USHAURI: Tubadili mfumo wa viti maalum, vifutwe!

Akili Unazo!

JF-Expert Member
Feb 18, 2009
3,930
4,892
MASWALI NA HOJA ZA WADAU KUHUSU SUALA LA VITI MAALUMU TANZANIA
Wakuu leo katika kupitia maandishi ya gazeti la mwananchi nimekutana na kichwa cha habari kisemacho Wabunge wa viti maalum ni feki kikatiba hivyo waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu (sera utaratibu wa bunge) Philip Marmo alisema utaratibu uemkua ukitolewa na CCM kama zawadi kwa wanawake hivyo anasema kama kuna uhitaji wa kuendeleza kutoa zawadi hizo bas litolewe pendekezo la kuingiza katika katiba.

Swali ni kwamba kwa miaka yote hii ya uhuru arobani na tano ni kweli kuna mambo serikali yetu inafanya ambayo hayapo kikatiba?

Wakuu nielimisheni maana yake mimi nilishakufa siku nyingi ndo maana nataka urithi wangu wanipe niache kuona kinachoendelea.
---
Katika kitu ambacho kinaniumiza ni viti maalumu tuna zaidi ya wabunge 100 ambao hawana majimbo wako bungeni wakipitisha sheria ambazo hazina maslai kwa taifa nyingine za kukandamiza.

Ndoto yangu siku hivi vitu maalumu vikifutwa kabisa sijui viwe vya CHADEMA, CCM, CU wote hakuna kitu samahani kama nitagusa maslahi ya watu sioni tija ya viti maalumu na sitakaa nione kama mfumo wa viti maalumu watu wanachaguliwa kutoka kwenye vyama vyao na kupelekwa bungeni.

Viti maalumu vya sasa vinakibeba CCM kwa sababu kinaingiza wabunge wengi ndani ya bunge hii ina maana wabunge wengi wa viti maalumu watatoka hiko chama cha CCM. Tatizo linakuja wakati wa kupitisha mambo yenye maslai mazuri ya nchi wengi wanaweka ushabiki huhitaji kuvaa miwani kujua kuwa wanatumika.

Viti maalumu vingi vimekuwa kandamizi sana wakina mama/dada wanadiliki kujitoa kwa vigogo wa chama ili wapate upendeleo fulani kuingia bungeni hii ni aibu kubwa sana wengi wanatoa hadi miili ile wapewe viti maalumu.

Viti maalumu vimekua vya upendeleo wa tabaka fulani kwamba ndo wanaweza kuingia bungeni huhitaji kuwa na Phd kujua hili kote CHADEMA, CCM kuna matatizo na wengi walilalamika mchakato wa kupata viti maalumu.

Je, tukifuta viti maalumu nini cha kufanya kuleta usawa bungeni.

Uundwe mfumo kila mkoa kuwe na majimbo maalumu ya wanawake
Hapa tutajenga uwanja mpana sana kwenye demokrasia hawa kina mama wagombee kwenye majimbo maalumu yatakayo tengwa kwa ajili yao ukifanya hivi kuna uhakika wa asilimia kubwa ccm ikapoteza viti vingi sana maana wabunge wengi wameingia kwa kubebwa.

Kuna wazo pia nilipewa sehemu mfano jimbo la ubungo mbunge si mnyika kungekua na mbunge wa pili ambaye angepigiwa kura jinsia yake iwe ya kike. Hili wazo bado sijaliafiki maana naona kutakua na uingiliaji wa utendaji.

Tuondokane na hili suala la viti maalumu tuunde mfumo mpya ambao wanawake watapambanishwa kumpata mshindi mmoja na kupigiwa kura.

Viti maalumu ni janga si kwa CCM bali kwa taifa kwa ujumla.

Fred kavishe
---
Wanajamvi,

Nimejaribu sana kuangalia na kutafakari sana mfumo wetu wa viti maalum... sijachukua reference ya nchi yoyote kwani sioni sababu na hasa ukizingatia kwamba our country is unique, blessed na inapitia kipindi kigumu cha mpito kwa kuondokana na dhana zama kwenda dhana halisia...

Ukiangalia hata mchakato unaotumika, kwangu mimi naona unanyima nafasi baadhi ya makundi hasa walio weledi kupita, kuchakachuliwa hadi kupata nafasi... teh current system [regardless of chama] imekua ni ya kupigia kura watu kutokana na popularity katika vyama rather than qualities.... si chadema, KAFU wala CCM walio na chakato wa kuridhisha kupata hawa watu... here are my proposals

  1. tupunguze idadi ya wagomea wa viti maalu kufikia asilimia kumi tu ya wabunge WAKUCHAGULIWA, kupunguza cost...
  2. tubakize nafasi za upendeleo kwa walemamu tu... hakuna sababu ya kuwa na viti maalum ya wanawake kwani WANAWAKE WANANWEZA, NA WANWEZESHDWA SANA TU SASA
  3. Nafasi za viti maalum zichanganuliwe kwa mtindo wa profession [au nyanja muhimu] kama vile afya, elimu, ulinzi na usalama, kilimo, sheria, madini, nishati, misitu, habari nk... ili kuongeza changamoto na profeissionalism kwenye bunge letu... huwa napata tabu sana kumsikiliza mwana kwaya komba na kuamini kama anaweza kuelewa mfumo mzima wa afya au nishati
  4. Rais abaki na nafasi zake 10

