Vitisho vya Malawi: Ni upi msimamo wa Kambi ya Upinzani Tanzania? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Vitisho vya Malawi: Ni upi msimamo wa Kambi ya Upinzani Tanzania?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by wimbi la mbele, Aug 7, 2012.

 1. w

  wimbi la mbele JF-Expert Member

  #1
  Aug 7, 2012
  Joined: Jan 4, 2011
  Messages: 647
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Huo ndio ukweli

  haonekani

  hatujui wanamsimamo gani

  wala hatujui huyo waziri kivuli alichaguliwa kutokana na credentials zipi

  btw

  CHADEMA ndio chama mbadala wa CCM if not CCM B
   
 2. webondo

  webondo JF-Expert Member

  #2
  Aug 7, 2012
  Joined: Apr 29, 2012
  Messages: 1,724
  Likes Received: 110
  Trophy Points: 160
  Someni makala iliyoandikwa na Ndugu JAMES ZOTTO

  Sakata la mpaka kati ya tanzania na malawi: POLITICS VERSUS FACTS

  Ndugu zanagu, huenda mnafuatilia vizuri tatizo la mpaka wetu wa ziwa nyasa na malawi! Nilishtushwa sana na hotuba ya bwana waziri. mimi napenda utaifa wangu na uzalendo wangu. lakini napenda sana kutetea mambo yangu kwa kuukubali ukweli, kujua facts zaidi, kukubali hata zile zinazonipinga na ndipo najipanga kujenga joja.

  Eneo hili nafanyia study yangu ya PhD. Sidhani kama nipo sahihi zaidi na lengo langu si kusema nani anamiliki nini! Ukweli naoufahamu, tatizo si kubwa kivile kama tunavyolifikiri kama tutachukua muda kupitia documents zote na muhimu. Tunahitaji kwenda Public Records Office-Uingereza, Colonial Archives Potsdam, ujerumani, pia malawi national archives, tanzania national archives, libraries za UDSM na Chancellor college malawi. naamini ubishi utaisha kwa kuwa documents zote zipo.

  Angalizo: ziwa nyasa liligawanywa na mabeberu wa kiingereza, kijerumani na kireno. mkataba wa 1890 uitwao anglo-german agrrement unasema mpaka wa German east africa(tz bara ya leo) na nyasaland(malawi ya leo) unapita kandokando ya ziwa nyasa kutoka mto ruvuma mpaka mto songwe! huu ni mkataba wenyewe, upo ktk documents nyingi sana.....!!international law inajua hili na international lawyers wanaelewa nini nazungumza! Sehemu nyingine ilikuwa ni 1891 kati ya ujerumani na ureno, mpaka ulianzia mto ruvuma kuelekea Portuguese east africa(msumbijin ya leo) na pia ureno ikawekeana mpaka na british nyasaland(malawi)...kwahiyo, kipindi cha ujerumani, mpaaka unasomeka 'it passes along the shore of the lake(nyasa).....

  Mabadiliko ya mipaka: kipindi cha kikoloni, kabla ya mjerumani kuondoka, marekebisho ya mipaka yalifanyika kati ya mjerumani na mreno kwa kuspgeza mpaka mbele 0.5 KM from the original tripartite point, na vijisiwa vya mto ruvuma vikagawanywa. mpaka leo ipo hivyo. na eneo lingine ni kati ya mwingereza na mreno, ambapo, kisiwa kilichopo eneo la malawi linamilikiwa na msumbiji mpaka leo na eneo la ardhi lililopo msumbiji linakaliwa na malawi. mhuo ulikuwa mkataba wa marekebisho na ipo hivyo mpaka leo. kwahiyo, tulivyorithi mipaka, tumerithi na mabadiliko haya na hivyo hatuwezi kugombana na msumbiji wala msumbiji hawawezi kugombana na malawi. Mpaka wetu na malawi haukurekebishwa popote pale mpaka mjerumani anatoka...

