ubunifu na initiative za wanafunzi.

Fursa za kitaaluma na kijamii zilizopo katika chuo husika.

(Mfano kuna vyuo ambavyo mbali na kufundisha taaluma mbalimbali, lakini pia wana shughuli mbalimbali za kuendeleza wanafunzi wake kitaaluma. Kama vile kutoa motisha kwa wanaofanya vizuri kimasomo, kuwasafirisha nchi za nje ili kujiendeleza kitaaluma, nk)
 
jaman mm nikitaka kucomfirm saut arusha naambiwa kua tayar nimeshacomfirm chuo kingine ilihali sijafanya ivyo wala taarifa sijapewa za chuo nilixho ambiwa nimecomfirm Sasa nitajuaje icho chuo kilicho comfirmiwa?
 
jaman mm nikitaka kucomfirm saut arusha naambiwa kua tayar nimeshacomfirm chuo kingine ilihali sijafanya ivyo wala taarifa sijapewa za chuo nilixho ambiwa nimecomfirm Sasa nitajuaje icho chuo kilicho comfirmiwa?
Kwan umechaguliwa kipi na kipi?
 
jaman mm nikitaka kucomfirm saut arusha naambiwa kua tayar nimeshacomfirm chuo kingine ilihali sijafanya ivyo wala taarifa sijapewa za chuo nilixho ambiwa nimecomfir
Kwan umechaguliwa kipi na kipi?
Nimewapigia TCU wakanamby inaonekana nimecomfirm CUCOM kwaiyo niwapigie niwaambie waicancel confirmation yangu nashangaa nawapigia CUCOM wanasema haiwezekani sas cjui nafanyej
 
jaman mm nikitaka kucomfirm saut arusha naambiwa kua tayar nimeshacomfirm chuo kingine ilihali sijafanya ivyo wala taarifa sijapewa za chuo nilixho ambiwa nimecomfir

Nimewapigia TCU wakanamby inaonekana nimecomfirm CUCOM kwaiyo niwapigie niwaambie waicancel confirmation yangu nashangaa nawapigia CUCOM wanasema haiwezekani sas cjui nafanyej

CUCOM WENYEWE WANA UKATA WA WANAFUNZI,
HALAFU WEWE UME_CONFIRM KWA KUWAJARIBU-
HAPO LAZIMA WAKUNG'ANG'ANIE MKUU!!!

JIPANGE TU KWENDA KUPIGA DESA MBEYA MKUU.
 
Back
Top Bottom