Nasema hivi kwasababu kubwa moja.... siku zote tangu nipate akili, nimekua nikisikia matatizo yasiyokwisha, mfano mimba za wanafunzi, MSD na tatizo la madawa, umeme na maji... naamini kabisa, kuongeza professionals kwenye bunge kutabadilisha mfumo wa vikao na kuleta tija zaidi....

siwadharau wasio na elimu kubwa lakini wakati umefika kubadili jinsi nchi inavyoendeshwa... nina imani kwamba hata awe kikwete, lipumba, slaa, nk... wote wanahitaji technical inputs kupanga sheria zruzi na zinazotekelezeka

NAWASILISHA
---
Habari waheshimiwa,
Najua mada hii inaweza kupokelewa kwa namna tofauti na baadhi yetu. Naomba radhi mapema. Ieleweke kuwa sijaandika kwa ajili ya kumdhalilisha yeyote, wala si kwa nia mbaya. Ni katika kuweka sawa pale ambapo naona kuna ulaghai wa wazi.

Kipindi cha nyuma niliwahi kuandika kuhusu dhana potofu kuwa viti maalum ni kwa ajili ya kuleta uwiano na vina maslahi gani kwa Taifa. Leo tena nimeona ni vema niongelee hili. Kimsingi ni kuwa hata baada ya kupita muda bado sijashawishika hata kidogo kuikubali dhana hii. Nitatoa sababu chache.

1. Kama viti hivyo ni kwa sababu busara za viongozi ziliamua kuwa kuna makundi maalum (mf. vijana) ambayo yanapaswa kuwakilishwa ni jambo zuri. Lakini kama kuna heri ndani ya hili wazo ni kwa nini wasiiweke hii nafasi iwe rasmi,vijana wagombee, sisi vijana tujichagulie wawakilishi wetu? Ni nani atanishawishi kuwa hao walioteuliwa ndiyo wawakilishi wetu? Kwani vijana wako hawapo? Hapa siwaelewi haraka!!!

2.Kama swala la msingi ni kuweka uwiano wa makundi ya wanawake kwa wanaume napo siyo mbaya. Lakini kama ni hivyo kwa nini nafasi hizo zisirasimishwe halafu tuwaache wanawake wajichagulie muwakilishi wao? Ni nani ataona nakosea kama nitakuwa na wasiwasi (not necessarily me) na jinsi wateule hawa wanavyopatikana?

Nani atanilaumu nikisema hii ilipitishwa ili kupata nafasi ya kuwapa ulaji tu wale wenzao ambao walikuwa pamoja kwenye harakati nyingine na wamekosa nafasi rasmi za kwapa ili kulipa fadhila? Ni nani anaweza kunishawishi kwa sauti, hadharani kuwa kuna utaratibu rasmi wa kuwateua hawa wateule? Na ni nani leo atalaumu kwa dhati kabisa, toka moyoni akisikia watu wanlalamika kuwa nafasi hizi wanawapa mahawara, wachumba, na ndugu zao?

Kama hili ni katika harakati ya kuweka usawa wa jinsia si neno pia. Lakini ninapata mashaka pale ambapo naona mazingira ya upatikanaji wa hawa Wabunge wateule yana utata. Mazingira haya yenye utata hayatapelekea Wanawake kutojikomboa tu ila yataendelea kuwadhalilisha na kuwafanya watumwa wa fikra na hoja za wengine ( waliowateua) Vinginevyo sioni jinsi mbunge teule anavyoweza kusimama na "kutounga mkono hoja 100%" ikiwa wale wa kuchaguliwa wenyewe wameamua kulinda shibe zao badala ya kuwawakilisha wananchi. Hiyo haitaleta usawa wowote! USAWA SAHIHI HUJA KWA MISINGI SAHIHI!

Siku moja nilikuwa nasoma moja ya hotuba ya hayati Mwalimu Nyerere alipokuwa akiwakumbusha Wanajeshi wetu majukumu.Akatoa mfano wa nchi ya marekani wakati wa kudai usawa kati ya wamarekani weusi na weupe. Ikafikia sehemu akatoa mfano wa kesi zilizokuwa zinaendeshwa mahakamani baada ya weusi kufanyiwa faulo mbalimbali. Unajua Mahakimu walikuwa wanaamuaje?

Wanamwita mweupe(mf George) wanamuliza "Bw. George kwa nini umemtemea mate huyu Ghachocha(mweusi)? Hujui kama kwa misingi ya katiba yetu yeye ni sawa na wewe? Haya nendeni,usimtemee tene mate huyu;mko sawa" Unajua nini kinafuata? Usishangae kuona hatua tano kutoka mahakamani ametemewa mate tena na kesi ikawa vilevile!

Labda ntawakera baadhi yenu lakini nakiri siyo lengo langu na naomba nisamehewe. Mpaka hapa mimi nimejifunza kuwa USAWA HAUOMBWI. Usawa huu mnaoutaka wenzetu haupatikani kwa kupitia migongo ya wanaume wanaotuhumiwa kuwanyanyasa.Badala yake mkitaka usawa wenye heshima onyesheni kweli kwamba mnaweza! Msipewe bure! Mkiona wametangaza nafasi na nyie kachukueni fomu.

Pigeni kampeni sambamba na wanaume.Mkishinda mtakuwa mmeweza. Mkipewa nafasi tu hapo siyo tu mtakuwa hamwezi bado ila pia mtakuwa mmejidhalilisha zaidi kwa kusubiri kumegewa,Na kwa hiyo mtakuwa hamjui mnafanya nini! Unajua ni kipi kibaya kuliko vyote hapo? Ni hiki kipengele cha kulipa fadhila kwa waliokumegeeni. Mtaendelea KUDHALILIKA TU.(Igeni kwa Hilary Clinton;wale wanaweza!).