  Marekebisho ya mipaka kipindi cha uingereza: sote tunajua german east africa, sisi pamoja na ruanda na urundi tuligawanywa katika sehemu mbili, ttukiwa chini ya League of nations tukiangaliwa na uingereza. Kunamabo nahitaji tuweke sawa. tukaitwa mandated territory na uingereza ni mandatory power. turudi ktk kamusi tutofautishe a an annexed colony and a mandate! Mpaka ukawekwa kati ya ubelgiji na uingereza, uliitwa the MILNER-ORTS AGREEMENT OF 1922! katika mkataba huu, mto kagera ulikatwa katikati na mpaka leo tumerithi hivyo. Hapakuwa popote pale ambapo eneo la ziwa nyasa lilirekebishwa kwa njia ya mkataba baina ya nyasaland state na tanganyika state...., isipokuwa, tofauti na mandates zote, tanganyika pekee, ilikuwa na tofauti ndogo, ambapo, mpaka wa ziwa nyasa ukapewa wanachoitwa 'wording', na hivyo, ramani ya tanganyika na official records zikaonyesha kuwa mpaka umepita katikati ya ziwa nyasa! na hapa ndipo tatizo linapoanza na sisi tumechukulia hii ndo absolute fact, hatuendi mbele kidogo. haya yapo pale national archives secreatarita files, ACCESSION NUMBERE AB 8 na AB 30! nafikiri hotuba yote ya bwana mkubwa jana imetoka ktk files hizi, ndizo walizopelekewa!!!

  twende mbele kidogo, ni kweli, kama mheshimiwa alivyosema jana, ramani nyingi kuanzia 1922 mpaka 1939 zinaonyesha mpaka upo katikati ya ziwa! je, ukweli huu utatutosha pekee mbeleni tukifikishana mbali? hapana!mheshimiwa hakusema kuwa ramani zingine, japo chache muda huu huu na official reports hazionyeshi mpaka au zinaonyesha mpaka upo chini. lakini ni chache! kwanini hili?bado natafuta majibu, lakini kwa harakaharaka, unaweza ukasema kuwa uingereza ilitamani tanganyika iwe koloni lake na si mandate! na pia ilishinikizwa na wawekezaji na hata jeshi ilisema afadhari waiteke ili liwe koloni na waachane na mandate! nahitaji tuelwe maana ya mandate.

  Hii yote ilitokea baada ya Donald Cameroon, governor wa tanganyika kusema kuwa tanganyika is a part of the british empire and it will remain so! hii ni siasa na si ukweli kama unaelewa maana ya kuwa wao hawakuwa wamepewa koloni kama mali yao, bali kuliangalia mapaka wananchi wapate 'akili' ili wapewe uhuru! kwa hiyo, kimsingi, kwa maana ya sheria ya kimataifa, tanganyika haikuwa part ya british empire kama yalivyo makoloni yaliyotekwa mojakwa moja na uingereza yenyewe! hapa pakatokea mvutano mkubwa sana katika house of Lords na house of commons! na hivyo basi, mtafaruku huu wa mpaka ulianzia hapa, kwa kauli hii na hivyo hata waingereza wenyewe walivutana kuhusu mpaka. ipo hivi, mwaka 1926, wajumbe wa mabaraza waliibana serikali iseme mipka ya tanganyika na ule wa ziwa nyasa! mabishano, kama haya yetu leo yalikuwa makubwa, ila si kwa kutishiana kwa kuwa walikuwa wenyewe na walitaka kuwekana sawa! ndipo secretary of state for colonies alibanwa na mjadala ulikuwa wa kisheria zaidi ukihoji status of the mandate, british empire, n.k; na kama waingereza wanamamlaka ya kujipangia kuhusu koloni waliolokabidhiwa kuliangalia(nieleweke na si kulimiliki)! mwishowe, mtu huyu mwenye dhamana alisema kwamba, hata yeye anashindwa kuelewa, 'what exactly is the sovereignty of tanganyika lying'! jamani mnamwelewa huyu mtu? kwamaana hiyo, haelwi vizuri mipaka yetu, ambayo wenyewe ndo wameirekebisha au kuipa 'wording'!! hivyo, tatizo linaanzia hapa na si muda mwingine wowot!!!

  Kipi hakusema bwana mkubwa jana: kuanzia 1939, mambo yalibadilika na hawa hawa watu tunaochukua ashahidi kutoka kwao, wakafanya madudu! na ilipoisha vita ya pili ya dunia, jamani oneni haya, hawa waingereza katika ramani zao, tena nyingi mno,(kaangalieni East africana section, university of dar es salaam, sehemu ya thesis, kuna cabins 3 zimejaa ramani na bado ni mpya sana kutokana na kutunzwa na pia kutotumka sana), kuimbezinaonyesha, bila shaka yoyote, kuwa mpaka wa tanganyika na nyasaland unapita pembeni mwa ziwa na si katikati! mkuu hakusema hili. aliishia 1939! kumbe hawa jamaa walichora tena ramani zote zikionyesha mpaka upo pembeni mwa ziwa!!!! kwanini hili?natafuta majibu, lakini nkwa haraka naweza nikaspeculate mawili. mosi, karibu na vita vya pili vya dunia, ilisikika tetesi kule duniani kuwa, ujerumani inarudi na inakuja kuchukua malokoni yake. (kasome national archives of tanzania, secreatariat files zote zenye kichwa cha habari, 'the future of tanganyika in british empire'). kwa hiyo, waingereza walihofia kutimuliwa na kurudi kwa wajerumani, na hivyo, wakarudisha ule mpaka wa awali wa 1890! na pia, muda huu, baada ya kwisha vita, tanganyika ikawa chini ya UNO ambapo ilipewa trusteeship status!maana ya hii ni rahisi kuliko mandate!ilimaanisha to be granted immediate independence! maana ya neno immediate hapa ni kwamba, kwa tafsiri yangu, waingereza wlifahamu wanatimka mapema mno kwani mkataba unasema hivyo....nafikiri, wakarudisha ramani zikionyesha mpaka upo pembeni...na kitabu ch Nyasaland cha mwaka 1958, kinaonyesha mipaka ya nyasaland na ziwa lote likiwa kwao! tukitaka kuwashinda wamalawi, lazima tukisome vizuri kipindi hiki na tuelewe facts zipi zinawapa kiburi na zipi sisi tuzitumie, la sivyo, tunaweza.............!!!!!!!!!!!!! kwahiyo future of tanganyika ilikuwa contested, uncertain, etc kipindi hiki, pamoja na mipaka yake pia!! tujiulize, kwa maana ya mandate, waingereza walikuwa na legal authority 'kurekebisha' mpaka wa ziwa nyasa? na je makosa waliyofanya waingereza, ndo legal backing yetu sisi? ebu tuzame tena tutafute facts tuwashinde hawa jamaa!

  Tulishindwana na uingereza kurekebisha mipaka. mwalimu alisubiri mpaka malawi iwe huru!akatoa miaka mitatu tu na asingetambua mipaka ya kikoloni(soma hansard, 1962). walipopata uhuru, kukawa na matatizo ambayo jana bwana mkubwa aliyaeleza. nampongeza ni dhahiri, 1964 cabinet crisis ya malawi na wale mawaziri kutorokea nchini kwetu kupitia ziwa, banda akaona ziwa ni infiltratio route! sera zetu za mambo ya nje zilikuwa tofauti. tulikuwa frontline state kwa ukombozi, wenzetu wakasapoti makaburu na wareno na wakawa na balozi sehemu hizo.....wakagombana na mwalimu, military show down miaka ya 1967-8; matusi na kejeli zikatawala kati ya mwalimu na banda, sisi na malawi.....kipara cha banda kinamagamba, tuliimba tukiwa jeshini, mwalimu akasema mpaka a sensible leader akitokea malawi ndipo tutajadili tena swala hili na si na kamuzu banda! tulikuwa kimy, na kuanzia 1975, hatukuwa na tatizo,lakini si kusema kuwa tulitatua tatizo la mpaka!

  Tulikaa kimya!mipaka haina tatizo isipokuwa ni time bomb ambapo ikitokea spark ni explosion! Tuliirithi kupitia Article III ya OAU CHARTER ya 1964 BAADA YA DEBATES KUBWA NA WENGI WAKARIDHIA TUIRITHI, uti possidetis, ita possidetis principle (so as you exist, so may you exist), kama kawaida yetu tulidesa ya kibeberu, Westphalia principle, border inviolabiliy! hatukupata muda mwingi wa kutafakari na kuangalia kila mpaka na matatizo yake....tulirithi na matatizo na yanatutatiza leo!!!

  Way forward! naikiri tuna namna tatu ya kulimaliza! moja ni kwa majadiliano ya kawaida yaani diplomacy kama bwanamkubwa alivosema jana. pili ni kupigana vita. (war is another means of diplomacy), mnataka kuniona kichaa!huo ndo ukweli, atakayeshindwa atasalimu kama ilivyokuwa kwa uganda na sis. tatu ni mahakama ya kimataifa yaani International Court of Justice! hapa ninawasiwasi. kama facts zenyewe ni zile za jana tu, sijui kama tutatoka.tutulie, tuite wataalamu wetu wajikite ndani sana. ni kweli kama alivyosema jana bwana mkubwa kwa kunukuu kesi nyingi na zilizoshinda, na kwa kusema kuwa, tukienda mahakama ile sisi ndo tutashinda!!!ninashaka....tumejipa favour ya verdict! kabla ya kesi.sijui.ninashaka kubwa!kunakushinda, kushindwa au suluhu!ninashaka tena na tena!

  mimi nimzalendo,nataka ukweli kwa njia ya mahojiano na kuumiza kichwa, tutetee mali zetu tukijua tunawashinda kwa hoja.....!!!!

  Wasiwasi: inasemekana kuna mafuta ziwani!!! kwahiyo mjue marekani na washirika wake hawako mbali! tujue operation ya military imperialism na huyu mama, mpwa wa kamuzu banda, anapata wapi hiki kiburi...nyuma yake kuna nini na nani!!1tuangalie haya pia.

  Hitimisho. tusiwe na hoja moj tu mkononi kama ndo water-tight evidence. tujaribu kuzibishanisha hoja zetu. na hoja nzuri ni zile zinazopingana nasi na tusizozipenda, tukizielewa na kuzikubali ndipo tutajipanga namna ya kuzigalagaza. tumwelewe vizuri adui yetu.....MUNGU IBARIKI TANZANIA!ZIWA NYASA!WANYASA!WATANZANIA!

  Tusing'ang'anie tu REPARIAN LAW!
   
 3. M

  Mundu JF-Expert Member

  #3
  Aug 7, 2012
  Joined: Sep 26, 2008
  Messages: 2,719
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Mwandishi wa makala amesomeka....
   
 4. Kasimba G

  Kasimba G JF-Expert Member

  #4
  Aug 7, 2012
  Joined: Jan 19, 2011
  Messages: 2,569
  Likes Received: 568
  Trophy Points: 280
  No! Sheria za kikiloni na za kimataifa ziko sawa? What happened to cameron vs nigeria and the likes? r we still colony?
   
 5. Kasimba G

  Kasimba G JF-Expert Member

  #5
  Aug 7, 2012
  Joined: Jan 19, 2011
  Messages: 2,569
  Likes Received: 568
  Trophy Points: 280
  something that we as learned people misses! The clear understanding and what was the main objective of partitioning afr!
   
 6. dudus

  dudus JF-Expert Member

  #6
  Aug 7, 2012
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 7,756
  Likes Received: 6,043
  Trophy Points: 280
  Sphere of influence! That was the fundamental motive.
   
 7. C

  Concrete JF-Expert Member

  #7
  Aug 7, 2012
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 3,607
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 0
  Jamaa amefafanua vizuri sana hapo juu, binafsi ninamuunga mkono.

  Mimi ni mtanzania ninayeamini kwenye haki na ukweli, ukweli ni kwamba ziwa Nyasa lote ni mali ya Malawi na hiyo ni haki ya wamalawi.

  Tamaa na wivu tulionao watanzania vitatuponza katika hili.
   
 8. Az 89

  Az 89 JF-Expert Member

  #8
  Aug 7, 2012
  Joined: Nov 20, 2011
  Messages: 1,613
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  Bora wachukue tu hilo maana hata tukibaki nalo ni faida ya ridhmoko na washirika wake!
   
