VITISHO VYA MH. WAZIRI KWA KIRANJA WA IDARA_Naomba ushauri jinsi ya kujihami | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

VITISHO VYA MH. WAZIRI KWA KIRANJA WA IDARA_Naomba ushauri jinsi ya kujihami

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Visenti, Jun 7, 2011.

 1. Visenti

  Visenti JF-Expert Member

  #1
  Jun 7, 2011
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 1,031
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 133
  Kuna ofisa mmoja ni kiranja katika idara ya serikali, kwa nia nzuri na uzalendo ofisa huyo alimlima karipio kali kulingana na kanuni mmoja wa watumishi kwa utovu wa nidhamu, kumbe huyo jamaa ni ndugu wa mh. waziri wa wizara husika, akaenda kumweleza nduguye (mh. waziri), mh huyo akamtwangia simu kiranja papo kwa papo na kutoa vitisho vikali, siku mbili baadaye yule kijana akarudi ofisini kwa kiranja na kumkabidhi barua iliyosainiwa na mh.waziri ikimpa maelekezo kiranja ku-withdraw hilo karipio na kumsafisha kijana. kiranja akasalimu amri na kuwa mpoleee. sasa wana JF kinachofuata hapo ni uwezekano wa kiranja huyo kuchakachuliwa/kuwa victimized, je afanyeje ili kujihami kama atadhuriwa hapo baadaye? maana hawa waheshimiwa wana nguvu za kufanya lolote.
   
 2. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #2
  Jun 7, 2011
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 3,962
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 180
  Mkuu lolote unalolifanya ukiwa kazini, ulindwa na sheria kanuni na taratibu.
  Na ndio maana ukichukua hatua yoyote ni lazima taratibu hizo zifuatwe kikamilifu kwa kulinda heshima na ajira yako.
  Mimi kwa kweli siamini kuwa unaweza kumuadabisha mtu aliye chini yako na akaenda kwa waziri kukushitaki, halafu waziri akakuandikia wewe binafsi kukukaripia kwa kumtumia mtu yule yule uliyemuadabisha!
  Kiutaratibu hilo haliwezekani, labda kampuni ya binafsi.
  Kati yako wewe na waziri kuna wakurugenzi , makamishna na hatimaye katibu mkuu, ambao ndio waangalizi wa ofisi/wizara, na kuhakikisha kuwa mambo yanaendeshwa kisheria.
  Ukijiamini katika maamuzi yako, mradi si ya kiimla hata viongozi wenzio watakubaliana na wewe.
   
 3. Mzee wa Rula

  Mzee wa Rula JF-Expert Member

  #3
  Jun 7, 2011
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 8,177
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Kosa alilofanya huyo bosi wako ni ku widraw hilo karipio lake. Kama kweli huyo dogo alifanya kosa kilichokuwa kinatakiwa ni huyo waziri kumuelimishwa tu juu ya kosa aliliofanya mwanae! Je angekuwa amefanya kosa la jinai angetishia mahakimu?
  Bossi wako hatakiwi kujihami hiyo ni dalili ya uoga, yeye aendelee kufanya kazi labda kama alikuwa muonevu.
   
 4. Mimibaba

  Mimibaba JF-Expert Member

  #4
  Jun 7, 2011
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 4,566
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Kwanza nakupongeza kwa kuleta hii thread.

  Jibu au ushauri akomae na afanye kazi zake kama alivyopewa barua, keshakosea kunyea kwa huyo kijana kwa barua ya waziri. Si ajabu na yeye ukiranja anao siyo kwa sababu ya "competency".

  Nitakupa mfano wangu binafsi ambayo ni true story. Nilianza kazi 1972 serikalini nikiwa mchapa kazi kisawa sawa. Kwa sababu mfumo wa serikali ulikuwa imara, hadi 1980 nikawa nimepata promotion 4 kwa wastani wa promotion 1 kila miaka miwili.

  Nakukumbusha tu kuwa Chama Cha Magamba kilishika utamu (hatamu) na kuanza real corruption 1977 with the collapse of EAC na mikakati yao mingine. Kitu cha kwanza walichokifanya ni kuua utumishi wa serikali ili wabadirishe utendaji wa serikali kuwa wakisiasa. Kwa hiyo njama za wazi zilifanywa kuwaondoa au kuwanyanyasa watendaji wasio yumba. Kwa maana hiyo watu serikalini walipewa madaraka kwa ukereketwa wao kwa chama au kwa kujuana na si kwa taaluma. Kwa hiyo kwa baadhi yetu tulioheshimu taaluma zetu na utendaji wa majukumu yetu ukawa ndiyo mwisho wa kupata promotion na kupandishwa vyeo kwa sababu yakutotii matakwa ya kisiasa katika utendaji. Kwa mimi toka 1980 sikupandishwa cheo mpaka nikastahafu 2009.

  Matokeo ya kuzingatia taaluma yangu ni kama hivi.

  Kabla sijastahafu waliniruhusu nikafanye kazi za Ushauri nchi za nje ili niondoe "kivuli" na kuwapisha kwa staili ya utendaji wa kisiasa. Kwa sababu siku zote walikuwa na nia ya kuniondoe ila walikosa sababu kwa vile utendaji wangu ulikuwa A1 siku zote bila dosari. Pia walinitenga na kazi zao za kisiasa na mimi nikatumia muda huo kupiga kitabu hapo hapo kazini.

  Malipo ninayolipwa kwa mwezi kwa scale za kimataifa kwa sasa ni mshahara wangu wa miaka miwili kwa mshahara wa wakati nilipostahafu.

  Siombi hizo kazi za ushauri bali ni wao wenyewe serikalini wakiulizwa nani alifanya kazi fulani? Kwa ujinga wao wananitaja mimi na kuwapa hao wanaouliza contact zangu.

  Huo ni mfano tu. Lakini issue ni muhimu kuheshimu taaluma yako uifanyie kazi kwa mazingira yo yote ukiwa imara bila kuyumba wala kushawishiwa. Kwa sababu kazi nzuri inajiuza hata kwa wabaya wako wataikiri na kosa watakalo fanya ni kukutafutia soko kwa utendaji wako mzuri na makini.

  ONYO

  AWE MVUMILIVU ANAPOKABILIWA NA HIZO CHANGAMOTO. MIKABALA KAMA HIYO NI KWELI NA INAJULIKANA KUWA IPO NA SI YEYE PEKE YAKE ANAYEPATWA NA HAYO. AJUE SIKU NJEMA ZA MUNGU HAZIISHI, HALAFU KWA UTENDAJI WAKE MZURI HAPO ALIPO ATAKUWA ANATEKELEZA WAJIBU WAKE KWA NCHI YAKE. KUWA CASUALTY (MHANGA) INAWEKANA LAKINI SIYO MWISHO WA MAISHA
   
 5. Visenti

  Visenti JF-Expert Member

  #5
  Jun 8, 2011
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 1,031
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 133
  Wakuu Lole Gwakisa, Mzee wa Rula na Mimibaba nimewapata, ahsanteni sana.
   
Loading...