Siyo Huko mjengoni tu,kote;mshuleni maofisini mitaani n.k. Mkisikia kuna nafasi 200 za sekondari wafundisheni binti zenu na wadogo zenu kuzipigania hizo 100. Na mkitaka kuonyesha mnaweza "kama wanaume" kama mnavyodai msikubali kushushiwa alama kwa kigezo cha kuwa wanawake.Mkikubali mwisho wa siku itakuwa kweli kuwa mlipeleka wasichana 100 wasio na sifa kwa vigezo ila walioachiwa tu na haohao wanaume ili tu mridhike mko sawa.Haya ni matusi na yataendelea hivyo mpaka muelewe tatizo liko wapi.Msitake kuwezeshwa kabisa!Vinginevyo huo usawa hautakuwa na heshima!Hii kaulimbiu ya kitoto ya "WANAWAKE WAKIWEZESHWA WANAWEZA"ifutwe kwani inawafanya dhalili zaidi.Kwamba bila huruma na fadhila za wanaume hamchomoki hapo.Mpaka muwezeshwe!USAWA HAUOMBWI.

Mkiona kuna kikosi cha wanajeshi kinajiandaa kwenda kwenye operationi ulizeni kuna wanawake wangapi wanakwenda? wako kwenye vitengo gani? Msikubali spicial treatment wala favours! Chukueni the same standard,no more no less.Hapa watawaheshimu.Lakini kabla ya 'kukagua majeshi' kakagueni mafunzo ili mhakikishe wanajifunza sawasawa na wanaume,No favours no special treatment. Ndugu zangu safari ya kudai usawa ina miiko.Kama mnanielewa hii ndiyo njia sahihi!

Kama nilivyosema awali, kwa mtizamo wangu hivi viti maalum havina maana.Vimelenga kubeba kundi fulani la marafiki ambao hawajapata nafasi rasmi serikalini.Ila kwa kuogopa upinzani usiseme na wao wakaruhusiwa! Hivi ni kweli kuna mtu anaweza kuniambia inakuwaje kuna MBUNGE wa VITI MAALUM VIJANA.Mbunge ambaye sisi vijana anaotuwakilisha hatujamchagua wala hatujashirikishwa uteuzi wake?

Au kuna mtu anajua imekuwaje Mbunge mteule James Mbatia ameteuliwa kuwa mbunge?( Brother James this is not personal please.) My logic is kama Mbatia kwa mfano tu, aligombea ubunge, wananchi aliokuwa anaomba ridhaa yao wakaona hatoshi, wakashindwa kumchagua, leo anateuliwa na rais akamwakilishe nani? Huyu alimteua (no offence) ametumia akili ipi? Huu Ni upuuzi!

Ni kweli kuna wanaosaidiasaidia lakini kwani hata wasiosaidia kwani wanawajibika kwa nani hawa? Ulisikia wana ofisi au bosi zaidi ya waliowateua? Labda tupate mfano; Mbunge wa viti maalum Mh.Mch.Dr. Lwakatare tangu ameingia bungeni hiyo awamu ya nne kuna aliyewahi kumsikia akichangia hoja yoyote ya msingi? Pamoja na u sifuri huo mbona bado karudi na kiti chake Maalum?

Hii ni hasara kwa taifa!.Mishahara nauli na posho jumlisha usafiri na mengineyo! Lakini si ni kweli pia kuwa hii nchi haina viongozi mwenye kuijali? Hasara hizi si za msingi Kabisa na zinauma kuzitafakari.!!!!
---
Habari za muamko Wana jamvi,

Niende moja kwa moja kwenye mada husika, binafsi nimekuwa nikikereka sana na hili Jambo"mbunge wa viti maalumu"daaah, hata kutamka hilo nahisi kichefuchefu kwakweli, tuna wabunge wa majimbo ambao pia niwawakilishi kwa Jimbo husika, bado tuna weka viti maalumu ambavyo kiujumla sioni chochote wanacho kifanya bungeni zaidi sana kula posho na mishahara monono nakupewa magari na 500lt za Diesel kwa mwezi na mwisho wa miaka mitano 230 ml Kama mafao, hii ndiyo Tanzania, najiuliza idadi ya viti maalumu bungeni ×kiasi Cha pesa kinacho tumika wakati vijijini Kuna mwananchi anaishi under 1$ per day,!!

Sent using Jamii Forums mobile app


1583400152061.png
===

MAONI YALIYOTOLEWA NA WADAU

Viti maalumu kwa tafsiri rahisi kabisa ni mpango mahsudi ambao unalenga kuwajengea uwezo kundi maalumu katika kushika nafasi mbalimbali katika ngazi ya maamuzi na uongozi.

mpango huo unalenga sana katika kupunguza na kutokomeza dhana za ukandamizaji wa kijinsia na makundi maalumu kwa kuwapa fursa ya kupata nafasi za usawia katika maamuzi mbalimbali na uongozi.

cha ajabu sasa tunawaona baadhi ya wawakilishi wetu kupitia viti maalumu wanaonekana kama hawajaielewa falsafa ya viti maalumu vizuri, maana mheshimiwa anapata fursa ya kuteuliwa mara ya kwanza….. tena kwa mara ya pili anapata bahati ya kuteuliwa tena….. lakini bado anakuwa hajajiamini na kujijengea dhana ya ushindani wajimbo. nilikuwa natoa tu kama angalizo kwamba inabidi serilikali iweke muda maalumu na kusiwe na firsa ya kujirudia mara mbili, na muwakilishi atayepata fursa ya kuteuliwa viti maalum afanyiwe majaribio baada ya kumaliza huo muda maalumu ili tuone kama dhana ya kmjenga katika kipindi alichopewa imemkaa?.

sina maaana ya kuvipinga viti maalumu, lakini je tunawasaidia au ndio tunawafanya wabweteke, binafsi nampenda sana mama kilango kwa ushupavu wake, na ninatamani sana wanawake wote wawe na ujasiri kama mama yangu huyu.

jamani viti maalumu ni chombo cha kutupa fursa na kujiandaa, sio tubaki hapo hapo. nimeshtushwa sana kusikia habari kuwa kuna mama yangu mwingine ambae nilikuwa nadhani na yeye atajitosa jimbo tena, sasa ametangaza kuwania apendekezwe viti maalumu…..??.