 9. Adharusi

  Adharusi JF-Expert Member

  #9
  Aug 7, 2012
  Joined: Jan 22, 2012
  Messages: 10,630
  Likes Received: 3,014
  Trophy Points: 280
  Nimemuelewa Jems Zoko...ila bora wachukue tu,kuliko kubakia tanzania linufaishe mafisad
   
 10. D

  Don Draper Senior Member

  #10
  Aug 8, 2012
  Joined: May 30, 2012
  Messages: 176
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mie hata simjui ni nani huyo waziri kivuli wa ulinzi wa CHADEMA

  its about time akajitokeza
   
 11. Ben Saanane

  Ben Saanane Verified User

  #11
  Aug 8, 2012
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 14,603
  Likes Received: 3,692
  Trophy Points: 280
  Kambi ya upinzani ilitakiwa iwe imeshatoa Tamko hadi leo bila kuacha kuilaumu serikali ya CCM kwa kutomaliza hilo Tatizo kwa kipindikirefu kilichopita
   
 12. r

  rodrick alexander JF-Expert Member

  #12
  Aug 8, 2012
  Joined: Feb 12, 2012
  Messages: 4,100
  Likes Received: 1,491
  Trophy Points: 280
  hakitoko kitu nyie mnajiita watanzania kumbe wamalawi ngoja ianze vita mtajutia kushabikia vitu msivyovijua hao waingereza mbona mpaka leo wanang;ang;ania visiwa vya Folkland na pia hao hao waliokuwa wanang'ang'ania Hongkong kwa kifupi hawaaminiki na ni matapeli solution ni mbili majadiliano ikishindikana vita kwani huwezi kumpelekea kesi ya ngedele nyani
   
 13. Goldman

  Goldman JF-Expert Member

  #13
  Aug 8, 2012
  Joined: Dec 10, 2010
  Messages: 1,260
  Likes Received: 847
  Trophy Points: 280
  Come rain come shine, we need another military showdown.
   
 14. m

  manucho JF-Expert Member

  #14
  Aug 8, 2012
  Joined: Apr 20, 2012
  Messages: 3,410
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Malawi wachukue ziwa lao na kama wakija kwa vita mimi wa kwanza kuwaonyesha wapite wapi ili watutandike vizuri.

  Nasema hivyo kwa sababu kama kuna mafuta hapo lake Nyasa, tanzania ikichimba nani atafaidika nayo zaidi ya viongozi wachumia tumbo wa serikali ya Chama tawala?

  Dhahabu pale Shinyanga yote wanavuna tu wazungu ila mwananchi wa mwadui Shinyanga ni masikini wa kutupwa.
  Mererani Mkoa wa Manyara madini ya tanzanite yanavunwa kwa kuvunwa na kaburu MATATA anayenufaika ni kaburu na wachache tunaosikia kina Riz1 n' family mwananchi wa pale ni masikini huduma za jamii ni duni.
  Mtwara gas imepatikana hali ya pale ni duni manyang'au yanafaidika huko Dar es salaam.

  Uzalendo utoke wapi kwangu leo hii? Uzalendo umekwisha na aliyeniondolea uzalendo ni mtanzania mwenzangu. Adui akija namuonyesha njia ya kupita mpaka chumbani.

  Wananchi wanagunduaga madini wenyewe huko Singida, Tanga, Mtwara, Kilimanjaro, Dodoma nk then anakuja kiongozi wa serikali anakuja anatoa amri wananchi waondoke eneo hili ni la mwekezaji kumbe ni huyo kiongozi kaja kwa mlango wa nyuma. Ukijiuliza muda wote serikali ilikuwa wapi haijui kama kuna madini.

  Uzalendo utoke wapi? Na hapa lazima wazungu wako nyuma ya Mama kutokana na upumbuvu, ujinga wa viongozi ndani ya serikali hii dhaifu na mbovu.

  Tumeshindwa kuendeleza na kusimamia rasilimali tulizopewa bure na mwenyezi mungu, viongozi wamekuwa walafi hawaijali nchi wanajijalh wao na familia yao kwanini asije kuchukua anayeweza kuziendeleza?

  Mzungu yuko pale na anamwambia Mama anzisha, wacha wachukue coz mkichukua nyie watz watafaidika watu wawili au watatu na sio nchi.
   
Loading...