Vitendo vya dhuluma vinavyofanywa na wateja kwa madalali wa majengo na ardhi, nini kifanyike?

Nov 28, 2010
21
5
Heri ya Mwaka Mpya 2019!

Kwanza natoa pole kwa madalali mliodhulumiwa pesa zenu na wateja. Pia natoa pongezi za dhati kwa madalali wanaofanya kazi zao vizuri na kwa uaminifu. Kuna usemi usemao “Samaki mmoja akioza, wote watakua wameoza” kwa kutumia usemi huu, mimi napingana nao kidogo nikiuhusisha na biashara zinazofanywa na madalali wa Ardhi na Majengo. Wapo madalali waaminifu na wapo baadhi yao wasio waaminifu. Soko la milki kuu ni soko ambalo lina udhaifu mkubwa katika upatikanaji wa taarifa kibiashara, hivyo madalali wanafanya kazi nzuri sana katika kufanikisha kupatikana kwa taarifa ya mali inayouzwa au kupangishwa (Real Estate Market (s) is an opaque market, according to Efficient Market Hypothesis {EMH}. Real Estate Markets fall under “weak form of information efficiency” kwa hivyo madalali wanamchango mkubwa sana katika kufanikisha taarifa za ardhi na majengo zinapatikana kwa uharaka na ufanisi katika industry ya real estate, na tukumbuke daima milki kuu haiamishiki (Immobile asset). Binafsi ninafanya biashara ya uwakala wa majengo na ardhi (Real Estate Agency), na maranyingi hua nashirikiana sana na madalali wa sehemu mbali mbali katika kufanikisha biashara zangu/zetu, ningependa ku share experience.

Kwa nini madalali wanadhulumiwa?

i.Kutokua na mikataba ya kimaandishi baina yao na wamiliki wa mali au mnunuzi/mpangaji au upande unaotoa maelekezo (instructing party). Dalali (broker)/Agent (wakala) hua ni mtu wa kati baina ya anaeuza/kupangisha na mnunuzi/mpangaji wa jengo au ardhi. Dalali au wakala hulipwa kamisheni kutokana na kazi aliyofanya kwa makubaliano baina yake na mwenye mali au mhitaji/mnunuzi/mpangaji. Kiwango cha kamisheni kinaweza kuwa katika muundo wa asilimia au kiwango maalumu cha fedha mtakachokubaliana.

ii. Msululu wa madalali katika biashara moja (Chain of brokers). Utakuta biashara moja ina msululu wa madalali mpaka hata kumi mara pengine, kwa mazingira hayo, hali ya kudhulumiwa ina nafasi kubwa zaidi, kuliko wakiwa wachache, hata mazingira ya kudhulumiana wenyewe kwa wenyewe hutokea pale mnapokuwa wengi katika biashara moja.

iii. Hulka ya kudhulumu, kuna wateja imekua ni tabia zao kudhulumu, hawezi kufanya biashara na dalali pasipo kumdulumu, ni tabia ya ubinafsi na kudhulumu.

iv. Hakuna chombo au baraza au taasisi inayosimamia maslahi ya madalali/mawakala wa majengo na ardhi.

v. Kutokuanza kazi kwa sheria mpya za milki kuu (Real Estate Laws);
a). Estate Agency Act, 2015 ambayo bado ni muswada “A bill for the Estate Agency Act, 2015” hii ndio itakayozungumzia kila kitu kuhusu madalali na mawakala wa majengo.
b). The Real Estate Act, 2017 ambayo pia bado ni muswada “The Real Estate Bill, 2017”.

vi. Kuna baadhi ya madalali wakipewa kazi ya kuuza mali au kupangisha huwa na tabia ya kuongeza bei sana, na hivyo kupelekea mazingira magumu ya biashara na hii huchangia sana mazingira ya kudhulumiwa endapo biashara ikifanyika. Haiwezekani upate sawa na mwenye mali, haipo hii mahala popote na kama ipo ni mara chache sana kutokea. Ushauri tu kiwango cha kamisheni hakitakiwi kuzidi asilimia kumi (10%) ya bei ya mauziano (1%-10%).

Kwa ufupi tu, hata kama sheria zikipitishwa na kuanza kufanya kazi, pia ni wajibu wetu kuzisoma sheria na kuzielewa ili tuweze kuzijua haki zetu za msingi na kuweza kuzitetea pale zinapokuwa kwenye mazingira ya kudhulumiwa.

Nini kifanyike?

Maoni yangu ni kwamba, badala ya kusubiri mpaka sheria zipitishwe na kuanza kazi, ni vyema sisi wenyewe kujiandaa na kujipanga vyema, mfano; kutumia platforms kama hizi group za WhatSapp kwa sababu taarifa inamfikia kila mmoja kwa urahisi na haraka. Kujadili na kuona namna ya kuanzisha na kusajili “Association of Real Estate Agents in Tanzania” ili sheria zitakapokuja, zitakuja Kuunda bodi za usajili (Estate Agency Board and Real Estate Regulatory Board) hivyo sheria zitatukuta tumeshajiandaa.

Karibuni kwa majadiliano yanayojenga!
 
Hii kali dalali kudhurumiwa.tatizo wengi awajasajiliwa wanafanyia kazi vichochoroni.sehemu inauzwa mara 2 hata hujui kwa kumpata.
 
Mbona zipo ofisi za real estates wanafanya kazi za real estate agency, sema umeeleza vizuri uwepo wa mkataba wa kazi, hapa ndiyo haipo bongo. Watu wanafanya upangishaji kiholela holela.
 
Back
Top Bottom