"VITISHO VYA JK NA SIMBA WA KUCHORA" - Admin Please Merge ***Rais Kikwete atoa Waraka | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

"VITISHO VYA JK NA SIMBA WA KUCHORA" - Admin Please Merge ***Rais Kikwete atoa Waraka

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by S. S. Phares, Jan 23, 2008.

 1. S

  S. S. Phares JF-Expert Member

  #1
  Jan 23, 2008
  Joined: Nov 27, 2006
  Messages: 2,141
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Rais Kikwete atoa waraka wa mwisho kwa majamabazi

  * Atangaza operesheni mpya, aonya serikali isije ikalaumiwa

  Na Midraj Ibrahim, Muleba

  Rais Jakaya Kikwete ametangaza rasmi kuanza upya operesheni ya kusaka majambazi nchini mwezi ujao.

  Aliwataka majambazi kujisalimisha na wananchi wanaowaficha kutoa taarifa kwenye vyombo vya ulinzi na usalama kabla ya operesheni kuanza.

  Akihutubia mkutano wa hadhara mjini Muleba jana, rais Kikwete alisema operesheni mpya haitajali mtu na hakutakuwa na huruma.

  "Napenda kuwaarifu mwezi ujao tutaanza operesheni kubwa nchini ya kusaka majambazi," alisema Rais Kikwete na kuongeza akiseama : "mtalaumu sana, lakini mtajilaumu wenyewe kwa kuwa ujambazi unafanya binamu, mtoto wa mjomba, lakini mnawaficha, watoeni kabla operesheni hiyo haijaanza."

  Rais Kikwete alisema tangu serikali yake iingie madarakani, hakuna jambo gumu lililowashinda na kwamba sasa watachukua hatua zinazotahili lakini serikali isije ikaluamiwa.

  Alisema hivi sasa vumbi la majambazi limetulia, wakibuni mbinu mpya na kwamba, kabla hawajaibuka watateketezwa na salama yao ni kujisalimisha.

  Akzungumzaia kuchelewa kukamila ujenzi wa wa barabara ya Kagoma-Lusahunga alisema watambana mkandarasi ili akamilishe kulingana na mkataba.

  Alisema suala la ulinzi na usalama halina mjadala ni jukumu la serikali na aliwaahidi wananchi kuwa majambazi hawataachwa watambe.

  Awali akizungumza kwenye mkutano huo, Mbunge wa Muleba Kusini, Wilson Masilingi, alimsifu Rais Kikwete kwa ujasiri wake wa kupambana na mafisadi wakubwa.

  "Umeonyesha mfano, umeanza na mafisadi wakubwa wewe endelea, sisi tutawashughulikia hawa wa chini ili tukutane katikati, wewe endelea kaza uzi!" alisema Masilingi.

  Masilingi alisema hawatakubali fedha za umma kufujwa na wachache na kuongeza kuwa watapambana nao, wakishindwa wataomba msaada ngazi za juu.

  Akiwa wilaya ya Chato juzi, Rais Kikwete aliwashukuru wananchi kwa kumchagua John Magufuli ambaye alisema ni msaidizi wake muhimu kutokana na utendaji wake mzuri.
   
 2. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #2
  Jan 23, 2008
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Duh!!! Huyu Mzee ndugu Rais namna gani ? Yaani alikubali maneno ya Masilingi na sifa zake ?
   
 3. D

  Dotori JF-Expert Member

  #3
  Jan 23, 2008
  Joined: Nov 3, 2007
  Messages: 547
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Muungwana hupimwa kwa vitendo
   
 4. Mwanamalundi

  Mwanamalundi JF-Expert Member

  #4
  Jan 23, 2008
  Joined: Aug 30, 2007
  Messages: 3,034
  Likes Received: 396
  Trophy Points: 180
  Kwa hivi hapa mheshimiwa raisi anawapa green light majambazi waendelee kutesa hadi mwezi ujao. Yaani wananchi waendelee kushuhudia majambazi wanatanua hadi mwezi ujao??? what is wrong dealing with majambazi right now??? Does the police force needs seminar at ngurudoto to deal with this issue???what is so special in february???
   
 5. S

  S. S. Phares JF-Expert Member

  #5
  Jan 23, 2008
  Joined: Nov 27, 2006
  Messages: 2,141
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Admin please merge na ile ya Mzee Mwanakijiji aliyoitoa hapa siku za nyuma kuwa JK na MIKWARA YAKE ni sawa na SIMBA WA KUCHORA asiyetisha hata sungura...

  Mwisho wa Mwaka tuangalie ni mikwara mingapi alifanya kweli na mingapi alitoa porojo.
   
 6. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #6
  Jan 23, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,361
  Likes Received: 6,384
  Trophy Points: 280
  mama weeeeeeeeee!!! nadhani wakati umefika wa kupigia saluti tai na kuachana na twiga..!!
   
 7. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #7
  Jan 23, 2008
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Katoa muda kwa kuwa wachangiaji mapesa ndani ya CCM ndiyo akina Nyali mshikaji wake na JK ambao ni majambazi so anataka kuwapa nafasi warudi wakatulie ili wakamatwe ambao siyo ama hata wapinzani wa CCM then waitwe ni majambazi .
   
 8. Mwanamalundi

  Mwanamalundi JF-Expert Member

  #8
  Jan 23, 2008
  Joined: Aug 30, 2007
  Messages: 3,034
  Likes Received: 396
  Trophy Points: 180
  Bwana weee mwanakijiji we acha tu. Yaani unamtangazia adui yako kwamba ebwanaeeee sasa jiandaee!!!Nakuja!! Huyu JK nadhani hata zile kozi za kivita alizofundiswa kule monduli hakuzielewa vizuri kama si kwamba ameshazisahau!!
   
 9. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #9
  Jan 23, 2008
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Alipewa majina na vyeo vya Kijeshi Kichama lakini hana mbinu wala kozi za kijeshi Momnduli alikuwa anakazana na siasa tu .
   
 10. Madela Wa- Madilu

  Madela Wa- Madilu JF-Expert Member

  #10
  Jan 23, 2008
  Joined: Mar 24, 2007
  Messages: 3,074
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 135
  Hizi ni njama za kudhoofisha ujambazi ufanywao na SISIEMU.

  SISIEMU wakiiba fedha za umma(BOT) ili washinde uchaguzi wanaua malaki kwa mkupuo:
  Tangu lini Chama kilichoshinda kwa kutumia Fedha ya wizi kikawajibika kwa wananchi?

  Uliwahi ona wapi ibilisi mmoja anachukua ufagio kumfagia ibilisi mwingine?

  Kwanza majambazi wengi wa kutumia Bunduki ni Polisi na wanajeshi ambao wanalinda wizi wenu wa mabilioni na wao kuendelea kuishi kwenye nyumba za FullSuit ya mabati huku ninyi mkiendelea kutanua kuliko hata Wafalme wenyewe.

  Kwanini asitangaze tarehe ambayo yeye binafsi atajifikisha kizimbani pamoja na wezi wenzie ili tujue kwamba ana uchungu na nchi?

  Mimi nilidhani huyu ni Rais Kijana angekuwa na uchungu na wenzake na kujenga uchumi kumbe ni nduli!
   
Loading...