Vitasa vya Azam Tv: Kuna maneno ya kukufurisha mule, tuwe makini

Trainee

JF-Expert Member
Sep 22, 2018
1,123
2,000
Nadiclare interest kwanza.

Mimi ni mwananchi wa kawaida kabisa mwenye elimu ya kidato cha nne japo ni mwalimu wa shule ya msingi pia maarufu kama "fom foo felia". Ni Mwislamu ninayependa kufuatilia sana dini

Niingie kwenye mada sasa.
Kuna vipindi vingi kwenye television na radio mbalimbali ambavyo vimekuwa vikipendwa sana na watu. Kupendwa huko kunatokana na sababu mbalimbali ikiwemo matangazo, maudhui ya kipindi uendeshaji wake warusha matangazo wenyewe kaulimbiu pamoja na maneno maneno yanayochomekezwa humo.

Sasa pamoja na kupendwa kote huko ila kuna baadhi ya vitu vinajitokeza kwenye vipindi hivyo ambavyo ni kinyume na maadili ya Kitanzania. Ukiangalia Azam utakutana na vimaneno vya ajabu ajabu tu kwenye matangazo ya (kipindi cha) Vitasa ambapo yawezekana vingine usijue maana yake.

Kwa kufupisha tu ni kwamba pamoja watu kupenda ngumi kama mchezo wa burudani ila ukiangalia vitasa vya azam utaona kwenye matangazo yao wamechomekeza vimaneno maneno na mbwembwe nyingi halafu mwisho kabisa wa tangazo kuna msela anasema "amituofo"

Sasa neno hilo (japo yawezekana nimekosea kuliandika) ukilifuatilia utakuta linatumika kutukuza mungu wa Kibudha. Kwa faida ya wale wasiojua ni kwamba kuna dini ya kibuda imeenea sana China na India ambayo wanaabudiwa masanamu ya watu wanaoaminika kufikia level fulani ambayo ukifikia hapo unakuwa sawa na mungu na ndipo utaitwa budha. Yaani kuna Mabudha wengi ambao huabudiwa na kuaminika au kuitwa sawa tu na mungu mfano kuna god of infinite, god of light nk.

Sasa unaporusha rusha mateke kisha ukataja neno hilo tunashindwa kuelewa uhusiano wa mangumi na neno ambalo ni la kiibada kwa upande wa watu wa China. Yaani ni sawa na mtu aruke ruke hapo halafu aseme allahu akbar au tumsifu yesu kristo au haleluya; sawa hatutashangaa lakini si ni pale ambapo yupo ndani kwake anafanya mazoezi binafsi!!! Sasa pale ni tangazo je kuna maana gani?

Nawaasa watu wawe makini na hizi burudani kwani kumekuwa na tabia ya kuingizia vimaneno maneno vingi ambavyo siyo vya kawaida (Kiswahili kigumu) na hata vya kigeni (lugha za kigeni) ilimradi tu kupotosha watu. Pia Mambo mengi yanayopingwa katika jamii yanahalalishwa kwa mbinu ya mlangonyuma Fuatilia muziki muvi na hivyo vipindi utaelewa tu nisemacho.

Mfano mmoja tu kipindi cha shilawadu kilikuwa ni maalumu kwajili ya kuhalalisha umbea na kusengenya, jambo ambalo hakuna jamii ya kitanzania inayolikubali

Kwa upande wa muziki angalia wimbo unaitwa "watakubali" angalia namna mbosso anavyowaaminisha watu kuwa kukaba ni jambo la kawaida na kuhalalisha kabisa ukabaji kuwa kazi kama kazi nyingine.

Kwenye muvi ndo hata hakuelezeki yaani yaleyale ya Hollywood, Bollywood na Nollywood ndo yamehamia Bongo.
 

MakaDik

Senior Member
May 31, 2019
123
225
Kwangu Binafsi Umeeleweka Isipokuwa Kwa Habari Ya Dini Wapo Ambao Watafurahia Tu Hayo Kwa Kuwa Ni Waumini Au Wanaoikubali Dini Hiyo. Wabudha Tunao Wengi Tu Hapa Tz Nadhani Hasa Wahamiaji Kwao Hayo Ni Halali.

Ni Kweli Vyombo Vingi Vya Habari Mambo Yaliyomo Yana Utofauti Sana Na Utamaduni Wa Kiafrika Lakini Ni Vigumu Kubadilisha Kwani Maisha Tunayoyaishi Kwa Sasa Mengi Yameathiriwa Na Utamaduni Wa Kimagharibi Hivyo Wakati Fulani Kwa Masuala Haya Ya Mabadiliko Ukiona Unaelemisha Hueleweki Kwa Wengi Basi Fuata Lako Au Simama Kwa Miguu Yako Kwenye Imani Yako
 

mkorinto

JF-Expert Member
Jun 11, 2014
21,056
2,000
Chukulia mambo easy tu,furahia maisha

Anyway nyie ni wale walimu wanoko mashuleni
Bila hawa inawezekana shule zote zingekuwa vituo vya kubadirishana tabia za ajabu ajabu.

Kuna mwalimu alizushiwa amefariki shuleni kwetu 1 April, shule nzima ikaripuka kwa furaha. ajabu saa mbili tunaona anakingizana skuli kwa madoido.

Mpaka nimekua ndio najua alikuwa napigania tabia zetu, wala sio kutafuta sifa.
 

Hazard CFC

JF-Expert Member
Apr 7, 2015
15,623
2,000
bila hawa inawezekana shule zote zingekuwa vituo vya kubadirishana tabia za ajabu ajabu.

kuna mwalimu alizushiwa amefariki shuleni kwetu 1 April, shule nzima ikaripuka kwa furaha. ajabu saa mbili tunaona anakingizana skuli kwa madoido.

mpaka nimekua ndio najua alikuwa napigania tabia zetu, wala sio kutafuta sifa.
Ni kweli mkuu
 

Demi

JF-Expert Member
Nov 22, 2016
23,588
2,000
Kupenda kwako dini kumekuathiri ndugu. Vipindi ulivyovizungumzia havina uhusiano na dini yoyote,na ukumbuke kuwa kila mtu ana dini yake. Unacomplicate mambo.
 

Jumong S

JF-Expert Member
Jul 3, 2013
6,295
2,000
Sasa c ukasikilize TV Imaan, channel nyingine hazikuhusu unafungua za nn?
 

kalonji

JF-Expert Member
Feb 17, 2021
1,261
2,000
Freemason ndo wanacontrol akili za watu kupitia media.Tazama tamthilia zote si za kiswahili,kichina, kihindi, korea,kiingereza lengo kuu ni kubomoa Jamii, kuchochea ubinafsi, maisha ya vitu kuliko utu. matusi kama mbwa, mjinga, mshenzi, mpumbavu, kwa sauti za ukali ni jambo la kawaida.

Na wateja wakuu wa hizi tamthilia ni wanawake nao uzipractize kwenye maisha yao kwenye ndoa zao zile ni roho chafu usambazwa duniani kupitia tv lengo kuu ni kuibomoa Jamii.
 

Mshuza2

JF-Expert Member
Dec 27, 2010
8,249
2,000
Broo iko hivi,chochote kile unachoangalia au kusikiliza kwa maana ya redioni au kwenye runinga, mpaka kwenye hizi social media kote huko kumejaa propaganda za kukushikia akili ili usiwaze vizure..usiwe na matumizi mazuri ya akili!

Mbaya zaidi kama uko kiimani basi utapata shida sana..coz kote huko ni mwendo wa kumtukuza shetani kwa asilimia kubwa..kazi kwako kupanga ni kuchagua!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom