Vitendo vinavyokatazwa kwa mujibu wa Sheria ya Gharama za Uchaguzi namba 6 ya 2010

Shadida Salum

Journalist at JamiiForums
Sep 11, 2020
69
104
Kwa mujibu wa Sheria ya Gharama za Uchaguzi namba 6 ya mwaka 2010;

Kifungu cha 24, kifungu kidogo cha 2 kinaeleza kuwa; Mgombea yeyote, awe yeye mwenyewe au wakala wake au chama chake, akifanya kitendo ambacho kimekatazwa kama ilivyoelezwa sehemu hii, atakuwa amekosa sifa ya kushiriki kwenye mchakato wa uteuzi au uchaguzi.

Vitendo vilivyo katazwa vinaelezwa kwenye kifungu cha 21, kifungu kidogo cha 1 na kifungu cha 22 ,kuwa mtu atakua amefanya kitendo kilichokatzwa pale ambapo;

A) Mtu yeyote ambaye kabla au wakati wa kampeni, moja kwa moja au la, atatoa au kukubaliana kutoa au kuazimisha, kuahidi kununua au kutoa pesa kwa mpiga kura kwa nai ya kumshawishi kumpigia kura au kuacha kupiga kura.

B) Kila mmoja aidha moja kwa moja au la,yeye mwenyewe, wakala wake au chama chake cha siasa kikanunua au kuahidi kununua au kutoa ofisi, sehemu au ajira kwa mpiga kura kwa nia ya kumshawishi kupimpigia kura au kuacha kupiga kura.

C) Kila mtu, ambaye kabla au kipindi cha kampeni moja kwa moja au la, yeye mwenyewe, wakala wake au chama chake cha siasa kikatoa zawadi, mkopo au ahadi kwa nia ya kuweza kuteuliwa kugombea nafasi ya udiwani, ubunge au urais.

D) Kila mtu ambaye kwa matokeo ya zawadi, mkopo, ahadi au manunuzi atatoa nafasi au kumteua mtu kuwa mgombea wa udiwani,ubunge au urais.

E) Kila mtu ambaye kwa dhumuni la kuhamasisha mchakato wa uteuzi au kampeni, au kipindi cha uteuzi au kampeni, akalipa au kusababisha kulipwa pesa yoyote kwa lengo la kuwa pesa hizo au baadhi ya pesa hizo zitatumika kama hongo kwenye mchakato wa uteuzi.

F) Kila mpiga kura ambaye,kabla au wakati wa uteuzi au kipindi cha kampeni moja kwa moja au la, yeye mwenyewe au mtu mwingine kwa niaba yake akapokea, kukubali kupokea pesa, zawadi, mkopo au ajira kwa ajili yake au mtu mwingine kwa ajili ya kupiga kura au kukubali kupiga kura au kuacha kupiga kura kwenye uteuzi au uchaguzi.

G) Kila mmoja ambaye ,baada ya uteuzi au uchaguzi ,moja kwa moja au la, yeye mwenyewe au mtu mwingine kwa niaba yake, akapokea pesa yoyote kwa kua mtu huyo alipiga kura au hakupiga kura au kwa kumshawishi mtu mwingine kupiga kura au kuacha kupiga kura.

Aidha kifungu cha 22 kinaeleza kuwa;

a) Kila mtu ambaye kwa njia ya rushwa, yeye mwenyewe au mtu mwingine kwa niaba yake kabla au wakati wa uteuzi au uchaguzi, moja kwa moja au la, akatoa au kulipia, yote au sehemu ya gharama za chakula, vinywaji au burudani, kwa nia ya kumshawishi kumpigia kura au kuacha kupiga kura wakati wa uteuzi au uchaguzi.

b) Kila mmoja ataepokea chakula, vinywaji au burudani kama hongo.

Mgombea hatokuwa na hatia na vitendo vilivyokatazwa kwenye Sheria ya Gharama za Uchaguzi, viliyofanywa na chama chake cha siasa bila matakwa yake au kuridhia kwake yeye mgombea iwe moja kwa moja au la.
 
Kama Mahakama zikiwa huru, Jiwe atatenguliwa hata akishindishwa.
 
Awamu ya 5 sheria zote zinatungwa, zinasimamiwa na kutekelezwa na mtu mmoja ambaye pia ni kiongozi wa malaika... Mwenye Madara ya kulevya... Mtukufu!!
Hivyo vifungu unavijua wewe... Usitake kututisha!!
"Posti Kwa Hisani ya Mataga" cc jingalao johnthebaptist, etc
 
kumbe Lisu tumeamua kumsamehe tu naamini Mungu atatulipa kwa hili
 
Back
Top Bottom