Pamoja na kuangalia yote hayo, watanzania tujitathmini tangu tumeanzisha viti maalumu je lile lengo letu tunafanikiwa? je wawakilishi wa viti maalumu wanaelewa kwa nini wamepata fursa ya kuwawakilisha watu maalumu katika viti hivyo maalumu??
---
Ni wazo zuri, binafc sikubaliani na suala la ubunge wa viti maalum kwani mchakato wa kuwapata kwa sehemu kubwa umegubikwa na utoaji wa rushwa ya ngono ndo mana wengi wao hawana impact yoyote si bungen wala mitaani wako kimaslah kuwafurahisha walowapa nafasi.

Tutumie mfumo wa majimbo ambapo mwanamke yeyote mwenye uwezo na uhitaji ataomba nafasi then watafanyiwa mchujo na mwisho watakaopita kwenye mchujo watapigiwa kura kumpata mbunge mwanamke wa jimbo husika, haya mambo ya kupeana ubunge wa ni udhalilishaji kwa wanawake wote Tanzania!
---
Siungi mkono hoja ya kutenga majimbo maalum kwa ajili ya wanawake kwakuwa wakazi wa majimbo hayo sio wanawake tu.
Siungi mkono kuwa na wabunge wawili kama ulivyopendekeza Ubungo, kwakuwa ni gharama zisizo na maana.

Ninachounga mkono ni kufuta kabisa Viti vya Upendeleo ingawa nyie mnaviita eti Maalum. Maalum kwa lipi? Kuna mbunge gani Maalum aliyefanya jambo maalum huko bungeni hata akastahili recognition? Upuuzi mtupu! Wanawake wanaohitaji ubunge wakachuane na wanaume huko majimboni.

Mbona wapo wengi tu waliofanikiwa kupata kura za kutosha majimboni na sasa ni wabunge wa majimbo.
---
Kwanza kabisa niwe wazi tu katika hili kuwa kitu tulichokikosea katika taifa letu ni kuwa na wabunge wa viti maalumu.hawa wabunge wamekua wa kwanza katika kutetea upumbavu ilimrad tu waonekane na wenyewe wamo.Mfano mzur ni hawa wabunge wa CHAMA CHA MAJANGA wanatia aibu bungeni,unakuta anatetea na kusema serikali ni sikivu wakati watanzania tunaona serikali ni KIZIWI.

CHAMA CHA MAJANGA kinawatumia sana hawa kujipigia kampen na wanasahau kuwa bungeni si sehemu ya kupeleka wapiga makofi tu bila kuwakilisha wananchi.Katika elimu pia WANASIFIKA KWA KUUNGAUNGA ILIMRADI TU WAWE NA SIFA YA KUPIGA DOMO KWA KISWAHILI KIRAHISI WAWE NA SIFA YA KUONGEA.WANALIPWA FEDHA NYINGI ZA WALIPA KODI ILA HAWANA MCHANGO WOWOTE.

PENDEKEZO
WABUNGE WOTE WAPIGIWE KURA NA WANANCHI NA MAMBO YA UVITI MAALUMU YASIWEPO ILI IKIFIKA MUDA WA KUJUA MBIVU NA MBICHI WANANCHI TUFANYE KAZI YETU.

ANGALIZO KWA CCM
HAKUNA CHAMA KILICHOTAWALA MILELE KAMA KIPO KINYUME CHA HAKI NA USAWA NA MIFANO IPO WAZI NA INAJULIKANA.MNACHOFANYA LEO KITAWA COST KESHO.

ANGALIZO KWA WABUNGE
USIFIKIRI KUTETEA CHAMA CHAKO ANGALI UNAUJUA UKWELI NA KUUPINGA KUTAKUSAIDIA KATIKA TAIFA LETU LENYE WATU WEREVU NA WALIOSOMA KWA MDA HUU.NAWE PIA NAKUHAKIKISHIA UNACHOFANYA LEO KESHO KITAKU COST NA WATANZANIA HATUTAKUA NA HURUMA KUMHUKUMU MWALIFU.

*TANZANIA MPYA INAKUJA*
---
SHILINDE,

1: Hii ni MIZIGO isiyo ya lazima. Kwani hawa wanawakilisha JIMBO GANI ikiwa wananchi wote wa jimbo fulani wanamchagua mwakilishi wao kwa kupiga kura?

2: Na je, kama ni mtu anafkiri waende basi kuwakilisha mbona hawaletwi kwa kundi wanalodaiwa kuwakilisha afu kundi hilo liseme kama linamkubali au laaa?

3: Hivi wa nyie mnaopewa izo nafasi bila kutoka jasho mnajiskia je kulipwa mamilioni kutokana na kodi za wavuja jasho nikiwemo mimi, wanaoteseka kwa mishahara ya TGSD?

4: Watu hamna udhaifu wowote wa viungo mnaitwa mnawakilisha "KUNDI MAALUM" what kind of maalum is this? Mbona sioni wanaume wanaowakilisha makundi maalum? Hakuna wanaume wenye wanaohitaji huo uwakilishi maalum?

5: Nafkiri huu umaalum huenda ni KA_MRIJA kalikobuniwa kumkaba zaidi mtu wa chini maana mi SIONI HAJA Ya wao kuwepo hali wabunge walopigiwa kura wapo, hawajashindwa kazi. Ni muda sasa na ni busara UMAALUM UACHWE ili hizo fedha zihudumie wananchi wa wanaowakilishwa na wabunge halali.

6: Afu inabidi tujifunze kwa wenzetu wa Afrika mashariki. Mi naona wenzetu wana mabunge madogo na wana MAENDELEO af wa TZ maskini af MATUMIZI YASIYO YA LAZIMA yako juu... This is senceless...

Mwisho kwa apa, kama wewe ni MTANZANIA unaeumia kuona nchi yako haisongi mbele miaka nenda rudi, chukua hatua ya kupinga "VITI MAALUM"
---
Mimi nakubaliana na wewe kabisa mkuu. Spirit ya kuwa na wabunge wa kuteuliwa ilikuwa kujaribu kuingiza wanamama strong kwenye system kama njia ya kuwawezesha, kwa sababu ku-compete kwenye majimbo ya uchaguzi na wanaume kwenye jamii ambayo ni gender biased ingekuwa vigumu. LAKINI LENGO LILIKUWA KUWAPA NAFASI WANAWAKE WENYE MTIZAMO WA KIMAENDELEO.

Sasa hawa wanaoingizwa sasa hivi hata mimi sielewi anaewaingiza humo bungeni. Ni wale wanaoenda kushindana kuvaa na kusukuma mikoko ya maana. Nchi haiendelei kwa kuagiza sana kutoka nje, bali kwa kuzalisha. Hii ni changamoto kubwa sana kwetu kwa sababu tunahitaji viongozi wa kike wengi tu (reasons are obvious, Madingi zetu walioko madarakani wametu-let down kwa kuwa wezi.

Wote ni wezi ambao kila mmoja anajitahidi awezavyo kuchota kwa ajili ya familia yake tu na wala hafikirii nchi itakuwa wapi 50 years later kila mtu akifanya hivyo). Sasa hatuwezi kuwa na wezi tupu kwenye safu ya uongozi!!! Wamama walau wana uoga kidogo. Nadhani wabunge wa kuteuliwa wateuliwe kwa kuwapima IQ kwanza!!! Sijui tufanyeje, lakini tunahitaji viongozi wanawake, kwa sababu nchi zote zenye maendeleo makubwa ya kiuchumi ni zile zilizowawezesha wanawake mapema.
---
Mdondoaji,
Well said mkuu!! Nimeuliza sana nini faida ya hivyo viti maalumu; mkuu Remmy akasema vinaleta uwiano wa kijinsi. Nikamuuliza kwani ni lazima kuwa na uwiano? Akasema haitaleta picha nzuri kwavile bunge litajaa wanaume!!. Hivi bunge likijaa wanaume wanaofanya kazi kwa manufaa ya taifa (ya watu waliowachagua) kuna ubaya wowote?!!? Au bunge lenye uwiano (wakiwepo wanawake) ambalo halina tija kwa taifa?!

Naona ameshakimbi tena.....

Hatuhitaji taifa lenye kujaa huruma kwa wanawake wasiokua na tija kwa taifa lenyewe; kama mwanamke anahisi anaweza kuwa kiongozi mzuri hazuiliwi kwenda kuomba kura na kuwashawishi wananchi kwamba anaweza kuwaongoza. Na si kukaa kusubiri kupewa ubunge wa bure husio na uwakilishi halisi na halali wa wananchi.
---
Wakuu yote haya yanakuja kwa kasi baada ya kazi hii ya ubunge kubadilishwa dhana kutoka kwenye ile ya uwakilishi kwa wananchi iliyokuwa na posho tu ya kutosheleza mahitaji muhimu ya mtumishi huyu wa wananchi mpaka kufikia sasa ambapo nafasi ya mtu kupata ubunge ni nafasi ya kuuaga umaskini kwani wanapata rundo la pesa, mishahara, marupurupu, na ahadi ya ya mafao ya kukufuru pale mwenye nafasi hii atakapokoma kuitumikia nafasi hii, na pia kwa hulka ya mabinti wengi ya uvivu wa kupindukia na ile fikra ya kwamba wao wanauwezo wa kutumia maumbile yao kwa vyovyote iwavyo ili kupata kipato kwani dhana yao ya kujaribu kushindana wao kwa wao na pengine kushindana na wanaume.

Kama ilivyo asili yao imekakamaa na kuitoa hiyo itachukua an effort to change their culture which is of the essence, ukweli uwekwe wazi kwa kuwapongeza wanawake wale wanaothamini haki sawa kwa kupigania hiyo haki kihalali na siyo kwa kujirahisisha rahisisha upande mmoja wanadai wako sawa na wanaume huku upande wa pili wnaregea regea na kugawa na kuumwaga utu wao bila kugundua ni namna gani utumwa huu wa kujitakia unavyo watawala na hautakuja kuondoka iwapo wao wenyewe ni rahisi rahisi na wa burebure namna hii.

