Viti Maalum vya Ubunge vyaigawa CHADEMA. Washindwa fikia muafaka kususia Bunge

Deo Meck Mbagi

JF-Expert Member
Apr 19, 2015
360
525
Kutokana na kura za ubunge walizopata CHADEMA wanaweza kupata wabunge wa Viti Maalum kati ya 12 na 18.

Sasa wazo la wao kususia bunge na mabaraza ya madiwani limekuwa gumu kwa sababu kuna wanawake wanaoamini bora kutumia fursa hiyo kuliko kuiachia iende bure.

Katika kikao chao, Halima Mdee na Esther Bulaya wameweka msimamo kuwa bora waende bungeni walau kupooza machungu ya kushindwa bungeni.

Wakati huohuo vita ya ninani na nani watateuliwa kuwa wabunge wa viti maalum kupitia CHADEMA inaendelea huku wanawake wanaofukuzia nafasi hizo wamezidi kujiweka karibu na viongozi wanaofanya maamuzi ndani ya chama.

Wacha tusubiri hii movie itaishia wapi.
 
Nawashauri wasisusie, bunge ni sehemu ya kupeleka ajenda za chama. Nashauri hizo nafasi wapewe viongozi/watu machachari ambao kimsingi kila mtu anawajua. Huwezi kuwaacha Halima Mdee, Bulaya, Matiko, Makamba na wengine wapya ambao ni moto kama yule binti aliyemshinda ubunge MwanaFA ila akaibiwa kura.
 
nawashauri wasisusie,bunge ni sehemu ya kupeleka ajenda za chama. Nashauri hizo nafasi wapewe viongozi/watu machachari ambao kimsingi kila mtu anawajua. Huwezi kuwaacha Halima Mdee, Bulaya, Matiko, Makamba na wengine wapya ambao ni moto kama yule binti aliyemshinda ubunge MwanaFA ila akaibiwa kura
Hahaha Huyoooo
Naona leo Umekuwa mpoleee
Zile Mbwembwe Kwishaaaa
Wewe Shabikia Simba tu
Hilo lichama ni Zero
 
nawashauri wasisusie,bunge ni sehemu ya kupeleka ajenda za chama. Nashauri hizo nafasi wapewe viongozi/watu machachari ambao kimsingi kila mtu anawajua. Huwezi kuwaacha Halima Mdee, Bulaya, Matiko, Makamba na wengine wapya ambao ni moto kama yule binti aliyemshinda ubunge MwanaFA ila akaibiwa kura
Sasa majina ya wabunge wa viti maalumu si tayari yalishapelekwa NEC, hao machachari wakiwa hawamo.
 
nawashauri wasisusie,bunge ni sehemu ya kupeleka ajenda za chama. Nashauri hizo nafasi wapewe viongozi/watu machachari ambao kimsingi kila mtu anawajua. Huwezi kuwaacha Halima Mdee, Bulaya, Matiko, Makamba na wengine wapya ambao ni moto kama yule binti aliyemshinda ubunge MwanaFA ila akaibiwa kura
Mmeshapoa sasa mnawaza mapanki ni bora muyale tu?
Vipi kuhisu bosi wenu Lissu mnaanza kumsahau kiaina, vipi misheni zake mara maandamano au mme mpuuza?
 
Kama wako serious, hakuna kushiriki ubatili. Chama kipitishe azimio marufuku kushiriki kwenye udiwani wala ubunge. Atakayekaidi, fukuza chama aende CCM akapate ubunge au udiwani. Viti maalumu inatumwa na Chama, simuoni Mnyika, Mbowe na Lissu wakituma hayo majina. Over
 
Kutokana na kura za ubunge walizopata Chadema wanaweza kupata wabunge wa viti maalum kati ya 12 na 18...
Huu ni ujinga au ni nini?

Hivi unajua mchakato wa viti maalumu ulivyo??

Huko Lumumba inamaana mlichaguana wajinga tupu au?
 
nawashauri wasisusie,bunge ni sehemu ya kupeleka ajenda za chama. Nashauri hizo nafasi wapewe viongozi/watu machachari ambao kimsingi kila mtu anawajua. Huwezi kuwaacha Halima Mdee, Bulaya, Matiko, Makamba na wengine wapya ambao ni moto kama yule binti aliyemshinda ubunge MwanaFA ila akaibiwa kura
Si wako jela hawa jamaa? Wamejadili saa ngapi?
 
nawashauri wasisusie,bunge ni sehemu ya kupeleka ajenda za chama. Nashauri hizo nafasi wapewe viongozi/watu machachari ambao kimsingi kila mtu anawajua. Huwezi kuwaacha Halima Mdee, Bulaya, Matiko, Makamba na wengine wapya ambao ni moto kama yule binti aliyemshinda ubunge MwanaFA ila akaibiwa kura
Kama viti vitakuwa 15 I suggest kila kanda itoe watu wawili wawili na moja ni Mwenyekiti Bawacha Taifa.

Mtihani utakuwa kanda ya serengeti na Victoria
Kanda ya serengeti.
1 Esther Matiko
2. Esther Bulaya
3.Catherine Ruge.
4. Salome Makamba.
5. Gimbi Massaba.

Victoria.
1 Anatropia Theonest
2. Conchester Rwamlaza
3.Pendo Peneza
4.Husna Said
5. Victoria kule Sengerema. hapa mtihani utakuwa mkubwa sana nani apate nani akose.
 
Kutokana na kura za ubunge walizopata Chadema wanaweza kupata wabunge wa viti maalum kati ya 12 na 18...
Kikao cha kususia Bunge kilipofanyika hakukuwa na mwanamke hata mmoja. Kwahiyo huu ni mfumo dume unaodharau nafasi ya wanawake kujiamulia mambo yao wenyewe.

Haikuwa Sahihi kutangaza uamuzi bila kuwashirikisha kinamama wenyewe.
 
waende tu ili wahalalishe uchaguzi ulikuwa huru na wahaki,pia itasaidia kupunguza kelele za mabeberu.
 
Kama viti vitakuwa 15 I suggest kila kanda itoe watu wawili wawili na moja ni Mwenyekiti Bawacha Taifa.

Mtihani utakuwa kanda ya serengeti na Victoria
Kanda ya serengeti.
1 Esther Matiko
2. Esther Bulaya
3.Catherine Ruge.
4. Salome Makamba.
5. Gimbi Massaba.

Victoria.
1 Anatropia Theonest
2. Conchester Rwamlaza
3.Pendo Peneza
4.Husna Said
5. Victoria kule Sengerema. hapa mtihani utakuwa mkubwa sana nani apate nani akose.
Itategemea nani anacheka vizuri na Mwenyekiti
 
waende tu ili wahalalishe uchaguzi ulikuwa huru na wahaki,pia itasaidia kupunguza kelele za mabeberu.
 
Hata hujasema chanzo cha habari yako, umekuja kuripoti hisia zako hapa, kawadanganye wajinga wenzio.
 
Back
Top Bottom