Wagundue kwamba kila mwanamke mwenye uke asio uthamini atakapotumia hiyo ati nafasi kupata manufaa isvyo halali, hata wale wnaowatumia watakuwa na uchaguzi na kuwathaminisha kama vile iwapendezavyo na hii hali itaendelea mpaka wanawake wenyewe watakapoiga mifano ya wanawake ngangari kama Mh. Halima Mdee, Mh. Asha Rose Migiro na wengine wanawake ambao hawadeki deki ili waachiwe nafasi.

Historia inaonyesha viongozi na wale wenye heshima kimataifa mfano waziri mkuu wa Australia, Rais wa Liberia na wengine wako ngagari, akina mama tunawapenda sana, ni mama zetu, dada zetu n.k. lakini hili la ati viti maalumu kuwawakilisha mlikatae kwa sababu hao machangudoa wanawawakilisha kinyume nyume and it is really an anarchy!

VAENI NGUO ZENU ILI MPATE HESHIMA! DHARAU MNAJITAKIA WENYEWE KWA KUJIRAHISI!
---
Wabunge wa viti maalum ni kero kero kero. Na kipindi hiki wale wa viti maalum - CCM wanatisha. They look/behave kama vile wametoka red-district. It is sickening na historia itawakumbuka.

Kuhusu mwanasheria mkuu, nadhani kazi yake ibakie kuishauri serikali, na kwa vyovyote vile ASIRUHUSIWE ku-debate bungeni. Kazi yake itaishia kwenye baraza la mawaziri na sio hii ya kujibizana na wawakilishi wa wananchi. Kama wabunge wanataka ufafanuzi basi aitwe kwa utaratibu maalum lakini mwanasheria abaki ofisini kwake. Bunge ni kwa ajili ya wabunge na yeyote anayekwenda bungeni lazima apitie sanduku la kura. No exemption. Yule Mama albino kasaidiaje maalbino wengine kwa kuwepo kwake bungeni? Sanduku la kura. basi.
---
Huu ni ukweli usiopingika kabisa kwamba hizi ofa wanazopewa hawa kina mama wa CCM kuingia bungeni wanazitumia vibaya.

Mara nyingi nimekuwa nikuatilia vikao vya bunge,na kwa umakini niliougundua ni kwamba, wabunge hao wa CCM hawako mle ndani kwa ajili ya kutetea maslahi ya watanzania bali kwa ajili ya kulinda chama chao na wale waliowapa ofa..

Wamekuwa ndio chanzo kikubwa cha kuvuruga amani bungeni,huku spika wao akiwakingia kifua.
Kutetea hoja zisizokuwa na kichwa wala mguu..
Hakuna wanachojua zaidi ya umbea tu.
---
Katiba ya Tanzania ibara ya 66
66. Wabunge Sheria Na. 15 ya 1984 ib. 13; 4 ya 1992 ib. 18; 12 ya 1995 ib. 9; 3 ya 2000 ib. 9
(1) Bila ya kuathiri masharti mengine ya ibara hii, kutakuwa na aina zifuatazo za Wabunge, yaani–
(a) Wabunge waliochaguliwa kuwakilisha majimbo ya uchaguzi;
(b) Wabunge wanawake wa idadi inayoongezeka, kuanzia asilimia ishirini ya Wabunge waliotajwa katika aya ya (a), (c) na (d), itakayotajwa mara kwa mara na Tume ya Uchaguzi kwa taarifa itakayochapishwa katika Gazeti la Serikali baada ya kupata kibali cha Rais, watakaochaguliwa na vyama vya siasa vinavyowakilishwa Bungeni, kwa mujibu wa ibara ya 78, na kwa kuzingatia masharti ya uwiano wa uwakilishi baina ya vyama hivyo;
(c) Wabunge watano waliochaguliwa na Baraza la Wawakilishi kutoka miongoni mwa wajumbe wake;
(d) Mwanasheria Mkuu;
(e) Wabunge wasiozidi kumi walioteuliwa na Rais kutoka miongoni mwa watu wenye sifa kwa mujibu wa ibara ya 67, isipokuwa sifa iliyotajwa katika ibara ya 67(1)(b).
(2) Rais, Makamu wa Rais na Rais wa Zanzibar, kila mmojawao hatakuwa Mbunge.
(3) Endapo Mkuu wa Mkoa atachaguliwa kuwa Mbunge anayewakilisha wilaya ya uchaguzi au endapo Mbunge anayewakilisha wilaya ya uchaguzi atateuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa, Bunge litahesabiwa kuwa lina idadi ya Wabunge inayohitajika na shughuli zake zitakuwa halali ingawaje idadi ya jumla ya kawaida ya Wabunge kwa mujibu wa masharti ya ibara hii, itakuwa imepungua kutokana na uchaguzi huo wa Mkuu wa Mkoa au uteuzi huo wa Mbunge anayewakilisha wilaya ya uchaguzi.
 
Kwa hiyo tunavunja katiba? Kama tumefikia huko basi hali ni mbaya sana na hatuna watendaji wa kuwashauri kitaalamu wanasiasa wetu au wanasiasa wetu ni madikteta ambao hawakubali ushauri wa kitaalamu
 
Wamelifanya BUNGE letu kuwa kuubwa unnecessarily, mzigo mzito kwa walipa kodi wetu. Kazi yao kubwa kuunga mkono hoja.
 
Katiba hii hapa http://www.tanzania.go.tz/images/katibamuungano.pdf

Katiba ya 1977 toleo la 2000

SURA YA TATU

BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO

SEHEMU YA PILI

WABUNGE, WILAYA YA UCHAGUZI NA UCHAGUZI WA WABUNGE

Wajumbe wa Bunge

Wabunge

Sheria ya 1984 Na.15 Ibara 13 sheria ya 1992 Na.4 Sheria 1992 Na.4 Ibara 18 Sheria ya 1995 Na.12 Ibara 9
Sheria ya 2000 Na.3 ib.11

66.-(1) Bila ya kuathiri masharti mengine ya ibara hii, kutakuwa na aina zifuatazo za Wabunge, yaani-

(a) Wabunge waliochaguliwa kuwakilisha majimbo ya uchaguzi;

(b) Wabunge wanawake wa idadi inayoongezeka, kuanzia asilimia ishirini ya Wabunge waliotajwa katika aya ya (a), (c ) na (d), itakayotajwa mara kwa mara na Tume ya Uchaguzi kwa taarifa iliyochapishwa katika Gazeti la Serikali baada ya kupata kibali cha Rais, watakaochaguliwa na vyama vya siasa vinavyowakilishwa Bungeni, kwa mujibu wa ibara ya 78, na kwa kuzingatia masharti ya uwiano wa uwakilishi baina ya vyama hivyo;


(c) Wabunge watano waliochaguliwa na Baraza la Wawakilishi kutoka miongoni mwa wajumbe wake;

(d) Mwanasheria Mkuu;

(e) Wabunge wasiozidi kumi walioteuliwa na Rais kutoka miongoni mwa watu wenye sifa kwa mujibu wa ibara ya 67, isipokuwa sifa iliyotajwa katika ibara ya 67(1)(b)
.

(2) Rais na Makamu wa Rais kila mmojawao hatakuwa Mbunge.

(3) Endapo Mkuu wa Mkoa atachaguliwa kuwa Mbunge anayewakilisha wilaya ya uchaguzi au endapo Mbunge anayewakilisha wilaya ya uchaguzi atateuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa, Bunge litahesabiwa kuwa lina idadi ya Wabunge inayohitajika na shughuli zake zitakuwa halali ingawaje idadi ya jumla ya kawaida ya Wabunge kwa mujibu wa masharti ya ibara hii, itakuwa imepungua kutokana na uchaguzi huo wa Mkuu wa


Mkoa au uteuzi huo wa Mbunge anayewakilisha wilaya ya uchaguzi.
 
Viti maalumu kwa tafsiri rahisi kabisa ni mpango mahsudi ambao unalenga kuwajengea uwezo kundi maalumu katika kushika nafasi mbalimbali katika ngazi ya maamuzi na uongozi.

mpango huo unalenga sana katika kupunguza na kutokomeza dhana za ukandamizaji wa kijinsia na makundi maalumu kwa kuwapa fursa ya kupata nafasi za usawia katika maamuzi mbalimbali na uongozi.

cha ajabu sasa tunawaona baadhi ya wawakilishi wetu kupitia viti maalumu wanaonekana kama hawajaielewa falsafa ya viti maalumu vizuri, maana mheshimiwa anapata fursa ya kuteuliwa mara ya kwanza….. tena kwa mara ya pili anapata bahati ya kuteuliwa tena….. lakini bado anakuwa hajajiamini na kujijengea dhana ya ushindani wajimbo. nilikuwa natoa tu kama angalizo kwamba inabidi serilikali iweke muda maalumu na kusiwe na firsa ya kujirudia mara mbili, na muwakilishi atayepata fursa ya kuteuliwa viti maalum afanyiwe majaribio baada ya kumaliza huo muda maalumu ili tuone kama dhana ya kmjenga katika kipindi alichopewa imemkaa?.

sina maaana ya kuvipinga viti maalumu, lakini je tunawasaidia au ndio tunawafanya wabweteke, binafsi nampenda sana mama kilango kwa ushupavu wake, na ninatamani sana wanawake wote wawe na ujasiri kama mama yangu huyu.

jamani viti maalumu ni chombo cha kutupa fursa na kujiandaa, sio tubaki hapo hapo. nimeshtushwa sana kusikia habari kuwa kuna mama yangu mwingine ambae nilikuwa nadhani na yeye atajitosa jimbo tena, sasa ametangaza kuwania apendekezwe viti maalumu…..??.

Pamoja na kuangalia yote hayo, watanzania tujitathmini tangu tumeanzisha viti maalumu je lile lengo letu tunafanikiwa? je wawakilishi wa viti maalumu wanaelewa kwa nini wamepata fursa ya kuwawakilisha watu maalumu katika viti hivyo maalumu??
 
Wanajamvi,

Nimejaribu sana kuangalia na kutafakari sana mfumo wetu wa viti maalum... sijachukua reference ya nchi yoyote kwani sioni sababu na hasa ukizingatia kwamba our country is unique, blessed na inapitia kipindi kigumu cha mpito kwa kuondokana na dhana zama kwenda dhana halisia...

Ukiangalia hata mchakato unaotumika, kwangu mimi naona unanyima nafasi baadhi ya makundi hasa walio weledi kupita, kuchakachuliwa hadi kupata nafasi... teh current system [regardless of chama] imekua ni ya kupigia kura watu kutokana na popularity katika vyama rather than qualities.... si chadema, KAFU wala CCM walio na chakato wa kuridhisha kupata hawa watu... here are my proposals

  1. tupunguze idadi ya wagomea wa viti maalu kufikia asilimia kumi tu ya wabunge WAKUCHAGULIWA, kupunguza cost...
  2. tubakize nafasi za upendeleo kwa walemamu tu... hakuna sababu ya kuwa na viti maalum ya wanawake kwani WANAWAKE WANANWEZA, NA WANWEZESHDWA SANA TU SASA
  3. Nafasi za viti maalum zichanganuliwe kwa mtindo wa profession [au nyanja muhimu] kama vile afya, elimu, ulinzi na usalama, kilimo, sheria, madini, nishati, misitu, habari nk... ili kuongeza changamoto na profeissionalism kwenye bunge letu... huwa napata tabu sana kumsikiliza mwana kwaya komba na kuamini kama anaweza kuelewa mfumo mzima wa afya au nishati
  4. Rais abaki na nafasi zake 10

Nasema hivi kwasababu kubwa moja.... siku zote tangu nipate akili, nimekua nikisikia matatizo yasiyokwisha, mfano mimba za wanafunzi, MSD na tatizo la madawa, umeme na maji... naamini kabisa, kuongeza professionals kwenye bunge kutabadilisha mfumo wa vikao na kuleta tija zaidi....

siwadharau wasio na elimu kubwa lakini wakati umefika kubadili jinsi nchi inavyoendeshwa... nina imani kwamba hata awe kikwete, lipumba, slaa, nk... wote wanahitaji technical inputs kupanga sheria zruzi na zinazotekelezeka

NAWASILISHA
 
Tuufutilie mbali kabisa.....hauna maana...kwani wapiga kura ni wanaume tu majimboni? takwimu zinasema wanaume ni wachache kuliko wanawake sasa hawa wanawake wanaogopa nini kwenda majimboni?
 
Quoted as a fair user
The Boss,

Tatizo la mfumo wetu wa sasa ni kusikiliza kila presha group na kuwanyamazisha kwa viti maalum, kuna siku waweza sikia chama cha wala bata nacho kina kiti kimoja, chamudata kimoja, TFF kimoja, BASATA kimoja, TBF etc

we only need 10% ya special seats and it is for special people sio tu akina dada basi, sanasana ni kwenda kuwavunjia ndoa zao tu
 
Tumeona wanachama na wapenzi wa Chadema na hata vyama vingine wamefanya kile walichokiita "kulinda kura". Tumeona wameweza uzito kuwa wanataka kujua matokeo ya uchaguzi walioufanya na hatimaye hata maeneo ambayo yalionekana yangekuwa tete kama Nyamagana, Iringa na Arusha Mijini watu wameng'ang'ania hadi matokeo yamekuja.

Sasa kweli Chadema inapata viti vingi, na tetesi za ndani kura za Urais nazo zinatishia (hakuna cha 70- wala 80 percent) sasa Chadema itoe msisitizo wa kutaka kura zote zitangazwe mapema? Au wasubiri ile ya "kutangazwa na kuapishwa" hasa ukizingatia hadi jioni hii ya Jumatatu ni majimbo 31 ambayo yametangazwa rasmi kati ya majimbo 239.

Je matokeo ya kura za Ubunge tu yanatosha kuwafanya waridhike?
 
mwanakijiji justice delayed justice denied, hizi fujo zinazooneshwa StarTV zinadhihirisha kuwa kuna hitaji la kutangaza matokeo haraka sana!
 
Ni kukaba kote kote kwa kweli ubunge na uraisi hakuna haja ya kuwaamini CCM.
Brazil wako 201 mil wameshatangaza matokeo yao sisi watu 41mil imekuwa issue.
 
Kaka nguvu ya umma ndio yenye kuamua. Hakuna kulala mpaka kiieleweke. Kitu cha msingi ni kushinikiza tume itangaze matokeo kwa wakati ili wasipate nafasi ya kuchakachua kura.
Tunaipenda tanzania na tuna nia njema na Tanzania ndio maana tunataka mabadiliko yenye tija kwa Taifa letu
 
Mzee Mwanakijiji,

Nadhani uwajibikaji upande wa Tume ungeleta maana sana kuliko nguvu za umma hasa inapokuja kwa kura za urais..japo bad wananchi una sababu za kushinikiza NEC lakini sasa maandamano yanaanzishwaje kudai tume kwa matokeo ya urais wakati hata wabunge bado!

Au wagombea urais waanzishe kasheshe ya kutaka kura zao zitangazwe?All in all nguvu ya umma imeonesha kuwa kumbe mabadiliko tanzania yanawezekana na wanancho wetu tuliowadhania wamelala ucingizi kumbe waliamka siku nyingi wakawa wamekosa kiongozi mwenye karismma kama Slaa wa kuonyesha Kanani!
 
Mkuu hili nalo ni la kujiuliza kwa umakini sana maana mpaka sasa kwa kiasi fulani ukiangalia utaona kwamba kuna moto mkubwa sana wa kutaka Makamanda wa Chadema kusimamia kura kuhakikisha kwamba hakuna haki ya mtu ambayo inaibiwa.

Jambo nililoliona ni kwamba yanapotangazwa matokeo ya Ubunge kuna baadhi ya maeneo furaha ya ushindi inasababisha na hata morale ya ulinzi ipotee na watu warudi makwao. Sasa nakaa na kujiuliza je tunatakiwa kulinda kura zote za Chadema ama ni kura za Ubunge na Udiwani tu ndizo ambazo zinahitaji kulindwa?
 
Kweli swali zuri sana..
Mkuu wangu JK kachemsha, kisha shindwa sasa swala kubwa ni CCM Mtandao kukubali matokeo na kuachia ndilo lisilowezekana..Maadam haiwezekani hivyo basi tutatangaziwa JK ameshindwa kwa asilimia 51 hiyo Ijumaa na msafara tayari kwenda uwanja wa Tiafa kuapishwa kama ilivyofanyika Kenya...
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom